Hivi Kuna Ugonjwa Wa mtu kupenda Maji kupita Kiasi?

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
44,583
188,793
Habari.

Kuna hili jambo ambalo limenishangaza kidogo baada ya kukutana na watu wa namna hii.

Mtu kupenda maji kupita kiasi nikiwa na maana ya kuyashika/kugusa mwili wake muda mwingi.

Madaktari na wataalamu hebu karibuni kutupa maelezo ya mtu kuwa na tabia ya kupenda maji kupita kiasi kama ni kuoga anaweza kuoga hata siku nzima ili awe na maji muda wote.

Nawasilisha.

Cc: Kichwa Kichafu
 
Kama Huo ni ugonjwa upo kwangu, hasa kwenye Maji ya kunywa

kwenye kuoga tena kukiwa na Shower ndio kabisaa... sijui ni kwa sababu gani basi tu najikuta napenda maji
 
Hali ya Hewa itakuwa inakusukuma kufanya hivyo....
 
Mmh sidhani sana maana nikiwa kwenye Halijoto au Halibaridi Routine yangu ya kunywa maji ipo hivi, Asubuhi nikiamka lita moja, saa 1-3-5-9-11 au siku ingine 2-4-6-8-10-12 Lazima ninywe maji sana hapo, siwezi kuacha...yaani hata nikiwa sina kiu nakunywa mpaka kiwango wanachoshauri kwa siku... Changamoto nipatayo labda ni route za msalani kila mara (kitu ambacho kwangu ni normal)

Kwenye kuoga ndio usiseme yaani kwangu kungekuwa na Swimming ningekuwa nalala huko😂
 
Wapo wengi tena huanzia utotoni wanasema mara nyingi ni wale ambao Nyota zao zipo kwenye kundi la Maji, kama nyota ya Samaki (Pisces) au nyota ya Nge (Scopio).
 
Mmh sidhani sana maana nikiwa kwenye Halijoto au Halibaridi Routine yangu ya kunywa maji ipo hivi, Asubuhi nikiamka lita moja, saa 1-3-5-9-11 au siku ingine 2-4-6-8-10-12 Lazima ninywe maji sana hapo, siwezi kuacha...yaani hata nikiwa sina kiu nakunywa mpaka kiwango wanachoshauri kwa siku... Changamoto nipatayo labda ni route za msalani kila mara (kitu ambacho kwangu ni normal)

Kwenye kuoga ndio, yaani kwangu kungekuwa na Swimming ningekuwa nalala huko
Unaifahamu nyota yako?
 
Mmh sidhani sana maana nikiwa kwenye Halijoto au Halibaridi Routine yangu ya kunywa maji ipo hivi, Asubuhi nikiamka lita moja, saa 1-3-5-9-11 au siku ingine 2-4-6-8-10-12 Lazima ninywe maji sana hapo, siwezi kuacha...yaani hata nikiwa sina kiu nakunywa mpaka kiwango wanachoshauri kwa siku... Changamoto nipatayo labda ni route za msalani kila mara (kitu ambacho kwangu ni normal)

Kwenye kuoga ndio, yaani kwangu kungekuwa na Swimming ningekuwa nalala huko😂

Hapo sawa kaka...wewe sio mlevi wa maji...maana umesema unakunywa kwa kiwango kinachohitajika.

Huko kuongelea na kuoga....punguza, fanya tu kwa kiwango cha kawaida...tusije haribu ngozi.🙃😉🙃😉
 
Sawa Dada, ila nisipokunywa maji nahisi mwili mzito na kuchoka
 
Naelewa na hata nikiwa addictive/mlevi sioni tabu maana maji sio sumu
Kuna uwezekano maji yakawa sumu kwenye mwili iwapo utazidisha, halafu figo ishindwe kuyachuja kuwa mkojo kulingana na ile kasi unayokunywa.....kila kitu kwa kiasi broh!
 
Wapo wengi tena huanzia utotoni wanasema mara nyingi ni wale ambao Nyota zao zipo kwenye kundi la Maji, kama nyota ya Samaki (Pisces) au nyota ya Nge (Scopio).
Mimi hata sijui nina nyota gani ila nachojua mimi na maji ni tofauti kabisa.
Afadhali kunywa najikongoja ila kuoga sijui kufua ni wito kwa kweli.
Kuna mchuchu mmoja aliwahi kunipiga chini akanitangazia kwa wenzie eti mimi nina harufu ya beberu mzee!...ndio sasa hivi najitahidi walau baada ya siku mbili tatu nakumbuka kuoga.
 
Daaah!
 
Back
Top Bottom