Hivi kuna sababu gani za kupost/kuweka picha za watoto wetu mitandaoni?

Hii ishu ghafla imehama imekua uhasama sijui wapi huu uzi umejikwaa.
 
mkuu hata mimi ni mmoja kati ya wasiopenda hyo tabia,si tu ya watu wangu wa karibu hata zinazohusu fargha zangu au maendeleo yangu labda picha ya kawaida tuu,inaaminika mtu akiku wish kitu kibaya just kwa husda kulingana na neema uliyo nayo au akiku wish kitu kizuri maombi yake huwa yanafika kwa haraka zaidi,ni kama maombi ya mtu aliyedhulumiwa kitu fulani alafu akaomba kwa Muumba wake,Atajibiwa kwa haraka sana,sasa si kila kitu unachomiliki ni lazima ulimwengu ujue,neema pia inaweza kuwa janga ingawa ukisema hivi wapo watakaohusisha na imani za giza,lakini ukweli hauko hivo,ndio maana unaambiwa ukimtendea mtu wema kesho utaongezewa haimaanishi kuwa yule uliyempa atakuongezea vingine,hapana! Maombi yake mema juu yako kwa kile ulichomsiadia yatafika moja kwa moja kwa Muumba kwa kua amekuombea toka moyoni kabisa kulingana na ulichomsaidia,
Na unapopata na neema fulani wapo wanaoomba kwa dhati ile neema iondoke katika milki yako au uendelee kuongezewa,tusipende sana kuanika kila kitu mitandaoni hasa watoto nk,maisha ya ki celebrity kwa maisha yetu ya uswahilini yanaweza kuwa na madhara,utakuja wakati hadi mtu alivyokuwa ana doo na mtu wake tutakua tunaona mitandaoni maana sasa hivi huo ulimbukeni ndo umeshamir ukitaka kujua mtu ana maisha gani usihangaike kumuuliza we nenda mitandaon hasa facebook utayaona
 
Hata haya pia yananihusu tena sana ndio maana nashughulika nayo maana miongoni mwa majukumu ya mtanzania mzalendo ni pamoja na kuwaelimisha wajinga wasio jielewa,kwa kudhani kuwa maisha yao hayawahusu watu wengine wakati toto lako likiwa jizi linaiba na kwa jirani halikuiibii wewe peke yako hivyo tambua jukumu la malezi ni la yeyote anaye ona anaweza kutoa mchango
Kumbuka mzazi una 75% za kumjenga mtoto kitabia na hizo 25% zilizo baki ndio za watu kama sisi na tabia chafu za mwanao hazi kudhuru peke yako bali zitaigharibu jamii nzima na taifa kwa ujumla hivyo usiwe mbishi kwa uvivu wako wa kufikiri.
Koma kumuita mtoto wangu toto, hajafikia hizo level. Wewe km una matoto it's up to you. By the way, I am done
 
Hahahaaa wewe nawe ni wakujiangalia kama uko sawa kiakili , hata mimi sina shida maisha yako kichekbob hayo ya vichochoroni na kingine ambacho nataka nikutoe ushamba na ulimbukeni wako ikiwezekana na ujinga pia ni kwamba kujifunza si lazima ujifunze kwa anaye kuona au anaye kufahamu ndio maana unasoma quraan au biblia na kuiamin kama muongozo wako lakin walio iandika huwajui na hujawahi kuwaona nahutawaona kamwe , lakin pia hadi leo tuna tumia theory za wasomi wa zaman ambao hatujawahi kuwaona lakin zinasaidia kuleta maendeleo , khaaaaaaa!!! Nimepata mashaka makubwa sana na upeo wako wa mawazo kwa comment yako hiyo ,inawezekana kabisa wewe upo darasa la tatu maana hata akili bado haijakomaa , shame! Jifunze maisha wewe acha kuishi kama mtu usiye na maono ya mbali
Niache, yes sina shule kichwani. Ww inakuhusu nini? Niache na ulimbukeni wangu mxiiiew
 
Kweli wewe ni litoto sasa hata ukipost mwanao anakunya nani ana hasara!!? Zaid zaid hasara itakuwa kwa huyo mtoto ambaye kwa sasa hana nguvu ya kuhoji ujinga wa mama yake anaye dhani matumizi ya socialmedia ni kupost picha za watoto tu, ulimbukeni na ujinga + ushamba kumbe nao ni kipaji aisee.
Ndo nna post
 
Hahahaaa unaringia kuzalishwa chini ya 16yrs we kweli ****! Wenzio tuna watoto sio vitoto kama wewe, habari ya vitoto wapekeelee sungura na nguruwe hukooo!! Ni kazi ngumu mno kumuelimisha kihiyo maana kihiyo hata jambo dogo ambalo halihitaji ufafanuzi yeye kwa ukihiyo wake atahitaji ufafanuzi zaid ya mara 10000000000 lakin bado hata elewa aisee kaaaaazi kwelikweli!!
Najua inakuuma ila kubali hali yako
 
Koma kumuita mtoto wangu toto, hajafikia hizo level. Wewe km una matoto it's up to you. By the way, I am done
Hahahaaa ni halali wewe kujiona una mtoto kwa akili yako ilivyo kiduchu bado hujui kutofautisha mtoto na litoto na litakuwa litoto kweli kama ukiendelea kuamini kuwa hakuna wa kukushauri wala wakukuingilia kwenye malezi teh!
 
Upo sahihi ...lakini kuna option mbili SHARE WITH PUBLIC & ONLY ME
Unachozungumziwa hapa ni kushare picha za watoto na siyo kuhifadhi maana unaweza kuhifadhi picha kimyakimya
kimya kimya alaf akiwa mmkubwa uanze kazi ya kumwonesha? ukifariki katikati
 
Niache, yes sina shule kichwani. Ww inakuhusu nini? Niache na ulimbukeni wangu mxiiiew
Usiwe mkali ukweli unaoo kuingia hahaja sindando imekuchoma kweli kweli ya imeingia chwiiiiii!! Pole weee!ulimbukeni wako usiuhamishie kwa watoto kufanao mwenyewe ati.
 
Sidhani kama ni tatizo, kila mtu na uhuru wake, labda kama wewe umeliona tatizo hapo.
Mkuu Athari Hasi Ya Kuweka Picha Ni Ipi? Coz Umeilezea Kwa Wanasiasa Tu Lakn Wapo Public Figure Wengi Kama Wanamusik Na Wengine Kama Hao.

Kwasisi Tusio Maarufu Nini Shida
Matatizo ya kuzaliwa mwaka arobaini ndio haya.Time zimechange acha watu wajivunie uzao wao.
Wacha wawaweke tu bana wakiharibu shauri yao
pilipili ya shamba mkuu wewe inakuwashia nini,zaa wako umuweke stoo

USHABIKI!!

Ushabiki wowote ni uwendawazimu,Uzwaza,Umaamuma na Unazi.Ushabiki unaweza kuwa wa Kiimani,Kimichezo,Kidini,Kikabila,Kitumwa nk.Mtu yeyote anayeshabikia lolote pasipo kuhoji,Kudadisi,Kusaili si mtu timamu,ni goigoi ambaye lolote kwake ni sawa tu.Hili halihitaji uzamivu kulitambua.Kwanini tunakuwa Mashabiki pasipo kujiuliza kwa kina,Kudadisi tunachoshabikia na kuwa na majibu mapana juu ya tukishabikiacho?.

Huku kote ni kufeli kwa taasisi ya kifamilia,Kiimani,Kijamii na hata kitaifa.Mzazi ni shabiki wa utamaduni fulani na haelewi lolote juu ya Utandawazi na athari zake,Je kama haelewi hili ni lini utamweleza kuwa hili ni jema na hili siyo jema akakuelewa?.Hivi tunafahamu dhana nzima ya matumizi sahihi ya Mitandao ya kijamii au kukurupukia tu vitu pasipo kujiuliza?.Ingia google na utaelewa.Hata Mark (Muasisi mmojawapo wa mtandao mkubwa wa kijamii) analishangaa sana hili la matumizi mabovu ya mtandao lakini sisi ndiyo kwanza hatuhoji,hatudadisi,hatusaili nk.Mwisho wa siku tunaishia kuwa na majibu mepesi juu ya maswali magumu tunayoulizwa kama baadhi ya majibu ya washiriki hapo juu.HUU NI USHABIKI.

Hivi ni kwanini tunapenda kuyageuza maovu kuwa mema na mema kuwa kinyume chake?.Maana haswa ya kupewa UTASHI na mwenyezi Mungu ni ipi kama mambo mepesi kama haya tunashindwa kuyangamua na kutoa maelezo ya kina juu ya Mustakabali wa Jamii na Taifa kiujumla?.Mbona tunazidiwa akili na paka wafugwao majumbani na bado tunajiona tuko sahihi?.

Yaani tupo radhi kuukumbatia uzwaza wetu kwa hali na mali na akitokea mtu wa kutueleza lililo jema tuko radhi tumtoe macho,Ni kwanini hivi?.Kwanini hatuko radhi kukaa na mapokeo yenye Staha njema na kuachana na hivi vikolombwezo vinavyoambatanishwa na utumwa mamboleo?.

Katika Saikolojia kuna kitu kinaitwa Defensive Mechanism (google it).Katika hili kuna dhana ya Replacement ambayo mhusika hudhihirisha upumbavu wake kwa kutafuta mbadala wa jambo fulani ambalo anadhani litamletea faraja ya moyo wake kumbe siyo.
Kwa mfano,Kama wewe ni wa mwisho darasani basi unaji-defense kwa kuwa mbabe kwa wenzio nje ya darasa,kuwa na wanawake wengi nk jambo ambalo kimsingi ni ujinga tu.
Basi kwa dhana hii hata hawa wanaowa-expose watoto wao katika mitandao ya kijamii nao wanaji-defense kwa upuuzi tu usio na maana.Pengine ndiyo siku ya kwanza kumvisha mwanae mavazi ya kimagharibi,Kumpeleka kwenye hoteli za kibepari nk hivyo akifanya hivyo ni unazi tu.

Hivi ulishawahi kujiuliza madhara ya kisaikolojia atakayoyapata mtu ambaye hakuwahi kuwaza kumiliki simu siku akimiliki anakuwaje?.mtu Kama hukuwahi kuwaza kuwa na Smartphone,Je siku ukiipata utaifanyia kazi gani zaidi ya KU-POSTujinga?.Kama ndiyo kwanza una wiki baada ya ku-join Fb,Whatsap nk unadhani utapost nini wakati huna lolote unalolifahamu?.

Kitu chochote kama hakina faida kwanini tukifanye?.Unamuweka mkeo/Mmeo kwenye DP halafu wenzio wakimkwapua unaanza kuja kulia humu,Why?.Unamu-expose mwanao kila uchwao MITANDAONI halafu akishaanza kupatwa na matatizo yasiyotatulika unaanza kumtafuta mchawi nani,Umesahau kuwa mchawi ni wewe?.

Halafu kwanini tuseme kuwa ni maisha ya mtu hivyo tumuache atakavyo?.Mbona kuna idadi ya kuzaa China na hakuna anayevunja sheria kwa kusema kuwa ni maisha yake?.Mbona Korea kaskazini kuna Sheria kibao za Mavazi,Mienendo nk na hakuna anayevunja kwa kusema kuwa ni maisha yake?.Kwanini sisi tudai kuwa ni maisha yetu wakati ni mmomonyoko mbovu wa maadili?.Hivi leo mwanao unayemuweka Insta kuwa ni mzuri,Je akibakwa na waliomuona ni mzuri hilo ni tatizo lako pekee?.

I stand to be corrected,Nb;Nikosoe kwa hoja na siyo Kishabiki.
 
Ndugu this life is too short let them appreciate and cherish what they have, you live only once [HASHTAG]#YOLO[/HASHTAG]
 
Najua inakuuma ila kubali hali yako
Hali gani bidada!? Nina watoto ati. Tena wa haja na ndio maana sina haja ya kuwatangaza mitandaoni kusubiri watu wawa thaminishe kama matunda sokoni na kuanza kuwasifia sijui kuwajadili hahahaa!! nadhani watoto wenu ni kama bidhaa sokoni inayo hitaji matangazo na mabango lukuki, shame!! Kwa staili hiyo naona mna waandaa mavideo qweeens /king hivyo mnawatafutia masoko mapemaa na sura zao za ajabu ajabu kama zenuzenu, ¥£§π~¢℅π§¿€¥€¢£
 
Hahahaaa ni halali wewe kujiona una mtoto kwa akili yako ilivyo kiduchu bado hujui kutofautisha mtoto na litoto na litakuwa litoto kweli kama ukiendelea kuamini kuwa hakuna wa kukushauri wala wakukuingilia kwenye malezi teh!
Wewe ni wa kupimwa akili wala siyo bure, kama una ushauri wa maana si uzae wa kwako? Au unadhani mtoto anapatikana tu kama mdoli?
 
Mkuu, tatizo la watu wengi kuwa 'vichwa maji', yani watu hawana content za kutosha alafu wanajilazimisha kupost vitu kwenye mitandao so unakuta anapost kitu icho hicho kila mara na vingine vinavuka mipaka. Wanachotakiwa kufanya ni kusoma sana vitabu mbali mbali na magazeti na kusikiliza habari ili kupanua ufahamu. There after unakuwa na vitu mbali mbali vya kupost kwenye mitandao ya kijamii.
ni ngumu kuelewa lakini kimantiki mtoto wako siyo wakuexpose kwa kila mtu! na kumsifia kwa uzuri wake! umakini na tabia za mtoto hutokana na maisha aliyoyaishi akiwa na wazazi wake! mpe mtoto vitu mhimu ktk maisha yake na siyo sifa za mitandaoni! kaa na mwanao mwambie ana kwa ana nataka uwe hivi na hivi hiii inamtosha kudraw atyention yake kwa yale unayomwbia.
somo zuri sana!!!! utasikia kama kaenda kununua shoes za mtot mliman city ili watu wajue kuwa kanunulia pale utaskia hapohapo anamfotoa akiwa kajaribu anarusha fb, inst, whtp n.K utaskia ma angle agrysh!! si ulimbuken huO jaman mbona hawapigag Na kupost wakiwa wamefilicka???
Kila jambo lifanywe kwa kiasi, privacy ni character muhimu kwa binadamu mwenye utashi kamili, family events kv birthday etc timely/rarely zinaweza wekwa online,mtoto hajafikia umri wa maamuzi huenda angekuwa mkubwa hata asingetaka hicho unachomfanyia AFA kumweka mitandaoni is concerned

Thank you sana Ma-GREAT THINKERS,YOU THINK BEYOND.
 
Hahahaaa ni halali wewe kujiona una mtoto kwa akili yako ilivyo kiduchu bado hujui kutofautisha mtoto na litoto na litakuwa litoto kweli kama ukiendelea kuamini kuwa hakuna wa kukushauri wala wakukuingilia kwenye malezi teh!
Wewe ni wa kupimwa akili wala siyo bure, kama una ushauri wa maana si uzae wa kwako? Au unadhani mtoto anapatikana tu kama mdoli?
 
USHABIKI!!

Ushabiki wowote ni uwendawazimu,Uzwaza,Umaamuma na Unazi.Ushabiki unaweza kuwa wa Kiimani,Kimichezo,Kidini,Kikabila,Kitumwa nk.Mtu yeyote anayeshabikia lolote pasipo kuhoji,Kudadisi,Kusaili si mtu timamu,ni goigoi ambaye lolote kwake ni sawa tu.Hili halihitaji uzamivu kulitambua.Kwanini tunakuwa Mashabiki pasipo kujiuliza kwa kina,Kudadisi tunachoshabikia na kuwa na majibu mapana juu ya tukishabikiacho?.

Huku kote ni kufeli kwa taasisi ya kifamilia,Kiimani,Kijamii na hata kitaifa.Mzazi ni shabiki wa utamaduni fulani na haelewi lolote juu ya Utandawazi na athari zake,Je kama haelewi hili ni lini utamweleza kuwa hili ni jema na hili siyo jema akakuelewa?.Hivi tunafahamu dhana nzima ya matumizi sahihi ya Mitandao ya kijamii au kukurupukia tu vitu pasipo kujiuliza?.Ingia google na utaelewa.Hata Mark (Muasisi mmojawapo wa mtandao mkubwa wa kijamii) analishangaa sana hili la matumizi mabovu ya mtandao lakini sisi ndiyo kwanza hatuhoji,hatudadisi,hatusaili nk.Mwisho wa siku tunaishia kuwa na majibu mepesi juu ya maswali magumu tunayoulizwa kama baadhi ya majibu ya washiriki hapo juu.HUU NI USHABIKI.

Hivi ni kwanini tunapenda kuyageuza maovu kuwa mema na mema kuwa kinyume chake?.Maana haswa ya kupewa UTASHI na mwenyezi Mungu ni ipi kama mambo mepesi kama haya tunashindwa kuyangamua na kutoa maelezo ya kina juu ya Mustakabali wa Jamii na Taifa kiujumla?.Mbona tunazidiwa akili na paka wafugwao majumbani na bado tunajiona tuko sahihi?.

Yaani tupo radhi kuukumbatia uzwaza wetu kwa hali na mali na akitokea mtu wa kutueleza lililo jema tuko radhi tumtoe macho,Ni kwanini hivi?.Kwanini hatuko radhi kukaa na mapokeo yenye Staha njema na kuachana na hivi vikolombwezo vinavyoambatanishwa na utumwa mamboleo?.

Katika Saikolojia kuna kitu kinaitwa Defensive Mechanism (google it).Katika hili kuna dhana ya Replacement ambayo mhusika hudhihirisha upumbavu wake kwa kutafuta mbadala wa jambo fulani ambalo anadhani litamletea faraja ya moyo wake kumbe siyo.
Kwa mfano,Kama wewe ni wa mwisho darasani basi unaji-defense kwa kuwa mbabe kwa wenzio nje ya darasa,kuwa na wanawake wengi nk jambo ambalo kimsingi ni ujinga tu.
Basi kwa dhana hii hata hawa wanaowa-expose watoto wao katika mitandao ya kijamii nao wanaji-defense kwa upuuzi tu usio na maana.Pengine ndiyo siku ya kwanza kumvisha mwanae mavazi ya kimagharibi,Kumpeleka kwenye hoteli za kibepari nk hivyo akifanya hivyo ni unazi tu.

Hivi ulishawahi kujiuliza madhara ya kisaikolojia atakayoyapata mtu ambaye hakuwahi kuwaza kumiliki simu siku akimiliki anakuwaje?.mtu Kama hukuwahi kuwaza kuwa na Smartphone,Je siku ukiipata utaifanyia kazi gani zaidi ya KU-POSTujinga?.Kama ndiyo kwanza una wiki baada ya ku-join Fb,Whatsap nk unadhani utapost nini wakati huna lolote unalolifahamu?.

Kitu chochote kama hakina faida kwanini tukifanye?.Unamuweka mkeo/Mmeo kwenye DP halafu wenzio wakimkwapua unaanza kuja kulia humu,Why?.Unamu-expose mwanao kila uchwao MITANDAONI halafu akishaanza kupatwa na matatizo yasiyotatulika unaanza kumtafuta mchawi nani,Umesahau kuwa mchawi ni wewe?.

Halafu kwanini tuseme kuwa ni maisha ya mtu hivyo tumuache atakavyo?.Mbona kuna idadi ya kuzaa China na hakuna anayevunja sheria kwa kusema kuwa ni maisha yake?.Mbona Korea kaskazini kuna Sheria kibao za Mavazi,Mienendo nk na hakuna anayevunja kwa kusema kuwa ni maisha yake?.Kwanini sisi tudai kuwa ni maisha yetu wakati ni mmomonyoko mbovu wa maadili?.Hivi leo mwanao unayemuweka Insta kuwa ni mzuri,Je akibakwa na waliomuona ni mzuri hilo ni tatizo lako pekee?.

I stand to be corrected,Nb;Nikosoe kwa hoja na siyo Kishabiki.
Ndugu yangu watanzania wengi uwezo wao kufikiri ni umbali wa 2cm pekee ndio maana wanaona ni salama tu, wanasahau kuwa hapa anaye tetewa ni mtoto asiye na haki kuhoji kwa nini anawekwa mitandaoni maana kesho na kesho kutwa ndio viongozi wetu wa kitaifa hao walio wengi wa watanzania wafikirirr huko kote wao wanadhan ataendelea kuwa mtoto tu na hato kuwa ndio maana kwa sassa hawainu ubaya wa kupost picha mitandaoni
 
Usiwe mkali ukweli unaoo kuingia hahaja sindando imekuchoma kweli kweli ya imeingia chwiiiiii!! Pole weee!ulimbukeni wako usiuhamishie kwa watoto kufanao mwenyewe ati.
Nadhani unapaswa kuishi bila kutumia internet ndio nitakuona wewe kweli si limbukeni.

Unafiki umekujaa tu, mtu akikuuliza role model wako utamtaja Christian Ronaldo na ukienda Facebook Ronaldo anashare picha mpaka za mamanyake mzazi akiwa na bikini.

Fala kabisa wewe.
 
Najaribu kufikilia kama ni kweli wajomba,mababu,ma baba mdogo,kaka zetu mashemeji zetu wanaowabaka watoto zetu kama ni kweli chanzo ni media sipati jibu.

Najaribu kufikilia wale watanzania wenzetu wanaoangaika mitaani wengine ni vichaa kama chanzo ni media sipati jibu.

Najaribu kufikilia kama ni kweli kabla ya media watu walikuwa hawarogani wala kuoneana wivu hata kuuwanaa sipati.

Ngoja kwa sababu Jf ni AKILI KUBWA lazima ntapata majibu wacha niwe mpole.
 
Back
Top Bottom