Hivi kuna sababu gani za kupost/kuweka picha za watoto wetu mitandaoni? utakuta wa kike kawekwa na maneno ya kumpamba kama
beautiful/cute/queen/mrembo wangu.
Wakiume: HB/ Prince /kidume changu
Mtoto anatakiwa kufunzwa kuanzia mdogo kabisa kuhusu faragha yake, nini cha kusema au kutoa na nini asiseme au asitoe. Hii ni pamoja na kwenye mitandao ya kijamii, simu na huduma nyingine za mawasiliano.
Umeshawahi kuona wanasiasa wanaweka picha za watoto wao au ndugu zao wa karibu kwenye mitandao hasa ya kijamii?Unajua ni kwanini?
Kwasababu kila anachofanya yeye kinamwathiri mtoto wake au watu wake wa karibu kwa ubaya au uzuri. Ni rahisi kuweka rehani faragha za watoto na ndugu zake.Kama ni mtoto wa kike anaweza kuanza kufuatiliwa na mabazazi kwa sababu ya picha tu. Watatafuta anapoishi, shule anayosoma na usishangae siku moja akabakwa.
Kwa hisani ya mwananchi tunapata elimu kwanini hii tabia imezuka sana wanandoa siku hiyo hiyo mama anaugulia maumivu badala ya baba kumhangaikia mama na mwanae yeye anafuta kamera iko wapi tena siku hizi mchina amerahisisha anamfotoa mtoto na kupost kwenye wall yake ili iweje? kwamba watu wajue na wewe ni kudume cha mbegu au una kizazi?
Matokeo yake ndo wazazi mnapotofautiana na marafiki zenu mnawatukana mpaka watoto, kuna wengne sijui mtandao gani yule dada anauza pichu anamtukana mtoto wa mwenzaje eti baboon hivi mnahisi watoto wanajisikiaje? unamharibia mtoto future yake bila kujua, ukifikiri ni fahari kuweka picha ya mwanao sijui facebook, twitter, instagarma na kwingne huko ni ushamba na ujinga, labda siku hizi kwa kuwa imekuwa issue sana kupata mtoto!
Badilikeni!