Hivi kuna propaganda iliyofanikiwa kwa miaka ya karibuni kuzidi "Ruto must go"?

Hivi kuna propaganda iliyofanikiwa kwa miaka ya karibuni kuzidi "Ruto must go"?

MR BINGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2016
Posts
1,208
Reaction score
2,591
Nchini kenya kumekuwa na maandamano ya kila mara yaliyoibuka kuanzia Rais William Ruto alivyoingia madarakani na yamekuwa yakishinikiza mambo mbalimbali yanayofanywa na Ruto na tukumbuke kuwa Ruto aliingia madarakani September 2022 na maandamano ya kwanza yalikuwa March 2023.

Kwa kipindi hicho kifupi nadiriki kusema kuwa maandamano mengi yaliyoandaliwa Nchini Kenya kuanzia wakati huo mpaka sasa mengi yana influence ya watu nyuma kisiasa walioweza kuwatengenezea "ideology"(propaganda) wakenya na katika hilo nadhani wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani vijana wengi kwa kujua au kutokujua wamekuwa wakishiriki na wengine hadi kupoteza uhai wao kisa maandamano haya.

KWA NINI NASEMA MAANDAMANO HAYA NI PROPAGANDA

1.YALIANZA KIPINDI KIFUPI SANA BAADA YA RUTO KUINGIA MADARAKANI
Ndani ya kipindi cha chini ya miezi sita tu kilitosha kuwafanya wakenya waone Ruto siye Raisi anayewafaa....hili lina ukakasi kidogo maana ndani ya miezi sita ni vigumu sana kuelewa utendaji kazi wa Raisi na kuweza kumuhukumu kama Ruto anavyohukumiwa

2.AINA YA MAADUI WA KISIASA ALIO NAO RUTO
Ruto alishinda uraisi mbele ya Raila Odinga ambaye alikuwa benet na Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi huo(kwa anayejua influence ya hawa watu wawili anaweza kuelewa Ruto maadui zake ni wa aina gani japo kwa sasa Odingo ni kama yuko neutral)

Aliyekuwa makamu wa Raisi wa Ruto,Mzee Gachagua pia naye amekuwa adui namba moja wa Ruto baada ya kuwa impeached na Bunge la Kenya na amekuwa akimtuhumua katika majukwaa kadha wa kadha bwana Ruto

3.MTIZAMO WA WAKENYA WENYEWE KUHUSU UCHUMI WA KENYA SASA HIVI NA KIPINDI CHA NYUMA
ukiangalia kwenye haya maandamano watu wanaosema Ruto must Go wanakubali kuwa Kenyatta alikuwa mwizi kupita Ruto na uchumi ulikuwa mbaya kipindi cha Kenyatta kuliko sasa hivi(ila wanadai Kenyatta alikuwa anajua kuwatuliza😅)

4.UKABILA
Hapa sina maelezo mengi Zaid ya kusema kuwa Ruto hatokei kwenye mojawapo ya makubwa mawili Nchini Kenya kitu kinachomuongezea maadui
 
Back
Top Bottom