Hivi kuna mradi mkubwa wa umwagiliaji kuliko wa Hombolo bwawani uliopo Dodoma?

uroto

JF-Expert Member
Jun 25, 2015
442
227
Habari wanajamvi,kama kichwa kinavyojieleza,ukitoa ule mradi wa mto Nile,
kwa hapa Africa kuna mradi mkubwa na ulio bora kuliko uliopo Hombolo bwawani Dodoma?

karibuni hombolo kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji (Irrigation)
siyo zabibu tu,hata nyanya,bamia,mihogo,mbogamboga nk.
 
Acha maskhara wewe, hicho kimfereji cha maji chumvi ndiyo mradi mkubwa?
Tembea uone ndugu yangu
 
Kuna gharama gani za kuchangia hapo ili uweze kupata eneo la kufanyia kilimo?? au ni bure??

Kila mwenye shamba hulipia 10000 kwa mwaka,ila ndani ya mradi wengi wa wageni hukodisha,na mradi umepewa namba,
kwahyo shamba moja unakuta ni heka moja na nusu
 
Habari wanajamvi,kama kichwa kinavyojieleza,ukitoa ule mradi wa mto Nile,
kwa hapa Africa kuna mradi mkubwa na ulio bora kuliko uliopo Hombolo bwawani Dodoma?

karibuni hombolo kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji (Irrigation)
siyo zabibu tu,hata nyanya,bamia,mihogo,mbogamboga nk.
Kilimo hicho kinasaidiaje kuondoa njaa Dodoma na Tanzania kwa ujumla? Au Ni msaada wa mboga kwa eneo Dogo tu?
 
Labda tu niseme huu mradi wengi wao wamejikita katika kilimo cha zabibu ambacho soko lake halina utata tofauti na mazao mengine,,

kwa mfano nyanya,bamia na mbogamboga ni mazao ambayo ukienda sokoni na 500 utarud nyanya,chainiz na bamia,maisha yatasonga

ila wanunuzi wanaotoka mijini,hununua kwa mfano debe la nyanya 12,000 yeye akienda anauza 22,000-25,000

mwisho wa siku wakazi wa hombolo magari,pikipiki si ndoto kwao,na hii inatokana na mradi tu
 
Tupatie maelezo zaidi au weka namba yko tukucheki mkuu

Mleta mada mi naona ungeweka, vitu muhimu zaidi ya kutaka kujua tu kama kuna mradi mkubwa zaidi ya huu ulioueleza, tuwekee bei ya kukodi shamba na gharama nyingine pamoja na mategemeo baada ya mavuno, itasaidia kwa ataependa kuwekeza huko"
 
Wakuu kama kuna yeyote humu anaepafahamu vizuri tafadhali atupe maelezo kwa kina ama kama kuna yeyote anaeweza kuwa mwenyeji wangu aje PM tuyajenge aliyeleta mada inaonesha kuna kitu hataki tukipate
 
Mleta mada mi naona ungeweka, vitu muhimu zaidi ya kutaka kujua tu kama kuna mradi mkubwa zaidi ya huu ulioueleza, tuwekee bei ya kukodi shamba na gharama nyingine pamoja na mategemeo baada ya mavuno, itasaidia kwa ataependa kuwekeza huko"

Ndugu ndani ya wiki hili nitafuatilia huu mradi kwa kina na nitaanika kila kitu ha jukwaani maana ni mradi nilioufikiria kwa muda
 
Back
Top Bottom