Makusudically
JF-Expert Member
- Feb 3, 2014
- 2,203
- 1,235
Wako baadhi ya watu ambao bila aibu wanahangaika na kumlazimisha Mkuu wa Mkoa wa Dsm aitwe Daud Albert Bashite, badala ya Paul Makonda. Sijui wanapata wapi mamlaka na sheria ipi inawaruhusu kufanya hayo, na najiuliza kuna tija gani kwa Watz kuhangaika na vyeti vya Rc Makonda? Wapo pia wenye mawazo finye wanalazimisha hoja kuwa, kwa vile tu JPM alianzisha uhakiki wa vyeti feki hivyo lazima na Rc Makonda ahakikiwe. Lakini hawajiulizi? Mwanzilishi wa Uhakiki ni JPM na siyo Gwajima au mtu mwingine yeyote, sasa iweje leo watu wasiokuwa na mamlaka ya uhakiki walazimishe kumhakiki Rc Makonda? Je JPM hakujua kuwa Rc Makonda hana vyeti? Hadi asubili Watu wapembeni kama Gwajima wapayuke ? Na wengine watumie tu-Mb twao kupost mitandaoni? Kwanini Watanzania tusijishughulishe na mambo yenye tija kama "Ugeni kutoka Ethiopia ambao unaleta tija na ajira nyingi kwa Watanzania? Ujio wa mwekezaji Dangote, Uthubutu wa kudhibiti usafirishaji wa mchanga wa madini usiokuwa na tija kwa nchi, JPM kudhibiti uhuni wa kuendeleza mikutano isiyokuwa na kikomo nchi nzima ? .Haya ni baadhi tu ya mambo ambao Wtz wapendao kupost mitandaoni wanatakiwa kufanya, badala ya kupost mistari miwili, Bashite, au Vyeti, tabia ambayo ni ya Kishetani. Tuweni Wazalendo hata kama kwa bahati mbaya tuliyekuwa tunampenda kura zilipungua. Tuwe kama Tundu Lisu ambaye kwa sasa ameamua kumkubali JPM kuwa ni Rais mahili na anafaa kuiongoza Tz, ndiyo maana amesema anaomba kukutana naye, na hakuthubutu kusema anataka kukutana na Rais Uchwara kama alivyokuwa akidai hapo awali. Big up Lisu kwa kutambua kosa lako na kukubali kuwa JPM ni Rais sahihi kwa Watz.