Hivi kugoma ni haki ya kikatiba kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kugoma ni haki ya kikatiba kweli

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by chumvichumvi, Mar 22, 2012.

 1. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  nilikuwa nasoma katiba siku chache zilizopita ili hali kutafuta kipengele kinachosema migomo au mgomo ni haki ya mwananchi wa Tanzania sasa cjui ni overlook as hicho kipengele sikukiona instead niliona kimoja kilichosema right to assemble ambapo tafsiri yake kwa haraka haraka naweza sema ni haki ya kukusanyika je kunatofauti gani kati ya kukusanyika na kugoma kama hamna migomo itakuwa ni haki ya nini au haki inayotokana na sheria zipi?​
   
 2. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  au katika nn ilo swala limezingumzwa
   
 3. M

  Mtoa Mada New Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani, katiba ni sheria ambayo inatoa mwongozo juu ya sheria nyingine zote ambazo kwa kuzihesabu ni zaidi ya 500. Sasa si lazima kila kitu kielezwe kwenye katiba na zaidi ni katiba hii hii ndio inayotoa mamlaka ya sheria nyinginezo kufanya kazi na watu kuzifuata ilimradi hazipingani nayo, sasa kwa hoja ya mgomo ktk katiba imeelezewa haki ya mtu kujieleza na kuwasilisha maoni(right to freedom of expression) chini ya ibara ya 18, na kama ni mgomo wa wafanyakazi sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, Sura ya 366 kama ilivyorudiwa mwaka 2004 imeeleza chini ya kifungu cha 75 kuhusu haki ya mfanyakazi kugoma kufanya kazi au mwajiri kugoma kutoa kazi kwa mfanyakazi wake ili mradi afuate procedures zilizowekwa.
   
Loading...