Hivi kosa la CCM ni kuaminiwa na Watanzania, au ni lipi?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kila siku nasikia vilio kwamba CCM inaminya upinzani tena wengine kama akina Tundu wanasema kwamba Bungeni CCM wanatumia wingi wao kupitisha mambo, hivi kosa la CCM hapo ni lipi?
Ni kushinda uchaguzi na kuwa Wabunge wengi kuliko wa Upinzani au ni nini?

Kuna tatizo gani CCM kutumia wingi wao ambao sisi wananchi ndiyo tumewapa kwa maana ya kuwaamini kupitisha mambo wanayoona yana manufaa?

Kama chadema na Wapinzani wengine mna shida na hilo, kwa nini msishinde kwanza uchaguzi na kuwa na Wabunge wengi ili msiburuzwe kwa wingi wa CCM?
 
Kila siku nasikia vilio kwamba CCM inaminya upinzani tena wengine kama akina Tundu wanasema kwamba Bungeni CCM wanatumia wingi wao kupitisha mambo, hivi kosa la CCM hapo ni lipi? Ni kushinda uchaguzi na kuwa Wabunge wengi kuliko wa Upinzani au ni nini?

Kuna tatizo gani CM kutumia wingi wao ambao sisi wananchi ndiyo tumewapa kwa maana ya kuwaamini kupitisha mambo wanayoona yana manufaa?

Kama chadema na Wapinzani wengine mna shada na hilo kwa nini msishinde kwanza uchaguzi na kuwa na Wabunge wengi ili msiburuzwe kwa wingi wa CCM?
Wapinzani hawana ushawishi kwenye kushinda!
 
Hivi ccm imeanza lini kuaminika, labda unamaanisha inaaminiwa na dola kwa maslahi ya watu fulani
 
Hivi ccm imeanza lini kuaminika, labda unamaanisha inaaminiwa na dola kwa maslahi ya watu fulani

Inaaminika kwa maana ina Wabunge 200 dhidi ya umoja wa upinzani 80, hivyo hakuna kipimo kingine zaidi ya hicho na mengine yote ni porojo tu!
 
Znz iliaminika lini?, kila siku Chama kinawekwa kwa nguvu ya dola

Hilo unasema wewe, isitoshe Zanzibar ni sehemu ndogo sana ya TZ na hata kama kuna matatizo lkn haibadilishi ukweli kwamba TZ Bara CCM imepata Wabunge sana na imeiacha Upinzani kwa mbali sana!
 
Hakika ya wachache kusikilizwa inakiukwa.....kumbuka kama haki hii ingedharauliwa 1992 basi ww mwenyewe usingefanya haya unayoyafanya sasa
 
Kushinda ccm ni kazi kubwa kwa sababu uamuzi haufanywi kwenye sanduku la kura bali nyumbani kwa akina JECHA. Wabunge wachache wa upinzani waliopenya ni wale ambao wapiga kura walivimba ile mbaya kulinda matokeo, wale walioachia akina JECHA ilikula kwao miccm ikachuka ushindi wa mezani.
 
kudanganya WATANZANIA.

CRtWHzpW0AABAon.jpg

swissme
 
Inaaminika kwa maana ina Wabunge 200 dhidi ya umoja wa upinzani 80, hivyo hakuna kipimo kingine zaidi ya hicho na mengine yote ni porojo tu!
Okay sehemu walizoshinda lindi mtwara mwanza ndipo wanashinda viti vingi je maeneo hayo yapo vipi?elimu ya wapiga kura maendeleo yao yapo vipi?mkuranga na majimbo mengi wamegawana na upinzani
 
Okay sehemu walizoshinda lindi mtwara mwanza ndipo wanashinda viti vingi je maeneo hayo yapo vipi?elimu ya wapiga kura maendeleo yao yapo vipi?mkuranga na majimbo mengi wamegawana na upinzani

Hiyo haijalishi, demokrasia maana yake wengi wape, au maamuzi ya wengi, hata kwa Wazungu ni hivyo, waliomuingiza Obama Ikulu siyo matajili upper middle class, bali ni masikini yaani watu wa daraja la chini kwa USA ambao wanaishi ghetto, wengi wao hawana Elimu ya kutosha hivyo hawana uwezo wa kupata kazi za kipato cha juu ...
 
Wapinzani hawana ushawishi kwenye kushinda!

Ccm iliwahi kushinda uchaguzi gani? Au ule wa Jecha? Kwa kumbukumbu zangu na ushuda wa usimamizi wa chaguzi zote za nchi hii toka 1995 hadi huu wa mwisho ccm haikuwahi kushinda.

Huwa wanabebwa tu na wasimamizi wa chaguzi hizo tena kwa vitisho vya hali ya juu. Tatizo dola ndio yenye kugawa ushindi kama zawadi na uoga wa dola kupoteza kazi na ulaji wao ndio waliotufikisha hapa.

Jambo ambalo lipo mbali na uelewa wa wengi ni kuwa kwenye semina za uchaguzi kuna semina nyingine ndani yake wanayopewa wasimamizi wakuu ambao wengi wao ni wakurugenzi wa mini na majiji ambayo neno ccm kushindwa huondolewa kwenye fikra zao na badala take ushindi wa kishindo wa namna nyingine hupandikizwa mioyoni mwao.

Laiti kazi zao zingekuwa za kuomba huenda ccm Ingeshasahaulika mioyoni mwa watanzania.

Bado tuna nafasi ya kuipigania katiba mpya ambayo itajibu shida hii ya ushindi wa kiudanganyifu.
 
Kila siku nasikia vilio kwamba CCM inaminya upinzani tena wengine kama akina Tundu wanasema kwamba Bungeni CCM wanatumia wingi wao kupitisha mambo, hivi kosa la CCM hapo ni lipi?
Ni kushinda uchaguzi na kuwa Wabunge wengi kuliko wa Upinzani au ni nini?

Kuna tatizo gani CCM kutumia wingi wao ambao sisi wananchi ndiyo tumewapa kwa maana ya kuwaamini kupitisha mambo wanayoona yana manufaa?

Kama chadema na Wapinzani wengine mna shida na hilo, kwa nini msishinde kwanza uchaguzi na kuwa na Wabunge wengi ili msiburuzwe kwa wingi wa CCM?
kuaminiwa na watanzania gani?
 
Back
Top Bottom