Hivi kosa la CCM ni kuaminiwa na Watanzania, au ni lipi?

Chadema ni bora mngejikita kuhoji ni kwa nini Mbowe aliuza chama chenu???

Naamini bila mbowe kuuza chama msingekengeuka kiasi hiki.

Leo mnapinga kila kitu na kujidai mnadai democrasia wakati ndani ya chadema hamna hata tone la democrasia.

Hebu jiulize wakati Mbowe anabadili gia angani alishilikisha wanachama wa ngapi??
 
l
Lowasa ni Fisadi sawa una uhakika?can you prove it?Tanzania kitu tunachoshindwa kuelewa kuna VYAMA na TAIFA.tutakapoweza kuelewa matakwa ya nchi kwanza then vyama tutafika mbali....Mimi mwana CCM kitambo,ila nchi kwangu inakuja kwanza then chama kitafuata...sio kila kitu u have to say kizuri hata kama hakipo katika level nzuri...ccm lazima wabadilike


Kwa nini hilo swali usiwaulize chadema? Tena hasa Lisu Tundu, Lema, Slaa &Co. ndiyo waliosema kwamba Lowasa ni fisadi na siyo mimi!

Kama nilivyokwishaandika kuchaguliwa kwa CCM na Watanzania ni kwa sababu hawaoni Chama mbadala wa CCM ni rahisi kihivyo tu!

Uchaguzi uliopita hata kama ungewaleta Wamarekani wako wapige kura TanZania kwa kuzingatia Historia ya wagombea wa vyama husika yaani fisadi Lowasa, Mr.Ziro vs Dr.Pombe Magufuli Wamarekani wangempa kura Dr.Pombe Magufuli tena kwa wingi sana, hivyo hiyo ndiyo sababu maadamu upinzani unaendeshwa kama mali binafsi na siyo kitaasisi hakuna jinsi unavyoweza kushindana na CCM ambayo ni taasisi huwo ndiyo ukweli na Watanzani tulio wewngi tunaliona hilo!

Hivi nina nani yuko tayari kuikabidhi nchi yetu kwa mtu kama Mbowe? Kwa maana kuichagua chadema ambayo ni mali ya Mbowe na familia yake, hakuna anayejua au mwenye uwezo leo hii wa kumfukukza au hata kumuonya tu Mbowe kwa lolote lile, hakuna kikao cha kumfukuza na wala haipo kwenye Katiba ya chadema ni jinsi gani Uenyekiti wake unakoma, sasa kwanini nimkabidhi nchi mtu kama huyo? Unaweza kuniambia?

Si ni bora CCM kwamba najua Uongozi una ukomo wake wanakuja wengine leo hii Kikwete anamalizia anaondoka na sheria na kanuni ziko wazi mwakani 2017 kuna Mkutano Mkuu, sasa wewe niambie ni lini kuna mkutano mkuu chadema na nani anaamua?
 
Back
Top Bottom