Hivi kilimo si kazi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kilimo si kazi?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Exaud J. Makyao, Feb 3, 2009.

 1. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nashangaa sioni nafasi za kazi ya kilimo zikitangazwa au kutafutwa.
  Kulikoni?
  Kwani kilimo siyo kazi?Au kuna shida gani katika kilimo?
   
 2. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Hapo sijakuelewa mkulu,kwamba unamaanisha nafasi za kazi ya wataalamu wa kilimo ama nafasi za kazi za watu wa kulima(watakaofanya kazi ya kulima)...Othewise kilimo ni kazi kama zilivyo kazi nyingine...Be blessed
   
 3. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bado kuna utata bwana Balantanda,
  Mbona kuna sikukuu ya wafanyakazi na sikukuu ya wakulima?
   
 4. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Nadhani ni mapokeo tu ambayo yalitokana na mfumo wa enzi zile za chama kimoja CCM ambapo ilikuwa inasemwa kwamba alama ya Chama cha Mapinduzi Jembe na Nyundo zilikuwa zikimwakilisha mkulima(Jembe) namfanyakazi( Nyundo) hata sijui ni kitu gani kiliwafanya watu waamini hivyo...Aidha kuna baadhi ya watu wanaamini kwamba mfanyakazi ni yule mtu anayefanya kazi ofisini tu(kazi za kuajiriwa serikaini ama katika mashirika na taasisi zisizo za kiserikali) na mkulima ni mtu ambaye anajishughulisha na shughuli nyingine(hajaaajiriwa) ndiyo maana mpaka leo kuna baadhi ya watu ambao si waajiriwa(mmoja wao) anaweza akaenda sehemu yoyote mfano hospitali akaulizwa kazi yako jibu atakalolitoa ni mkulima japo katika hali ya kawaida hajishughulishi na kazi ya kilimo(unaweza kukuta ni fundi seremala,fundi nguo,fundi bomba,mwanamichezo,mwanamuziki nk)...So kimsingi kilimo ni kazi kama zilivyo kazi nyingine tatizo ni mazoea na ugando wa fikra ambao umejengeka miongoni mwetu,elimu yahitajika katika hili...Be blessed
   
 5. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkulu Balantanda, asante kwa ufafanuzi wako. Nikweli mapokeo tuliyonayo sii mazuri sana juu ya kilimo. Mtumwingine akiulizwa unafanya kazi gani atakwambia sinakazi. Kimsingi wawezakutamtu huyu labda anajishughurisha na kilimo cha bustani mfano lakini kwake kuwa na kazi ni kufanya kazi kwenye maofisi tuliyo yazoea bilakujua kuwa hata bustani ni office pia.

  Kwa upande wa mkulu Exaud J. Makyao swali la je kilimo ni kazi au la na kwanini watu hawajishughulishi kuomba kazi za kilimo. Nadhani kwa lugha nyepesi mkuu utakuwa shahidi, shule nyingi hasa za kijijini mwanafunzi akifanya kosa basi adhabu kuu atakayopewa utakuta ni kulima, kufyeka nyasi, kupalilia mazao fulani, na shule niliyosoma mimi ilikuwa kung'oa visiki na kupasua kuni. Kaka adhabu kama hizi zinamfanya mtu aone kilimo ni adhabu na akichukie kabisaa.

  Mwenye uzoefu mwingine atuhabalishe
   
 6. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
   
Loading...