Hivi kile kitengo cha usalama kimekufa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kile kitengo cha usalama kimekufa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mabewa, Dec 3, 2011.

 1. M

  Mabewa Senior Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mara ya kwanza ktk historia ya vikao vya nec ya ccm,maoni ya EL na wote waliomfatia yalikuwa yakisikika kila kona ya nchi na dunia kwa ujumla hii ni kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano.

  Upo ushahidi usiotia shaka kwamba baadhi ya wahariri ktk vyumba vya habari walijua neno kwa neno alilolisema lowasa kuliko mwandishi aliyepo ktk jengo kunakofanyika kikao.

  Sasa nauliza haya yote wakati yanatokea usalama wa chama upo wapi? Au nao wamehongwa au kupangwa ili kumdhalilisha mwenyekiti? Ipo siku hivyo vikao vya maadili vitarushwa 1 kwa 1 tusubiri.

  Source(mayage s mayage)mwanahalisi
   
 2. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Jana Nape alilalamikia uvujaji wa taarifa na nyaraka za ccm.

  ...Pakacha bovu hudondosha kilichomo ndani, kimoja kimoja.
   
 3. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Inavyoonyesha aliyoyasema Lowasa Rais bado hayajamfkia,manake kama tafsiri ya umma kuhusu aliyoyasema Mheshimiwa huyo,ndani ya vikao vyao ambayvyo wamezoea kuviita vikao halali vya siri,siri yote ya yaliyosemwa ambayo yamekwenda nje kiasi kuwa aliyosema yametoka kama yalivyotamkwa mpaka na nukta,imekuwa sio siri tena,na yeye msemaji anaonekana kuwa anachokitamka na kuwa YEYE AJUI RICHMOND NINI HIVYO TUMUULIZE RAIS WETU.Kwa watu wenye akili zao ni kwamba kamlushia Rais mzigo wa RICHMOND.

  Ila haya yote nina sentesi moja WHAT GOES AROUND COMES AROUND [Hii kanuni piga ua iko pale pale inafanya kazi na itafanya kazi daima] kama binadamu ni swala ni moja kumtendea binadamu mwenzio yale ambayo ungelitendewa wewe ungefurahi.

  Japo aliyasema hayo akitegemea UMMA UNGEHAMAKI,lakini walio hamaki ni vyombo vya habari kwa kuwa watu makini wote ambao wangesimama na kusema hisia zao juu ya taarifa hiyo ya NEC,wanajua kilichojili kwenye mwenendo mzima wa RICHMOND ya kuwa MPENDAKUJILIMBIKIZIA ALIMWINGIZA MKENGE MTOTO WA MWENZIE [MAFIOSO STYLE] ILI NDOA IKUE NA KUTENGENEZA AINA YA BLACKMAIL AMBAYO INGEKAA KWENYE KUANGALIA MASLAHI YAO KULIKO UKWELI WA ZOEZI ZIMA KWA KUWA LENGO SI KUJENGA BALI LENGO NI KUJIJENGA.

  UBAYA KWA KUWA MLEZI NA MJENZI WA MFUMO ULIYOYATENDA HAYO,HAKUWA NA BUDI KUBEBA KIUBISHI NAMNA YA KUIONDOA AIBU HIYO KWA NJIA ZA PANYA.NA HATIMAE HISIA ZA KIMUNGU [YANI ASILIMIA 80% YA WAPIGA KURA ] ZIKACHUKIZWA NA MATENDO HAYO,KUTOKANA NA KUWA NA IMANI NAE ZAIDI NAE AKAZIDIWA NA URAFIKI ULIOMFIKISHA HAPO KWENYE DONDA AU KAA LA MOTO.

  NDIO MAANA MZIKI ULIOCHEZWA NA UNAOENDELEA KUCHEZWA DAIMA AUNOGI KWA KUWA KWENYE UMMA WA WENGI MKONO WA MUNGU USIMAMA IMARA JAPO KUNA UZEMBE WA MUHUSIKA.
   
 4. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Title yako inaongelea usalama wa Taifa, kwenye text unaongelea Usalama wa chama. Napata shida kuelewa nini hasa wataka kuelezea, so far Usalama wa Taifa hawapo kwaajil ya CCM mana ile ni Taasisi ya Umma na wanalipwa mishahara kutokana na Kodi zetu, CCM wanakitengo chao cha usalama kilichojaa wahuni, wanakiita Green Guard, labda ungeuliza wakati hayo yaliyotokea yanatokea Green Guard walikuwa wapi????
   
 5. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Du mdau vipi kidogo uwa sipendi kuchangia thread ya mtu unless ina content ila imebidi nichangie kwako kwa swala moja statement ya thread inasema hivi ''HIVI KILE KITENGO CHA USALAMA KIMEKUFA'' mwadishi hakusema ''HIVI KILE KITENGO CHA USLAMA WA TAIFA KIMEKUFA'' mbona hizi ni sentensi mbili tofauti sana P.Pole sijua level yako ya uelewa,ila kwa taarifa yako Mwandishi anazungumza katika lugha tofauti sana kwa lugha nyingine,style hii inazungumza lugha pana,wala hamaaaanishi usalama kwa maana ya ulinzi,na kulindwa watu au mbwa au chochote.


  Mwandishi anawaauliza CCM imekuwaje leo ndani ya NEC,siku za nyuma taarifa za vikao vyao zilikuwa azipenyi kuwafikia,watu wengine na umma huku nje,lakini mara ghafla,Mpenda vyombo vya habari,alipowasilisha mada yake ndani ya kikao hicho cha siri,hapo hapo Waandishi wa habri walioko ndani ya vyumba vya habari walijua kila kitu mpaka nukta ya hotuba yake hiyo ya dakika saba.Na ikashindikana vipi wahudumu na wasaidizi waliomo ndani ya jengo kunakojili kikao cha NEC wasijue Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kapewa ujumbe mkavu mkavu mpaka yale ya mwaka alobaini na saba,ambayo wakati hayo yanafanyika zanzibar nilikuwa bado niko form one,sijui kutofautisha kuwa kiongozi aweza kuwa jinamizi,niliamini viongozi wengi ni watenda mema kwa Wananchi.

  Lakin leo kupitia kikao hicho cha NEC, ambacho natafsiri kuwa kilienda LIVE kasolo PICHA ZA TELEVISION nimejua kumbe Paul Sozigwa alishamkabaga koo Rais wetu.Hivyo kuhalalisha haya yanayojili kuwa Mzee yule alikuwa sahihi.Mimi na ujana wangu wa leo watu wazima hao mmoja kumuumbua mwenzie hadharani mpaka wengine mtaani na Nchi nzima anayoingoza wakiwemo vijana wadogo tumejua siri za miaka hiyo tisini kweusi ndani ya vikao vya NEC [Zanzibar] ndio kusema mmoja kamchoka mwenzie na hivyo lilobaki ni KUALIBU.

  Hivyo P hapa hakuna swala la usalama wa Taifa,hapa ni maadili [Usalama] wa chama na viongozi.yani ile misingi ya kuwalinda wao na chama kukaa kwenye UADILIFU [Usalama].Mtu akiwa mwadilifu anakuwa salama wa aina yoyote ya migongano na jamii yake.Cha ziada yeye anakuwa ni mpiganaji wa mbele dhidi ya maadui wa umma wake.
   
 6. M

  Mabewa Senior Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umemaliza kaka kuna cha kuongeza?
   
 7. M

  Mabewa Senior Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Namaanisha kitengo cha usalama cha chama,navyofahamu ukiacha green guards kuna kitengo maalum cha usalama kinashirikiana kwa karibu na TISS so wakati ule ingekuwa wote walioshiriki mchezo ule wangekuwa wamebainika na kuchukuliwa hatua
   
 8. M

  Mabewa Senior Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana kwa kusaidia jamii yako kwa kuelimisha watu wa kurukia na kuchangia humu jf soma kwa makini elewa kilichoandikwa kisha changia,nakushukuru mkuu
   
Loading...