Hivi kama ninamchukia mtu nawajibika kumpinga hata kwenye ukweli?!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kama ninamchukia mtu nawajibika kumpinga hata kwenye ukweli?!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FDR.Jr, Jun 4, 2012.

 1. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]NIMELISOMA GAZETI LA MWANANCHI LEO NIKAINGIA MTANADAONI KUANGALIA MAONI YA WADAU LOOOOH NIMEKUTANA NA JINA LA MWANA JF AKIMSULUBU MH.KAFULILA KUPITILIZA. HOJA YANGU NDANI YA JAMVI; HIVI CHUKI KWA MWANADAMU MWENZAKO INAKUPA UHALALI WA KUPINGA KILA ANALOLISIMAMIA HATA YALE AMBAYO 100% NI UKWELI NA HAKI? SOMENI HABARI HII NA CHINI MSOMENI MWANA JF MWENZETU ALIVYOITIKIA TAARIFA HII. NADHANI TUNAPASWA KUBADILIKA KIMTIZAMO ILI TUWEZE KU SECURE BRIGHT FUTURE.


  Kukamatwa kwa mbunge kwaibua mapya
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 04 June 2012 09:11 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila

  Raymond Kaminyoge
  WAKATI Mbunge wa Bahi, Omar Badwel anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za kupokea rushwa, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ameilipua Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) kuwa imekithiri kwa rushwa.

  Kutokana na tuhuma hizo, Kafulila amemtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda kuvunja kamati hiyo, vinginevyo yeye atajiondoa.

  Pia mbunge huyo ameitaka Kamati ya Maadili kulitumia Bunge kumvua ubunge, Badwel, kutokana na tuhuma za kupokea rushwa zinazomkabili.

  Kafulila alisema hayo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari huku akisisitiza kuwa, wananchi hawatakuwa na imani tena na kamati hiyo.

  “Ikumbukwe Juni 13, 2011 nilieleza bungeni namna wabunge wa Kamati ya LAAC wanavyoomba rushwa kwa watumishi wa Serikali, huku nikimtaja kwa jina Mbunge wa Bahi, Omary Badwel kuwa ni miongoni mwao,” alisema Kafulila ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo.

  Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi ya Takukuru, Alex Mfungo alisema juzi kuwa mbunge huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

  Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema hana taarifa zozote za mbunge huyo kukamatwa.

  “ Sina taarifa za mbunge kukamatwa na Takukuru, kama ni kweli tutaletewa taarifa rasmi ndipo ninaweza kuzungumzia suala hilo,” alisema Makinda kwa simu.

  Awali, Kafulila alisema licha ya kutoa taarifa hiyo bungeni na kumwandikia Spika kuhusu vitendo vya rushwa vya baadhi ya wajumbe, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

  “ Nilijitoa mhanga kwa kutaja majina ya wabunge wanaoomba rushwa kwa watumishi wa Serikali, lakini hatua hazikuchukuliwa, sasa leo Takukuru wamemtia mbaroni mmoja wao, bado hamuamini,” alisema Kafulila.

  “ Sasa naomba niweke wazi kwamba kama Spika hataivunja kamati hii na kuunda nyingine nitajiondoa kwenye kamati kwa sababu itakuwa imepoteza imani kwa wananchi,” alisema Kafulila.

  Alisema kamati hiyo imepoteza uhalali na sifa za kuendelea kuzikagua hesabu za serikali za mitaa kwa sababu wajumbe wake wanatuhumiwa kwa rushwa.

  Kafulila alisema ni wajibu wa Spika kutafakari upya kuhusu hadhi ya kamati hii na kuipanga upya kwa kuzingatia masilahi ya umma.

  Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema, ndiyo yenye jukumu la kusimamia hesabu za serikali za mitaa.

  “Serikali legelege ni matokeo ya Bunge legelege kwa kuwa ni kazi ya Bunge kusimamia na kuidhibiti Serikali kikatiba,” alisema Kafulila.

  Mbunge huyo wa Kigoma Kusini aliitaka Bunge kuweka azimio la kumvua ubunge Badwel kwa vitendo vyake vya rushwa.

  “ Kamati ya Maadili ya Bunge ifanye hivyo ikiwa ni hatua za kinidhamu kuchukuliwa kwa mbunge huyo kwa tukio hilo la aibu,” alisema.

  Kafulila alisema hata mabunge ya Jumuiya za Madola ambalo Tanzania ni miongoni mwao, huchukua hatua za kinidhamu za kuwavua wabunge wanaotuhumiwa kwa makosa ya aibu kabla ya mahakama hazijatoa uamuzi.

  Kwa mujibu wa Kafulila, Bunge la Uingereza limeshachukua hatua za kuwavua ubunge watuhumiwa zaidi ya 59 ili kujenga imani ya wananchi kwa Bunge lao.

  “Kwa hiyo nafahamu kwa kutumia azimio, Bunge lina uwezo wa kumvua madaraka mbunge yeyote ambaye amefanya vitendo vya aibu vya kuliaibisha Bunge,” alisema.

  Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 71(1) (d) Mbunge anaweza kupoteza nafasi yake ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

  Mbunge huyo wa Bahi, Badwel, na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi wote wa CCM ni miongoni mwa wabunge waliotajwa na Kafulila (NCCR-Mageuzi) katika Bunge la bajeti mwaka jana kwamba aliwakuta wakiomba rushwa kwa viongozi wa halmashauri ambayo hakuitaja.

  Juzi saa 9.00 alasiri, Badwel alikamatwa na Takukuru akidaiwa kupokea rushwa kutoka kwa watumishi wa Serikali katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  MSOMENI HUYU NDUGU YETU HAPA JF; NAAMINI HAKUMTENDEA HAKI MH.KAFULILA HATA KIDOGO
  #5
  rutashubanyuma 2012-06-04 10:27 kafulila naye aache ubabaishi na ubaguzi. yeye alifukuzwa uanachama NCCR MAGEUZI akakimbilia mahakamani ikawa kinga yake. Sasa naye badwel bado hata hajafikishwa mahakamani unadai avuliwe ubunge na siyo kusimamishwa hadi suala lake litakapokwisha. Ikumbukwe bunge lililopita akina pesambili alikuwa na kesi ya ya jinai lakini hakuzuiwa kwendelea na ubunge sasa huyu badwel tatizo liko wapi?

  Au Pesambili alipendelewa............sahihi ni kusimamishwa ubgune lakini huwezi ukamvua ubunge kwa tuhuma tu ambazo mahakama inaweza ikamsafisha.....sasa ikimsafisha ndipo mtafidia vipi yeye na wapigakura wake..........tujifunze kuheshimu sheria hata kama kuna ushindani wa kisiasa.
  Quote
   
 2. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Kweli hakutendewa haki.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,599
  Likes Received: 3,892
  Trophy Points: 280
  sio huyo tu ndugu yangu FDR.Jr wako wengi humu!!! kuna watu wanakuwa na akili za nguo , kuna wakati wanazivua na kuna wakati wanazivaa!!
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  FDR,
  Sioni kama kuna chembe ya chuki. Anachosema mdau ni kuwa mahakama iachiwe ifanye kazi yake kwani hata David alipohisi kufukuzwa uanachama NCCR kwa kuonewa alitafuta haki mahakamani.
   
 5. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ilisemwa "Ceasar's wife should be beyond suspicion" hawa viongozi wetu wa umma ni sawa na mke wa kaisari ni lazima wawe juu ya tuhuma na maana hawapaswi kutuhumiwa ni lazima wawe as clean as possible!
   
 6. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,530
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  have you done any self assessment?
   
 7. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  nadhani mtoa maoni yuko sahihi kabisa
  mahakama ndicho chombo pekee chenye mamlaka
  ya kusema mshtakiwa ana hatia au lah na sio bunge au waziri
  katiba pia imeanisha hivo,sisi tunaweza kujua mtu ana kosa lakini
  mamlaka ya mwisho ni mahakama.Sasas Kafulila mamlaka hayo katoa wapi?
  labda spika kwa busara zake avunje kamati lakini sio kumvua ubunge hadi mahakama ithibitishe.
  tusikurupuke kuhukumu kama great thinkers tambueni uwepo wa sheria za nchi.
  Presumption of innocence imefia wapi?? what if he was planted? what if its true?
  doubt ziko nyingi hapo.
   
 8. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Nimesoma kwa makini maneno ya Ndugu Rutashunyuma.Kwa mtazamo wangu,sijaona mahali alipoonyesha chuki yoyote dhidi ya Kafulila.Kama unadhani hayo ni 'mashambulizi & chuki",basi labda maneno 'mashambulizi na chuki' yana maaana nyingin tofauti na ninayoijua mimi!
   
 9. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Ubinafsi ukizidi ni mbaya, bunge limvue ubunge wake baada ya hukumu kutolewa mahakamani
   
Loading...