Hivi Kagasheki na wenzake serikalini wanayakumbuka haya maneno ya Mwalimu?

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Leo nimefarijika sana kuisoma hotuba ya Freeman Mbowe ambayo amenukuu maneno mazito kutoka kwa baba wa Taifa. Nikakumbuka kujiuliza swali linalohusiana na hilo kwenye mawazo yangu nilipomsikia jana Waziri Kagasheki akisema ya kwamba watu wa Loliondo siyo wamiliki wa Ardhi ya Tanzania, bali ardhi yote ya Tanzania ni mali ya Rais... Nilimshangaa sana Waziri Mbunge Balozi msomi kama Kagasheki akiongea maneno kama kasuku kutetea 'status quo'. Nani anawapa jeuri kama hiyo hawa watu waliomo madarakani?

Leo kama jibu la maswali yangu na alama kuu ya mshangao iliyokuwepo juu ya kichwa changu imetoweka baada ya kusoma nukuu ya maneno ya baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere juu ya kuboresha maisha ya Watanzania kutoka kwa Mbowe:

"Tukiwasaidia watu wa Tanzania kuendelea, ndiyo tunaiendeleza Tanzania. Maana Tanzania Ni ya Watanzania Na Watanzania Ni wote, Hakuna mtu mwenye haki ya kusema "Mimi ndiyo watu". Wala hakuna Mtanzania mwenye haki ya kusema " Najua linalowafaa watanzania na wengine lazima wafuate".


Kwa nini jk na serikali yake ya ccm haitaki kuelewa hilo?
 
Hata mimi nimemshangaa sana yule mzee! Ina maana kama ardhi ni ya rais, basi anao uwezo wa kukifuta kijiji chochote na wanakijiji wake akawapotezea mbali!
 
Back
Top Bottom