TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,513
- 11,276
Hili swali limenijia ghafla wakati tunaendelea kuomboleza Kifo cha Rais Magufuli.
Kutokana na ukweli kuwa Uchaguzi uliofanyika mwaka Jana umeacha majonzi makubwa Kwa Viongozi na wafuasi Wa Vyama vya Upinzani. Pamoja na kuibuka manung'uniko miongoni mwa watanzania kuwa Vyombo vya Dola vilivyohusika kwenye Kampeni na hatimaye Uchaguzi vilipendelea Chama Tawala hata katika maeneo kilipoonekana kushindwa ama kuzidiwa na Upinzani.
Tuliona hali ya majonzi na hata manung'uniko kule Zanzibar lakini baada tu ya Rais Mwinyi kumwapisha Maalim Seif kuwa makamu Wa kwanza Wa Rais, ghafla hali ikabadilika na wananchi wengi hata wapinzani wakaonesha imani na mapenzi Kwa Serikali ya Rais Mwinyi.
Je, katika wakati huu tuliogubikwa na chuki na mpasuko Wa Kiitikadi za kisiasa, Mama Samia Suluhu anaweza kuteua Makamu wake kutoka Chama kikuu cha Upinzani nchini ili kutuliza hali?