Gojaga Nize
JF-Expert Member
- Jul 1, 2015
- 2,755
- 1,734
Leo nimekumbuka story moja ya zamani kidogo.
Nilipomaliza darasa la saba 2001 nilienda kwa ma mkubwa ambako nilikuwa nimetafutiwa shule ili nianze form one. Niliwahi mwezi kabla shule haijafunguliwa.
Nilipofika pale nilikuta kuna vijana wa kiume wawili na wa kike wawili. Wa kiume tulikuwa almost umri sawa, ila wa kike walikuwa wamepevuka kidogo tayari kwa kuolewa kijijini.
Basi usiku tulikuwa tukimaliza kula tunakaa nje kupiga story. Kuna katabia siku za mwanzo sikukashitukia kwa hawa mabinti. Yaani katika ule mda tunapiga story utawaona wanaingia ndani. Kama robo saa wanatoka then utawaona wananong'ona na mother mkubwa then wanazunguka nyuma ya nyumba halafu wanaondoka hamuwaoni tena.
Kumbe walikuwa na wachumba ndiko wanakoendaga. Siku moja tukasema ngoja tuwafatilie tujue wanaingia nyumba gani. Walivoondoka tu na sisi tukafata kwa nyuma. Duuu hadi nyumba waliyokuwa wanaingia tukaiona ni gheto kwa jamaa alikuwa mwalimu wa shule ya msingi.
Tulikula mingo kama masaa mawili hivi ndio tukaona wanatoka kurudi home. Tulishangaa sana inakuaje mama anawaruhusu watoto wa kike watoke usiku. Baadae tulikuja kudodosa wakasema yule ni mchumba wa mmoja wao. Nyumba haikuwa na baba ndio maana yawezekana walikuwa wanauhuru sana.
Sasa nimegundua kuwa nyumba nyingi zenye watoto wakike, mara nyingi utumbo wote ambao mtoto wa kike anafanya mama lazima anajua.
Kwahiyo kuharibikiwa kwa msichana yeyote kuna mchango 80% ya mama mzazi kachangia.
Mwisho wa utafiti