Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 46,322
- 114,626
Habari za wakati huu wanaMMU, natumaini usalama upo na mnaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Niende moja kwa moja kwenye mada, kuna jambo moja lilinishangaza sana redioni nadhani kwa wale waliobahatika kusikiliza XXL ya clouds fm jana watakua wamenipata vyema kabisa.
Kuna bwana mmoja wa Morogoro alipiga simu kwa sudi brown akilalamika kuhusu mke wake kutumia mda mwingi kusikiliza nyimbo za msanii wa bongo fleva Jux mpaka inapelekea kuacha kutekeleza majukumu yake kama mke na mama wa familia.
Kwa mujibu wa huyo bwana anasema ilifikia hatua mpaka wakafikishana kwa wazazi kuhusu hilo swala na bado hawakulipatia utatuzi na alikua akiyasema hayo yote mkewe akiwa nae.
Kilichofuatia waliunganishwa na Jux na kumueleza hali iliyokua ikiendelea kati yao na huyo mke wa huyo bwana akamuomba sana Jux amtembelee/waonane ndio labda tatzo litaweza kuisha.
Inashangaza sana, Hivi kweli mwanaume na akili timamu unaruhusuje ujinga kama huu kuwepo kwenye ndoa yako? Au ndio kulogwa maana hadi hali kama hii kufikishwa kwa wazazi ni aibu.
Bado najiuliza inakuwaje unampenda mtu kiasi hicho adi unakwamisha majukumu yako ya muhimu?
TOO MUCH IS HARMFUL, KILA KITU KWA KIASI.