Hivi huu ndio mwanzo wa kuachika ama...msaada tafadhari...

Hivi huu ndio mwanzo wa kuachika ama...msaada tafadhari...

Wakuu sana,

Mimi Pangu Pakavu leo nimeota ndoto. Nimeota ndoto ya kusikitisha hadi sina amani kabisa. Nikiwa kitandani na mke wangu nimeota mke wangu anafunga ndoa na mtu ingine kabisa. Hata church pastor alipomuuliza kama anakubali kuolewa akasema ndio nakubali.

Mimi eehh Pangu Pakavu nilikuwa mbele yao eti nimewashikia vitabu vya liturgia ili wasome vizuri.

Asubuhi nimeamka jicho nimelifyatua kama mwendawazimu. Nimemwamsha wife kwa fujo na nikataka maelezo kamili kwa nini anataka kuniacha/kunisaliti. Naamini kichwa yangu sababu mwaka 2011 december niliota niko angani na familia yangu. Wiki mbili baada ya xmas nilipata scholarship huko Cardiff na wife na dogo walinisindikiza kisha wao wakageuka baada ya siku 2.

Hapa wifw kanuna...mie ndo usiseme...chai hainyweki...simu zote zake ninazo...hakuna kuoga...gari funguo zote ninazo mfukoni...housegal hamna kupika...milango bado sijafungua...mpaka nijue sababu ya ndoto hii mimi Pangu Pakavu.

Nimeileta ndoto niliyoota mie ili ninyi mnisaidie mimi Pangu Pakavu.

mara nyingi unabii unatimia pale unapojidai kuukimbia au kuepusha jambo linalokuja kukutokea kusababisha litokee.
ukisoma kwenye biblia uakuta mara nyingi unabii wa hatari ulipokua unatoka mhusika anajaribu labda kumuondoa huyo atakeutekeleza au kukimbia kutoka maeneo husika kumbe huko anakokwenda ndo anaenda kutimiza huo unabii, sasa wewe endelea kushikiria sicmu na funguo za gari hapohapo utatimiza huo unabii
 
Baada ya kucheksa sana sasa ngoja nikusaidie kutafsiri ndoto yako kutokana na maelezo yako, vile umesema kwenye ndotowewe ndo uliwashikia litugia mkeo na jamaa mwingine wakiapa kiapo cha ndoa yao na mke anitika ndio nakubali basi hiyo tafsiri yake ni kuwa, umekuwa daraja au umeshiriki kumsaidia mkeo kupata mume nje. Jiulize wapi ulimpeleka mkeo na ukamuacha kwa mwanaume unayemuamini hata akalala huko au baada ya kumkwaza mkeo amekulalamiakia badala yakusolve umekuwa ukimpa mgongo na kumtuma nenda kwa wanaume wako huko sina haja tena na wewe hivyo kaenda kweli sasa huna jinsi ndo keshaolewa hivyo, badala ya kuwauwa wao na huo upanga wako utakufa wewe.

Na hapo ukijamuachia mkeo nakwambia atatoka nduki na mtoto wenu hatarudi tena maana ataenda na polisi kusema mume wangu hayuko sawa kapanda kichaa bora mtuachanishe na mie niendelee na maisha yangu na ndo utakuwa chizi zaidi ya hiyo ndoto yako inavokufanya.
Wanawake wakiwa wamenuna huwa wanawaza solution ya tatizo likiisha tuu utaona kafanya uamuzi ambao utashangaa aliupanga saa ngapi, kumbe wakati wewe unahangaika kumkaba akupe jibu yeye akipata upenyo tu hafanyi kosa lazima upigwe 3-0.
  • JF ina wataalamu kila idara. Safi sana Mkunde Original ndoto nyingine nitakuletea! Ndio namalizia kuiota. Copy Over and Out
 
Last edited by a moderator:
Daviey 69...hapa ninampango huo huo...wacha niwahi hardware kufata panga...leo hapakaliki wala hapaliki hadi aniambie tafsiri sahihi ya hii makitu...wacha niwahi panga...

ha ha ha, hata abunuasi alikuwa anaota ndoto kama hizi zako.😛op2:, btw, how old are you brother:confused2:

Mkuu get serious, wahi hosii ukachekiwe malaria, uote ndoto wewe akutafsirie mkeo!!!:doh: isije kuwa kinyume wewe ndo utafunga ndoa na mwanamke mwingine, unajua mara nyingi ndoto ni marudio ya vile vitu ambavyo tumekuwa tukiviwaza, kwanza mods Invisible, Paw hili bandiko lilipaswa kuwa kwenye jokes na gossips, kwa mfano ungeota ulikuwa ungeota kibarua kimeota nyasi au biashara mtaji umefilisika ungemshikia nani bango?

muombe radhi mkeo na hausigelo wenu kwa kuwadhalilisha, sio kila ndoto ina maana, usifikiri kilichotokea last time ndo hicho hicho, ile iltokea tuu na kwa taarifa yako sio ile ndoto ilitimia hapana maana itakuwa tayari ulishadhamiria na wazo/shauku na hamu ya kufanya hilo uliloota na likatimia. be a gentlemen vinginevyo utampa mkeo kila sababu ya kuisaliti ndoa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom