Hivi hili tangazo la ACACIA mnalielewa?

Caroline Hans

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
723
386
Kila nikifikiria ile ripoti ya Makontena ya Mchanga iliyowasilishwa juzi hata matangazo yao siyaelewi!! Hili ni moja ya tangazo linalovuma kwenye baadhi ya vyombo vya habari likieleza kwamba nchi yenye maendeleo ni ile inayotengeneza nafasi za ajira, na kwamba mgodi wa ACACIA kwa kila muajiriwa mmoja waliyenae hutengeneza nafasi 11 za ajira nchini, Je kuna ukweli wowote hapo?

IMG_4838.jpg
 
Kwani hamjui kuwa nchi hii ina watu wajinga hadi huko mgodini?

na hapo unaweza kukuta hao jamaa wa kitanzania wameitwa ofisini na HR wao na CEO na kuagizwa kuwa wajiandae watapigwa picha na hayo maneno yaandikwe ili kumpa pressure Rais.

Poor kabisa Ninyi ACACIA, nguvu mnayotumia sasa mngeitumia hiyo hiyo kutuingizia Bilioni 500 kwenye Account ya serikali pamoja na kuomba radhi kimya kimya na kukubali kurekebisha hali.
 
Hilo tangazo ni mbwembwe tu kutuzuga eti wanatusaidia katika tatizo la ajira. Lakini kiukweli wanachochuma na kutunyonya havilingani hata kidogo na hiyo ajira wanayojitapa kutoa kwa Watanzania.

Mtoa Mada lazima ujue kuwa Serikali inajitahidi kuona nayo inafaidika na rasilimali za nchi na siyo serikali ikae kimya kwa kuogopa kuhoji tena kwa ushahidi kuhusu wizi unaofanywa na ACACIA.

Kawaida ya Mwizi yoyote yule au Muuaji tena na ushahidi upo dhahiri dhidi yake kuhusu vitendo vyake ni lazima atakataa kuhusika na tukio hilo.

Tatizo la ajira ni world wide siyo kwetu tu. Na hiyo ajira wanayotoa ACACIA kwa Watanzania ukiangalia utagundua kuna GAP kubwa ya Kipato mishahara marupurupu kati ya International Staffs na Local Staff. International Staff wanavuta dola kibao ukilinganisha na Local Staffs. Hapa kuna shida.

Mi nadhani tusubiri Matokeo ya hizo Tume nyingine afu tuendelee kushauri Serikali namna ya kulimaliza hili Suala la mchanga huku tukiweka maslahi ya Taifa letu mbele badala ya kutanguliza maslahi ya Mabeberu mbele.

Kwanza hizi nchi za Ulaya zimetunyonya sanaaaaa na bado zinaendelea kutunyonya kwa kutumia Mawakala wao. Ilitakiwa hivi sasa Watulipe fidia ya miaka 400 ya Utumwa na Manyanyaso waliyowafanyia Mababu zetu.
 
Nadhani sio kuajiri bali wanalisha watu 11 maybe katika familia zao
...ila nisiwe mnafiki dah hawa jamaa ACACIA ntawamis sana zile party zao pale Hyatt Kilimanjaro zilikua zakufa mtu yani unakula mtungi tani yako, warembo classic mi ilikua ni mwendo wa Hennessey tu mezani na mishkaki ya samaki
Kwahesabu za haraka nilikula tungi kama za laki5 hiv maana nilibeba zingine.
 
Mlipokua mnaambiwa mikataba hii in tatzo na wabunge was upinzani pale bungeni mbona mlikua mnawazomea sana mliambiwa sana tunaibiwa mlikataa mliwaona wabunge was upinzani in waongo Leo JP amejiongeza eti mnamshangilia wkt tumeshabakwaa.natamani JP ahame ccm ili awanyonge wabunge wt kaka zake 3 wote uvccm wanaoshangilia kila utumbo nao wanyongwe mana
Hawa ni wala pipi wakubwa kumbe wenzao wanakula minofu.uvccm mjitathini hapo mlipo..na kuanzia Leo mm ccm basi ccm kila kitu mmetunga wenywe ufisadi wenyewe unafiki wenywe.lo ccm ni hovyo ni janga.
 
Jina lao linaishia na CIA.....huenda ni kitengo cha CIA cha kuibia nchi masikini.
 
Siwatetei Acacia, lakini nadhani wanazungumzia kitu inaitwa Trickle Down Effect. Acacis ikiajiri mfanyakazi, huyo mfanyakazi atanunua chakula kwa mama ntilie, naye mama ntilie atamuungisha mtu wa sokoni,mtu wa sokoni atanunua bidhaa kwa mkulima, mkulima atanunua mahitaji yake dukani kwa mangi, mangi atashona nguo kwa fundi juma, fundi juma atanunua kitambaa kwa Ali mpemba etc etc etc... Nadhani ndo maana ya hilo tangazo. Wanazungumzia indirect employment
 
Kila nikifikiria ile ripoti ya Makontena ya Mchanga iliyowasilishwa juzi hata matangazo yao siyaelewi!! Hili ni moja ya tangazo linalovuma kwenye baadhi ya vyombo vya habari likieleza kwamba nchi yenye maendeleo ni ile inayotengeneza nafasi za ajira, na kwamba mgodi wa ACACIA kwa kila muajiriwa mmoja waliyenae hutengeneza nafasi 11 za ajira nchini, Je kuna ukweli wowote hapo?

View attachment 514779

WEZI TU HAWA.... PERIOD.
 
Nadhani sio kuajiri bali wanalisha watu 11 maybe katika familia zao
...ila nisiwe mnafiki dah hawa jamaa ACACIA ntawamis sana zile party zao pale Hyatt Kilimanjaro zilikua zakufa mtu yani unakula mtungi tani yako, warembo classic mi ilikua ni mwendo wa Hennessey tu mezani na mishkaki ya samaki
Kwahesabu za haraka nilikula tungi kama za laki5 hiv maana nilibeba zingine.
kuna jamaa anamiliki mabus ya abiria ni mfanyakazi wa acacia katoa ajira ngapi huyu
 
Watu wa migodini bwana wanatia raha. Nakumbuka mwaka Fulani mgodi ambao uko Nzega walijisifia kuwa kwenye mrahaba wamemgharamia Katibu Mahususi (Personal Secretary) wa Mkuu wa Wilaya kwenda kusoma computer. hahahahah
 
Back
Top Bottom