Nimeshuhudia mara nyingi teuzi za watendaji wa nafasi mbali mabali za serikali na taasisi za umma kwa kuwateuwa wanataaluma waalimu wa vyuo vukuu na kuwaweka katika nafasi hizo.
Nijuavyo mimi vyuo vikuu ni vinu vya kufua watendaji wa nyanja mbalimbali. Utaratibu wa kuwapata waalimu wa vyuo huandaliwa kwa kuangalia maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi tangu anaingia chuo mapaka anahitimu. Ni waliofauru vizuri wanabakizwa chuo, wanaendelezwa kutaaluma hadi kuwa waalimu wakiwa na Masters, Phd na kuwa ma-profesa. Kazi ya kuwaandaa ni kubwa na yamuda mrefu.
Sasa hivi naona viongozi wetu wamvamia vyuo na kuchukua wanataaluma hao kuwapa kazi nje ya kusudio la vyuo, nani atafundisha wanavyuo wetu mbona mnawamaliza? Si tunasema kipaumbele ni elimu, sasa elimu bila waalimu itapatikanaje? Tutapata wataalamu wengine wenye uwezo kama mnabomoa vinu vya kufua wataalamu?
napenda pia kutoa tahadhali kuwa uwezo wa wanataaluma hauna mahusiano kabisa na utendaji kazi na ufuatiliaji wa shughuli nyingine nje ya taaluma. Mala nyingi wanataaluma hupenda kukaa kwenye kusoma vitabu, makala, tafiti, makongamano n.k, kwenda site kusimamia utendaji physically wengi hawawezi. Tunahitaji watu wafuatiliaji na hasa wanaopenda na kuweza kusimamia site nikiwa na maana maofisini, viwandani, mashambani, migodini, n.k.
Hawa tukitaka kuwatumia tuwape tu asigment wakiwa hukohuko vyuoni watuandalie drafts za sera, mikataba, mipango kazi, na kutfanyia tafiti n.k. Twaweza kuwalipa kwazi hizo tu basi lakini waendelee na shughuli za kutuandalia wataalam.
Sasa tumeisha wapoteza profesa Sarungi, Tibaijuka, Asha Rose, Shukuru Kawambwa, Mack Mwandosya, hawapendi tena kwenda kufundisha! na hakuja jipya walilolifanya katika nafasi walizotumikia, Hii ni hasara! Sasa naona Magufuli ndio kamaliza waooote kabisa. Kila nafasi - ni profesa, Dr na woote anawatoa vyuoni!
Hebu tuone mfano huu:
Linganisha Dr Asha Rose na Balozi Mahinga katika nafasi ya uwaziri wa mambo ya nje,
Profesa Tibaijuka na Lukuvi katika uwaziri wa Ardhi,
Profesa Kapuya na Hamisi Kagasheki katika uwaziri wa Mali asili
Kama mawazo yangu si sahihi nawaomba radhi, wala sina wivu na uteuzi wao maana mi najiajiri, najipangia kazi, najisimamia, najitathimini, na najitumbua jupi mwenyewe!