Hivi hii serikali ya CCM inachukuliaje swala hili la mkuu wa wilaya huko Mwanza?

SonGod emo

Member
Apr 5, 2012
17
12
Kwa watu wengine inaweza kuwa kama tuko ndotoni lakini huwezi kuamini kama nchi hii kuna watu wanaishi kama wakimbizi .Inasikitisha sana kuona kiongozi anaamuru polisi kuchomea wananchi nyumba zao kisa eti wamejenga kwenye hifadhi wakati wanajenga mlikuwa wap? Mmechoma nyumba zao isitoshe na vyakula walivyokuwa wamehifadhi kweli hii ni Tanzania au ndo tunaelekea kuwa kama Somalia au Eritrea maana na hao walianza hivi hivi kwa kweli inauma kuona mtu kwenye bchi yako unafukuzwa kama mbwa koko asiye na mwenyeji upinzani wakiliongelea eti wanavuruga Aman ya nchi sasa imefika mahali pa kusema imetosha kunyanyaswa .
 
Ukifatilia elimu za wakuu wa wilaya ni viio weng plus magumashi tu, kwahiyo wanakulupukaga na present tense tu
past na future tense hakunaga kwa hawa watu...

Nakingine utumwa kufanya hivyo sasa lazima wafate waliowaweka bila kuchanganya naza kwake ( a.k.a kama KOVA), poleni mangosha wenzangu wote mliochomewa.... vuteni subira T2015CDM inakuja kuwapa amani na maisha safi.

V
SENGEREMA
 
kha kwani kule kagera wale ng'ombe waliopigwa risasi jana,MR DHAIFU AMEANZA U DICTATOR,ANAJUA HANA JINSI LIWALO NA LIWE,ILA 2015 C MBALI,PANAPOTOKA MOSHI.......
NAMI NAENDA KUSALI NIMECHELEWA SANA LEO SABATO JUMAMOSI.
 
Huyo kada wa ccm dawa yake ni kuchoma na yeye nyumba yake halafu tuone atajisikiaje, ndipo kitakapoeleweka.
 
Kwa nini wananchi walijenga ktk hifadhi hawajui au ni viburi ili wapate kulaumu serikali. Mimi siamini kama Mwanza viwanja vimekuwa adimu kiasi hicho mpaka kujenga kwenye hifadhi. watanzania tuache tabia ya kuwa tegemezi
 
Kwa hiyo unamaanisha M4C Itaruhusu watu kujenga kwenye hifadhi/ Kama unawapenda watanzania wenzako toa elimu kuhusu umuhimu wa kutojenga kwenye hifadhi na si kuleta ushabiki humu JF
 
Kwani kama walivamia wangefanya kubomoa wasingehama? Pia serikali ilikuwa wapi mpaka wanajenga na kuishi? Tatizo ulegelege umezidi kwa serikali yetu
 
Kwa hiyo unamaanisha M4C Itaruhusu watu kujenga kwenye hifadhi/ Kama unawapenda watanzania wenzako toa elimu kuhusu umuhimu wa kutojenga kwenye hifadhi na si kuleta ushabiki humu JF

nikutoa elimu ya kutovamia hifadhi zetu na kutunza mazingira
 
Back
Top Bottom