Hivi hii ni sawa au mimi ndio nakosea

Hivi hii ni sawa au mimi ndio nakosea

Mimi nimeolewa na watoto wawili tatizo mme wangu alikua anafanya kazi kwenye kampuni fulani ila kwa bahati mbaya katika punguza punguza wafanyakazi naye akawa amepigwa chini.

Kajitaidi kuapply sehem nyingi ila hajafanikiwa kupata kazi sasa mimi kama mke nikaona miezi inakatika bado hajafanikiwa nikaona nilikua napesa kidogo kwenye akounti nikamwambia chukua walao ufanye biashara huku tukisubiri kama mambo yatakaa vizuri.

Daa nashangaa mwenzangu hataki anataka biashara kubwa kubwa na hela anategemea apewe na ndugu wa ukoo na hao ndugu wanampiga kalenda kila siku.

Hivi mimi kumshauri afanye biashara ndogondogo nimefanya kosa au yeye kubaki nyumbani kusubiri hela kubwa ya kupewa na ndugu ndio anakosea nawasilisha kwa maoni na ushauri.
Hyo kampuni itakua tbl
 
Pole sn. Kikubwa ana angalia financial status aliyo kua nayo. Umefanya jambo jema sn na ww ni wife material. Nenda nae taratibu tu maana mtegemea cha nduguye hufa maskin. Nazd kukupongeza sn tena sn.
Ubarikiwe mkuu
 
Psychologically jamaa yupo kwenye hali mbaya ni vile huwezi jua anahitaji msaada zaidi kabla ya hilo ulilo mshauri keep digging
 
Yapo mambo mengi, yamkini hana uzoefu na biashara, lakn pia ushauri wa nduguze au rafikize unaweza usiwe mzuri kwa kumzuia asitumue fedha yako. Pia ni vzr kumwona mtaalam wa saikolojia kwa ushauri zaidi.
 
Wanaume waliowengi huwa ni ngumu kukubali pesa ya mwanamke maana wanatujua tulivyo na masimango.

Yawezekana anakufahamu vizuri hivyo anaogopa masimango ya baadae.

Au anaogopa kuonekana dhaifu.

Au anaogopa kushusha heshima yake kwa kumtegemea mkewe.

Au.......
Au hapendi kuulizwaulizwa mahesabu ya jinsi alivyotumia hizo fedha alizopewa...
 
Kumsaidia mumeo katika kipindi kigumu kama hicho ni jambo jema sana. Mambo ya kuzihgatia, pamoja na michango ya maana mingine iliyotolewa, ni
1. Angalia ni kwa kiasi gani tatizo la kazi limemshitua na kumchanganya, inawezekana bado haamini kuwa kazi imeondoka
2. Msaidie aweze kufanya shughuli anayoweza kufanya na kuifurahia. Usimlazimishe kufanya shughuli fulani kwa vile wewe ni mtoa pesa
3. Mtafutie washauri wazuri katika masuala ya biashara na ujasiliamali ili asichanganye mahusiano yenu ya ndoa katika biashara
4. Endelea kumuonyesha kuwa bado unamtegemea kama baba wa familia, usimsimange kwa kutafuta kwake misaada na kushindwa kwake.
 
Mimi nimeolewa na watoto wawili tatizo mme wangu alikua anafanya kazi kwenye kampuni fulani ila kwa bahati mbaya katika punguza punguza wafanyakazi naye akawa amepigwa chini.

Kajitaidi kuapply sehem nyingi ila hajafanikiwa kupata kazi sasa mimi kama mke nikaona miezi inakatika bado hajafanikiwa nikaona nilikua napesa kidogo kwenye akounti nikamwambia chukua walao ufanye biashara huku tukisubiri kama mambo yatakaa vizuri.

Daa nashangaa mwenzangu hataki anataka biashara kubwa kubwa na hela anategemea apewe na ndugu wa ukoo na hao ndugu wanampiga kalenda kila siku.

Hivi mimi kumshauri afanye biashara ndogondogo nimefanya kosa au yeye kubaki nyumbani kusubiri hela kubwa ya kupewa na ndugu ndio anakosea nawasilisha kwa maoni na ushauri.
Saikolojia inamsumbua,kutoka kuwa na kazi nzuri anayoipenda alafu aanze na mtaji mdogo anaona rafiki jamaa n n.k watamcheka.mshauri zungumza naye kwa upole akae ktk uhalisia atakubali wazo lako,pia Nina wasiwasi w yy kuogopa masimango
 
Wanaume waliowengi huwa ni ngumu kukubali pesa ya mwanamke maana wanatujua tulivyo na masimango.

Yawezekana anakufahamu vizuri hivyo anaogopa masimango ya baadae.

Au anaogopa kuonekana dhaifu.

Au anaogopa kushusha heshima yake kwa kumtegemea mkewe.

Au.......
Sikuwahi kujua kuwa una akili kubwa hivi
 
Sipokei hela ya mtaji kwa Mwanamke wangu kamwe!

Nitaparangana hata kwa kukopa kwa washkaji.

Yakwake anunue vitenge
 
anaogopa neno hili...bila mimi usingefika hapo?......au. ....mnhu! shukuru Mimi..ungekuwa mtu wewe!!!??
 
Hata kipindi yupo kazin namzidi kipato na vitu vingi tunasaidiana na cyo ananilisha tunalishana
Kama unamzidi kipato wekeza ww uzibe pengo , anzisha biashara ya familia na sio yako , pengine ni mapito ili mjifunze kuwa na kipato mmbadala bila kutegemea kuajiriwa...hii itakusaidia endapo utajiuliza je? Na wewe ukipumzishwa kazi itakuje ...
 
Back
Top Bottom