Yaani sometimes inabidi tu tuwahurumie nahisi uelewa wao hauko sawa..kuna msichana nilimpeleka kwa mama yangu..akakaa nao karibu miaka 3 akiwa huru(jumapili the entire day anaruhusiwa kwenda kushinda kanisani-as according to yeye aliokoka) sasa nadhani sometimea uhuru unapowazia kuna tatizo..akaanza mara kununa ohvyo wakati mwingine bila sababu,tho ni mchapa kazi kwakweli..au akienda churc anazidi kuchelewa mmh...ghafla siku hiyo kaamka akamwambia mama ..kesho naomba niende..mama akamwambia ok but anipigie mimi kwanza..nikamuuliza vipi kuna tatizo akasema hapana bali tu amepata kazi kwengine-Buguruni(hope wanamlipa juu zaidi) nikamwambia fine..u may go hata leo,nikatoa baraka zote.sasa cha ajabu tangu aondoke huu ni mwezi wa pili...simu,msg kila mara..za ooh nimewamiss..sometimes najibu,zikinichosha nazichunia..jana ndo kaanza anaomba hata elfu 5..amechacha mno,maisha ni magumu..jamani sasa nimweleweje huyu?kwanini aliondoka kama hakuwa na uhakika na anakoenda?huwa kinawapata nini hawa wasichana?