Nimeleta hii mada baada ya Kushtushwa na mdogo wangu mmoja aliponiambia the way wanavyofundishwa Kingereza
Jamani watoto siku hizi wanakaririshwa hata Kingereza? Imagine Mwalimu anawapa Mbinu wanafunzi kwamba
Katika Mtihani Ukiona If basi jawabu lake ni then kama ukiona Whom basi jibu lake ni You yaani kuna formula za namna ya Kujibu maswali ya Kingereza siku hizi!
Sasa najiuliza Tatizo liko wapi?
Walimu hawaandaliwi Vizuri au hawana knoledge ya kile wanachopaswa kufundisha au Wanafunzi wanasukumwa kutoka Primary kwenda Secondary!
Ni wapi makosa yamefanyika jamani kwa maana the situation is worse than what someone can imagine