Hivi hakuna uwezekano wa kusimamisha safari za rais?

Collins

Senior Member
Jul 19, 2012
145
48
Hizi safari za rais zimezidi sana,hakuna uwezekano hizi safari zichunguzwe au kuundiwa kamati/tume ili
kujua imeleta manufaa gani kwa taifa,au hakuna mamlaka inayoweza kufanya uchunguzi wa hizi safari au hata kustopishwa kwanza.
 
Safari za Raisi kwa mawazo yangu sio tatizo la Tanzania. Ukizuia safari wakati ili kupunguza matumizi wakati pesa za matumizi zinatoka hukohuko haina msingi. Ni sawa na kusema watu wabaki vijijini wasije msini kutafuta kazi kwasababu watatumia pesa nyingi kusafiri!!. Hii hoja ni ya kutokuelewa pesa ya Tanzania inatoka wapi!!
 
Kwa Mawazo yangu safari alizofanya hapa USA ni za msingi sijui sehemu nyingine.
 
Hizi safari za rais zimezidi sana,hakuna uwezekano hizi safari zichunguzwe au kuundiwa kamati/tume ili
kujua imeleta manufaa gani kwa taifa,au hakuna mamlaka inayoweza kufanya uchunguzi wa hizi safari au hata kustopishwa kwanza.
Sasa kama hutaki asafiri nje unataka aje kukutembelea wewe kila siku?
 
Akija kwetu Katavi ni neema wazee tunajichana vyakula na mapilau kwa hiyo kwetu asiache kuja
 
Safari za Raisi kwa mawazo yangu sio tatizo la Tanzania. Ukizuia safari wakati ili kupunguza matumizi wakati pesa za matumizi zinatoka hukohuko haina msingi. Ni sawa na kusema watu wabaki vijijini wasije msini kutafuta kazi kwasababu watatumia pesa nyingi kusafiri!!. Hii hoja ni ya kutokuelewa pesa ya Tanzania inatoka wapi!!

hiyo safari angefaa afanye ndani ya nchi
 
Hizi safari za rais zimezidi sana,hakuna uwezekano hizi safari zichunguzwe au kuundiwa kamati/tume ili
kujua imeleta manufaa gani kwa taifa,au hakuna mamlaka inayoweza kufanya uchunguzi wa hizi safari au hata kustopishwa kwanza.

Ushindwe na Ulegee unataka tufe na njaa we thubutuuuuuuu
 
Hizi safari za rais zimezidi sana,hakuna uwezekano hizi safari zichunguzwe au kuundiwa kamati/tume ili
kujua imeleta manufaa gani kwa taifa,au hakuna mamlaka inayoweza kufanya uchunguzi wa hizi safari au hata kustopishwa kwanza.

Ushindwe na Ulegee unataka tufe na njaa we thubutuuuuuuu hata mi sikubali acha safari ziwe nyingi ili matumbo yetu yapate kushiba
 
WE HUJUI ANATEMBEZA BAKULI ILI WANAWE TUPATE CHAKULA NA CHAKUNYWA, INGAWA AMELETEWA HOJA YA USHOGA ILA KAIPOTEZEA BADO ANAENDA TU KUWAOMBA. Na nahisi itakuwa ile hoja ya Cameron imekubaliwa kimyakimya.
 
Zipo zenye tija kwa taifa ila zingine mhhhhhhhhh
Kuna haja ya kuprune baadhi maana too much of anything is harmfull
 
Hizi safari za rais zimezidi sana,hakuna uwezekano hizi safari zichunguzwe au kuundiwa kamati/tume ili
kujua imeleta manufaa gani kwa taifa,au hakuna mamlaka inayoweza kufanya uchunguzi wa hizi safari au hata kustopishwa kwanza.
Unaongelea impossibilities!! Fahamu kuwa hobby kubwa ya JK, ni kusafiri nje!! Na kumbuka kuwa wapambe wake kwa kuwa wanaijua hiyo hobby yake kuu, hawaishi kumfagilia, kuhusu safari zake za nje,popote penye mkusanyiko.Kwani hujamsikia Magufuli jana akimuhimiza JK, aendelee kusafiri kwenda nje, kwa kuwa anajua kuongea kiingereza mpaka anawalainisha wafadhili wetu wana tumwagia misaada, kama hao walitufadhili kwenye huo mradi wa mabasi yaendayo kasi?! Kweli ukishangaa ya Musa, utayaona ya Firauni!!
 
Back
Top Bottom