Hivi hakuna mamlaka zinazosimamia wenye nyumba?

Hassani

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
710
1,140
Imekuwa ni kawaida wenye nyumba kunyanyasa wapangaji,kama upangishaji wa nyumba ni biashara kama biashara zingine e.g guest,hotel.kwanini usiwekwe mfumo wa kuwalazimisha wenye nyumba wapate leseni na kukubaliana na vigezo vyote vitakavyowekwa na mamlaka husika kabla ya kuanza biashara hii?.Kwanini wenye nyumba wanaachiwa kufanya watakavyo,vitu kama kumzuia mpangaji wako asisikilize gospel kisa wewe muislam,kumfungia geti akichelewa kurudi wakati yeye anafanya kazi hotelini,kumpandishia kodi utakavyo,kuzuia wageni wake eti wanajaza choo,kumfukuza mpangaji kwa madai anaringa sana,kubagua wapangaji kwa kuangalia dini,jinsia,kabila.Hivi huyu Prof Anna anasimamia makazi yapi wakati huku uswazi tunataabika?
 
Mkuu umesahau; ukila vizuri bila kumpa baba mwenye nyumba inakuwa kero na unaweza kuhamishwa bila notice. Nchi yetu hii mambo yanaenda segemnege. Biashara ya kupangisha haiwezi kufanywa na kila mtu kwa kupangisha kachumba kamoja kamoja inatakiwa tuwe na real estate developers ambao watapangisha watu kwa mikataba maalumu kama ilivyo kwa NHC! Haya masuala ya kila mtu kupangisha ni kero kubwa ndio maana utakuta kila mtu anataka kujenga kakibanda kake ili kuepuka hizo kero na matokeo yao tunayaona; nyumba zinajengwa pasipojengeka.
 
Hassani,
Hiyo avatar yako ni noma, yaani glock haiishi njugu!!??
Nchi yetu kila kitu ni ukichaa tu, hakuna taratibu za kuwafanya wananchi wafurahie kuwa waTZ, hata wapangaji wa kitaa
 
Mkuu umesahau; ukila vizuri bila kumpa baba mwenye nyumba inakuwa kero na unaweza kuhamishwa bila notice. Nchi yetu hii mambo yanaenda segemnege. Biashara ya kupangisha haiwezi kufanywa na kila mtu kwa kupangisha kachumba kamoja kamoja inatakiwa tuwe na real estate developers ambao watapangisha watu kwa mikataba maalumu kama ilivyo kwa NHC! Haya masuala ya kila mtu kupangisha ni kero kubwa ndio maana utakuta kila mtu anataka kujenga kakibanda kake ili kuepuka hizo kero na matokeo yao tunayaona; nyumba zinajengwa pasipojengeka.
Unachosema ni kweli mkuu,tatizo tuna watekelezaji wa hiyo kitu?maana nyumba za NHC ,kwa wanaoafford 30 au 40 kwa mwezi hawaziwezi hata kidogo,na ndio wapangaji wengi wa nchini kwetu.
 
huku chuo cha SAUT mwanza ndo job true true mtu ana ka kibanda kadogo lkni anataka laki 8 kwa mwaka.the dead government.
 
aisee ma landl
oRd noma sana.kuna mmoja tabata kimanga usipotembea na bint yake ndani ya miezi mitatu anakupa notice.anaitwa mama joji naskia noma sana.wapangaj hawakai.inabidi govt iweke utaratibu wa kuwabana hawa makaburu weusi
 
Kwa tanzania, ninavyojua mamlaka zinazosimamia wenye nyumba na zenyewe zinamiliki nyumba!
labda itungwe sheria kwamba wajumbe wa bodi ya mamlaka ya usimamizi wa nyumba wawe wapangaji tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom