Hivi Faida ya mkonga wa Internet ni upi mbona gharama ziko juu sana na bando ni kidogo

tanzanite miner

JF-Expert Member
Feb 2, 2016
257
172
Sijui ni uelewa wangu mdogo au ni nini,nijuavyo ni kua baada ya huu mkonga kusambazwa karibu nchi nzima tuliahidiwa kua gharama zitapungua na kua bora zaidi.alakini mpaka muda huu gharama zipo juu sana.
Inakuaje hii kitu au tuhamie ttcl ndio kuna nafuu?
 
Mkuu sio uchochezi lakini nimegundua upigaji hapa tanzania unakuja kwa "watanzania watafurahia gharama ndogo baada ya kukamilika" ule ni upigaji. Mangapi tumeona
Mkongo wa taifa
Gesi mtwara
Bombadia
 
Tanzania bado tuna safari ndefu sana.
Mpaka hapo asilimia kubwa ya wananchi watakapojitambua ndio haya mambo yatakwisha.
 
Sijui ni uelewa wangu mdogo au ni nini,nijuavyo ni kua baada ya huu mkonga kusambazwa karibu nchi nzima tuliahidiwa kua gharama zitapungua na kua bora zaidi.alakini mpaka muda huu gharama zipo juu sana.

"Tukihamia kwenye mfumo wa dijitali, local channels 5 zitakuwa ni bure"
Inakuaje hii kitu au tuhamie ttcl ndio kuna nafuu?
 
Sijui ni uelewa wangu mdogo au ni nini,nijuavyo ni kua baada ya huu mkonga kusambazwa karibu nchi nzima tuliahidiwa kua gharama zitapungua na kua bora zaidi.alakini mpaka muda huu gharama zipo juu sana.
Inakuaje hii kitu au tuhamie ttcl ndio kuna nafuu?
Wakati Wa uwekezaji huwa tunaambiwa lugha nzuri sana na wanasiasa hata cement walisema baada ya kupata gesi itashuka,thubutu dangote tuu kaishusha.Umesahau Viettel Halotel eti watagawa smartphone bure??????
 
Wamepandisha kwa karibu 50%. Wanapandisha kwa jinsi wanavyojisikia. Nadhani haya makampuni huwa yanafanya makubaliani fulani kwa sababu mtandao mmoja ukipandisha bei basi wiki hiyo hiyo wengine nao wanafuata. Sasa sijui watasingizia nini kimebadilika mpaka wamepandisha bei.
 
Waziri mwenye dhamana kashindwa kazi TV za bure wamefunga,bando za mitandao zimepanda nk
 
Tanzania ndio nchi yenye gharama nafuu za internet kusini mwa jangwa la sahara kuliko nchi yeyote ile.
Unalosema ni kweli ila kwanini tusiendelee kuwa cheap kwanini wapandishe?
Kwanini na sisi tusiwe na jambo zuri ambapo wengine wakiwa wanalalamika watatutumia kama reference?
Sasa wanapandisha kila kukicha ili tufanane na zimbabwe ambapo mb 2 almost sawa na 0.99 USD
 
Back
Top Bottom