Hivi Dodoma mjini kuna mbunge?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,784
12,226
Tafadhali ndugu zangu naomba kufahamishwa mbunge wa Dodoma mjini anaitwa nani? Kama kuna mtu ana contacts zake tafadhali ziweke javini nina maswali machache nataka kumuuliza.
 
Kimsingi malole kalala. Yaani Dodoma, inatia uchungu! Barabara zinavyotengenezwa, mji unavyoendeshwa, kweli magamba nchi imewashinda. Hivi soko la miembeni barabara ilitengenezwa siku ngapi zilizopita? Tena magufuli kwa mkwara akawafukuza watu. Eti wiki iliyopita barabara imekuwa mashimo matupu. Magufuli hii ni aibu! CCM kuweni na aibu! Jamani! Kwa vile wakazi wa hapa hawawasemi ndo mmeamua kuwachinjia kwenye maji siyo? Ka, serikali hii ya ajbu sana. Hivi lami mliyoweka area c ndo ya kiwango cha lami au kiwango cha kokoto za kuchana tairi za magari? Hata hili humwoni? Ndugu kuweni binadamu basi. Kweli watu wa Dodoma wamenyamaza lakini mnavyofanya imepita mipaka. Inatia huruma. Dodoma ni kama kondoo wasiokuwa na mchungaji kabisa.
 
Asante kwa kuweka baadhi ya kero jamvini, hata hivyo haitoshi lazima nimtafute na kumpa vidonge vyake kwa maandishi!
 
Endeleeni na magamba, walijua nyie ni makondoo ndio maana wakaweka hapo kwenu makao makuu hewa. Shughuli zote dar, hapo wanawazuga tu na vikao vikao.
 
Mbunge wa Dodoma mjini anaitwa Dr. David Mchiwa Malolle. Ni mmiliki wa shule ya sekondari City iliyopo kizota.. Area A. Hana bachelor lakini anajiita Doctor. Ni mtu mwenye mcmamo acyependa kushauriwa hata kwa mambo ya mcngi.
 
Ni kwa nini Tanzania nzima ikikutwa sehemu yoyote ambayo haina maendeleo mtu wa kwanza kuuliziwa ni mbunge? Je, imesahaulika kuwa majimbo yote yapo pia chini ya halmashauri, serikali za mitaa, madiwani, n.k.?
 
umejaribu kuorodhesha watu wengi na kujifanya humjui mhusika mkuu,baba wa watoto wa division four mbona haumtaji?
 
Kimsingi malole kalala. Yaani Dodoma, inatia uchungu! Barabara zinavyotengenezwa, mji unavyoendeshwa, kweli magamba nchi imewashinda. Hivi soko la miembeni barabara ilitengenezwa siku ngapi zilizopita? Tena magufuli kwa mkwara akawafukuza watu. Eti wiki iliyopita barabara imekuwa mashimo matupu. Magufuli hii ni aibu! CCM kuweni na aibu! Jamani! Kwa vile wakazi wa hapa hawawasemi ndo mmeamua kuwachinjia kwenye maji siyo? Ka, serikali hii ya ajbu sana. Hivi lami mliyoweka area c ndo ya kiwango cha lami au kiwango cha kokoto za kuchana tairi za magari? Hata hili humwoni? Ndugu kuweni binadamu basi. Kweli watu wa Dodoma wamenyamaza lakini mnavyofanya imepita mipaka. Inatia huruma. Dodoma ni kama kondoo wasiokuwa na mchungaji kabisa.
Ndugu yangu pole hii sumu ni kama kansa maana aliiacha yule wa mwanzo Ephraim Nehemia Madeje naye alikuwa ni magamba maana amevuna weeee sasa kaamua kukaa kando anakula aliyoiba, anyway i wish binadamu tungekuwa tunafufuka tungemfufua Mwl JKN aje ajionee haya yaliyopo Tz kwa ujumla.
 
Jamani mbona ukilinganisha Dodoma na Dar es Salaam utaona Dodoma ina fadhali mara mia ya Dar. Dar ni chafu, inanuka na ina Rais, Mawaziri, wabunge wengi, Mameya wanne na Halmashauri tatu. Mji wa Dar haujapangwa hata kidogo, 75% ya Dar ni mabanda na sehemu iliyopangwa ni 25%. Dodoma sehemu iliyopangwa ni 80% na mabanda ni 20%. Kwa kupangwa kwake, Dodoma ina barabara nyingi za mitaa kuliko Jiji la Dar ambapo viongozi wote wa nchi hii wanapatikana. Aibu ya Dar ni aibu ya Taifa.

CDA wamejitahidi sana kuipima Dodoma kuliko hizo Halmshauri za Dar ambazo zinawaibia wananchi kwa kisingiazio cha kuuza form za viwanja ambavyo hata havipo. Afadhali haya huyu Malole kuliko akina Masaburi, Zungu, Azzan, Mtemvu, Mnyika, Mdee, Makongoro, nk.
 
Ni kwa nini Tanzania nzima ikikutwa sehemu yoyote ambayo haina maendeleo mtu wa kwanza kuuliziwa ni mbunge? Je, imesahaulika kuwa majimbo yote yapo pia chini ya halmashauri, serikali za mitaa, madiwani, n.k.?
Tafadhali rejea majukumu ya mbunge. Moja ya kazi zake ni kuisimamia serikali kutekeleza ahadi zake. Mbunge akilala watumishi wa serikali wanatumia mwanya huo kuhujumu na kujinufaisha lakini akiwa sambamba nao ahadi za serikali zinatekelezwa tena kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu.

Mbunge amka kumbuka kuwa Dodoma inapaswa kujengwa kama makao makuu ya Tanzania.
 
Jamani mbona ukilinganisha Dodoma na Dar es Salaam utaona Dodoma ina fadhali mara mia ya Dar. Dar ni chafu, inanuka na ina Rais, Mawaziri, wabunge wengi, Mameya wanne na Halmashauri tatu. Mji wa Dar haujapangwa hata kidogo, 75% ya Dar ni mabanda na sehemu iliyopangwa ni 25%. Dodoma sehemu iliyopangwa ni 80% na mabanda ni 20%. Kwa kupangwa kwake, Dodoma ina barabara nyingi za mitaa kuliko Jiji la Dar ambapo viongozi wote wa nchi hii wanapatikana. Aibu ya Dar ni aibu ya Taifa.

CDA wamejitahidi sana kuipima Dodoma kuliko hizo Halmshauri za Dar ambazo zinawaibia wananchi kwa kisingiazio cha kuuza form za viwanja ambavyo hata havipo. Afadhali haya huyu Malole kuliko akina Masaburi, Zungu, Azzan, Mtemvu, Mnyika, Mdee, Makongoro, nk.
Umenena vyema. Dar ni uso wa Tanzania, ni taswira ya nchi nzima. Dar kuna shida kubwa hili linajulikana. Mara nyingi huwa najiuliza je hawa viongozi wamewahi kutembelea nchi za nje? Hivi mfano pale Tokyo jinsi kulivyo na Dar unaweza kufananisha? Jamani hata Kigali tu nendeni mjionee. Lakini hawa viongozi hutembelea huko na hakuna wanachofanya hapa kwao. Hivi wakoje? Nakumbuka wakati nikiwa shule ya msingi huko kijijini baba yangu mkubwa alikuwa akija anashangaa sehemu tunayolala kwa sababu palikuwa pachafu kweli, shuka chafu, godoro chafu, chumba kichafu yaani taabu tupu. Lakini kila mara alipofika alisafisha na kutoonesha tunapaswa kuishije. Na nakumbuka siku moja alituambia kwamba tusipende kuisha kama mapanya. Hili halitanitoka na kwa kweli sasa naishi sehemu safi na hata barabara karibu na nyumbani kwangu huwa nazilima mwenyewe.
Tuje sasa kwenye mada yetu ya Dodoma, ndugu yangu umesema kwamba CDA wamejitahidi kupima viwanja. Unajua CDA iliyopangilia mji huu? Si CDA ya sasa ni ile ya miaka ya 70 iliyokuwa chini ya wataliano. Sasa hivi kuna watu wamepatikana na viwanja 160 katika manispaa ya Dodoma. Hebu fikiri mkurugenzi anapatikana na viwanja 100 na zaidi. Inaingia akilini? Njedengwa imepatikana wakati wa CDA ya sasa, Kwa Mwatano panaendelea, Mlezi karibu na Mirembea panaendelea, Swaswa ndo kabisa, Mji Mwema pameshika kasi. CDA ipo inaangalia tu. Barabara za hapa mjini ni balaa. We acha bwana nchi hii bila mabadiliko tutaendelea kuishi kama mapanya tu. Mtu unakwenda kwako utafikiri unakwenda kujisaidia kichakani.
 
Back
Top Bottom