Hivi Dar hii kuna watu bado wanatumia mkaa badala ya gesi kupikia?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
37,882
43,772
Nimeshtushwa na kushangazwa na tangazo la Mihan gas linalohimiza akina mama kutunza afya, kuokoa mazingira na kuepuka usumbufu kwa kutumia gesi ya Mihan badala ya mkaa, je, inamaana bado kuna watu wanatumia mkaa Dar hii?! Naomba taarifa zaidi.
925062018s.jpg
11137659_357069831154348_1419005774_n.jpg


==============================
UPDATE: Baada ya kuleta hoja hii ya kupinga matumizi ya mkaa, Prof.Maghembe ameamua kuniunga mkono, big up Prof.!

downloadfile.jpg
 
Gesi ninayo lkn siwezi acha kutumia mkaa au kuni,

Kwa sababu

Ukisonga ugali kutumia kuni hauwezi kufanan na ugali uliosonga kutumia mkaa au gesi,

Halikadhalika ubwabwa,

Ubwabwa wa kwenye mkaa tofauti na wa kwenye kuni na gesi, hata hivyo siwezi acha asili yangu eti kwa sababu Nina gesi,

Hata kaniki ninayo
 
Nina wazo la jinsi ya kuzuia matumizi ya mkaa kwa miji kikubwa Tanzania. Kama tunaweza kuondokana na matumizi ya mkaa Dar, Mwanza, Arusha na Mbeya Tanzania itaepuka kuwa Jangwa. Kama serikali na wafadhili mbali mbali waliweza kusambaza vyandarua milioni 20 kupita mradi wa hatia punguzo, inawezekana kabisa kuhakikisha kuwa kila kaya katika miji mikubwa ina jiko la gesi. Mpango huu utachangiwa na wananchi wenyewe, makampuni ya gesi, wafadhili wa shughuli za mazingira nakadhalika. Kama yupo mkereketwa tuwasiliane tuandae andiko. Tukishahakikisha kuwa kila kaya ina jiko la gesi, ndipo tunapoweza kuweka sheria kali za kukataza matumizi ya mkaa kwenye miji mikubwa.
 
Nimeshtushwa na kushangazwa na tangazo la Mihan gas linalohimiza akina mama kutunza afya, kuokoa mazingira na kuepuka usumbufu kwa kutumia gesi ya Mihan badala ya mkaa, je, inamaana bado kuna watu wanatumia mkaa Dar hii?! Naomba taarifa zaidi.
View attachment 491971 View attachment 491972

Mi kwangu mkaa, gesi,,jiko la mafuta vyote vinatumika,,,,,Kingine mkuu uchumi unatofautiana ,,,usidhani kila mtu anamudu kununua jiko la gesi Boss
 
Tatizo ni gharama, kipindi cha nyuma simu zilikuwa ghali, wamiliki wachache, ila angalia mazingira ya sasa bei zimeshuka kila mtu anamiliki, na gesi bei zingekuwa affordable sidhani kama soko la mkaa lingeendelea kuwa kubwa.

hata umeme ungekuwepo wa kutosha na wa gharama ya chini, watu wangetumia majiko ya umeme badala ya mikaa na kuni kwa wingi.
 
Back
Top Bottom