Wanajamvi naomba kuwasilisha yafuatayo:- Kwani nakumbuka miaka ya 1990 kurudi nyuma kulikuwa na Daftari la kudumu la Makazi kwa kila Kijiji na Mitaa kwa nchi ya Tanzania. Utaratibu huu ulisaidia sana kuwatambua wageni wote waliokua wakifika sehemu hizo kwa kujiorodhesha majina yao kwa balozi wa nyumba kumi. Hii ilisaidia kutambua kwa haraka tukio lolote liwe baya au zuri kama limetendwa na mgeni au mwenyeji. Chakushangaza utaratibu huo hata sijui uliishia wapi. Nadhani ni wakati muafaka kwa serikali kuhimiza daftari hilo lirudishwe ili kuepuka yaliyotokea kwa ndugu zetu wa Kenya na kuzuia uhamiaji haramu hivyo kudhibiti matendo ya Kigaidi, Ujambazi, Biashara ya madawa ya kulevya, Magendo n.k.
Miaka hiyo ya 1990 kurudi nyuma jukumu la Ulinzi katika eneo husika lilikua ni kwa kila Mtanzania lakini kwa sasa Jukumu hili limeachiwa kwa Idara za Ulinzi na Usalama peke yake, tukumbuke kuwa madhara yatokanayo na kutokua na Ulinzi wa kutosha yanaathiri Taifa kwa ujumla na sio kikundi cha watu fulani, nijukumu letu kwa pamoja kuhimiza Daftari hili la Makazi lirudishwe kwa kuikumbusha Serikali kupitia Wizara ya TAMISEMI.
Nawasilisha tafadhali.