Hivi Chuo Tanzania ni UDSM tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Chuo Tanzania ni UDSM tu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Peter Kilanga, Mar 10, 2008.

 1. Peter Kilanga

  Peter Kilanga New Member

  #1
  Mar 10, 2008
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani watanzania mimi ni mwanafunzi lakini naomba swali hili nisaidiwe jamani kulijibu.Ni kwa kipindi kirefu nimesikia migogoro ndani ya chuo kikuu cha Dar Es Salaam.
  Chuo kiku cha dare s salaam ni chuo maarufu sana duniani kifupi cha chuo hicho hujulikana hivi UDSM.Chuo hiki kimebujikwa na rundo la wanafunzi wapya waingiao kila mwaka na hivyo kusababisha hata kuwa na upungufu wa majengo.Hivi ni lazima kweli wanafunzi wote wamalizao kidato cha sita na kuwa na sifa za kujiunga na Vyuo kwa masomo ya elimu ya juu wajiunge UDSM?Hivi ni kitu gani kilichopo pale ambacho vyuo vingine vyenye sifa kama ya UDSM hamna?.Kwa binafsi yangu mimi naona migogoro mingi iliyowahi kwisha tokea ni kutokana na wingi wa wanafunzi hao na hivyo kupelekea uongozi wa chuo kushindwa kuwahudumia kikamilifu.Hivi kuna haja gani ya wanafunzi kurundikana pale.Mimi nawasihi wanafunzi wenzangu migogoro katika sekta ya elimu hususani ya juu hushusha kiwango cha elimu kitolewacho mahala husika nchi yetu imekuwa ikijitahidi sana katika sekta ya elimu na hivyo kuwa na vyuo mbalimbali vyenye sifa.Mimi naomba kuliko kurundikana chuo kimoja na kutopata kile tulichokusudia au kukipata katika wakati tusiokusudia ni bora kabla ya kujiunga na UDSM ni jukumu letu kutafuta vyuo vyenye sifa kama ya UDSM ili pia ikiwezekana basi twende huko kuliko kujazana sehemu moja.
  Na vile vile uongozi wa chuo hivi ni kigezo gani chatumika kuwa na idadi inayotakiwa ya wanafunzi chuoni?Kwa upande wangu nahisi ni kutokana na uwezo wa vyumba vya madarasa katika kuchukua wanachuo.Sasa kama ndivyo hivyo kama nijuavyo mimi inakuwaje wanafunzi wakawa wengi kuliko Vyumba vya madarasa?Naomba uongozi wa UDSM pamoja na SERIKALI iliangalie swala hili kwa macho yote na kwa mikono yote katika kulipatia ufumbuzi.
   
 2. a.9784

  a.9784 Senior Member

  #2
  Mar 10, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama unaishi DSM,lazima unazijua kampuni nne zinazosafirisha abiria kati ya DSM na MOROGORO.Abood na Hood bei zao ziko juu sana ukilinganisha na Islam na Sdique ambao bei zao ziko chini lakini cha ajabu ni kwamba watu wanajaa kwa Abood na Hood na kwa hali za watanzania nadhani wangejaa kwa Islam na Sadique Why suuch situation.
   
 3. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Nafikiri kuna umuhimu wa kuangalia idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa na miundombinu iliyopo kwani MADARASA,LIBRARY,HOSTEL,MAJI,VYOO na vitu vingine muhimu havitoshelezi mahitaji ya wanafunzi
   
 4. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Vyuo viko vingi, ila si unajua tena hicho ndicho chuo cha kayumba! Ila hata mzumbe pale moro hali ni hivyo. kwani si unakumbuka ile system yao ya kusepetua!!! Ni matatizo kama hayo.

  Ila nashangaa zile pesa za Bush hawakuzungumzia juu ya kulitatua tatizo hilo la elimu ya juu. Hata zitto amelisahau hilo wakati ametoka hapo hapo. Anang'ang'ania Buzwagi tu....
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kwani maji na hosteli ni jukumu la UD?

  Kwani UD wamekukataza ukae nyumbani uje asb chuo kusoma?

  Hatuko tena ktk enzi za Ujamaa!!

  Let us argue beyond the box!
   
 6. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2008
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  kah!! sasa jamani hata kama hatuko kwenye ujamaa, kwahiyo ndo mtu apate tabu!! hivi wale waliotoka mbali na dar, unataka wawe wanakuja na kuondoka kila siku!!!!! manake wale makazi ni hostel za chuo na wanahitaji huduma zote muhimu za kijamii!!wapo wanaotoka vijijini huko na wanafaulu vizuri sana na elimu ndio inawaleta jijini pale, hawana mjomba wala shangazi.ubepari haumaanishi watu wasionacho wapate tabu.we have to be considerate on this.
   
 7. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2008
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mkubwa naona wewe umeenda mbali sana. Hili tatizo la miundo mbinu nadhani ni kuanzia Chekechea. Tumeona sasa hivi shule za msingi zimefurika ile mbaya. Idadi ya wanafunzi hailingani na madarasa, walimu, vitabu vya kusoma na kufundishia, viwanja vya michezo na hata maji safi ya kunywa.


  Ukienda secondary usiseme hasa baada ya ujenzi wa shule nyingi za kata. Kuna shule ina walimu wawili, kuna shule haina hata madawati, kuna shule zanyasi kwa hiyo hili ni tatizo kubwa.

  Ukienda high school ndio usisema kabisa maana wanafunzi wanaoma maliza O level na kufaulu ni wengi sana lakini hatuna shule za kuwapeleka wote. Ingekuwa ni uwezo wangu ningesema shule ni compalsory hadi High school kwa kila mtanzania. Walimu hatunao hata wa kupeleka huko masekondary nakumbuka kuna askari polisi walijitolea kufundisha.

  Vyuo vikuu tunavyo vingi vya serikali na vya binafsi. Chuo kikuu cha DSM kina wanafunzi wengi na kimekuwa hivyo miundo mbinu haitoshelezi japo baadhi ya miundo mbinu inaongezwa lakini kasi ya kuongezwa haiendani na kasi ya kuongezeka kwa wanafunzi. Mfano sisi tukisoma hapo kulikuwa hamna Mabibo hostel wala lecture rooms mpya. Kule Yombo cafteria nasikia siku hizi ni lecture rooms.

  Kumbuka tatizo sio miundo mbinu tuu bali hata maprofessor ni issue. Serikali imeongeza chuo Dodoma nasikia ni chuo kikubwa pia lakini hata tukijenda vyuo vingine vitano bado vitakuwa na wanafunzi wengi maana Serikali ilianza na MEM kwa shule za msingi ikaja na MEMKWA kwa shule za sekondari nadhani kuna haja ya kuja na MME........ nyingine kwa elimu ya Juu, ufundi na VETA.

  Kwa mantic hiyo basi Chuo kikuu cha Dsm bado kitaendelea kuwa na wanafunzi wengi na kila mmoja anataka aende pale kwani wengi bado wanamentality kuwa kama hujapita pale hujaenda chuo. Na mtuu akisema anasoma chuo kikuu anamaanisha anasoma UDSM. :)
   
Loading...