Nimeambiwa pale hakuna wa kuongoza CHADEMA kama mwenyekiti zaidi ya Mbowe! Huenda ndio maana walimkopa Lowassa toka CCM awe mgombea wao wa urais.
Najaribu kuwaza kama CHADEMA hawana tu mtu wa kuwa mwenyekiti wa chama chao,
Je, ile 2015 wangeshinda urais wangetoa wapi watu wa kuwa mawaziri na mabalozi?
Juzi nilimsikia Seif akisema yeye ndio alieilea CUF na siyo CUF kumlea Seif.
Kumbe wakati CCM mtu anaegemea kwa chama wao wapinzani chama ndio kinaegemea kwa Mtu.
Nikapata jibu kwamba, hivi vyama vya upinzani kumbe havipo kama taasisi bali ni tu vikundi vya watu flani chini ya watu flani na hao watu flani wakiondoka na hivyo vikundi ndio kwa heri.
"Jf tudumishe uhuru wa maoni ili tuwe mfano. Na kwa sababu hiyo huu uzi usiunganishwe wala kufutwa"
Umesema katika angle moja nami wacha nitupie hili, nje ya ccm kuwa madarakani, Hakuna chama kingine chenye manpower ya kujaza nafasi zote serikalini wateuliwa wa Rais kikatiba, vuta picha tu, baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, DAS, RAS, Wakurugenzi wa halmashauri, jiji, majiji, nk.
Wakati huo huo kwakua chama kimeshika hatam lazima kada zake zote ziwe zimekamilika kwa kuwa na watu wenye weledi sio hawa waganga njaa waliopo.
Najikuta nawaza kwa sauti Ni aidha CHADEMA MSETO, CUF, TLP, TADEA, NCCR - MAGEUZI, CHA ZITTO MAGEUZI NK mbaya zaidi mseto utahitajika toka hawa hawa CCM ambao wananchi wamewakataa na kuwapa walioshinda.
HOJA YA KWAMBA SIO CCM WOTE WABIVU AU WANAUNGA MKONO YALIYIKUA YAKIENDELEA! ITAKUA DHAIFU MNO.
KWANINI?
Rais Dr. Magufuli anapambana na wanaccm wenzie ambao walikua wezi, waliolewa madaraka nk. Kama hivyo ndivyo! ipo haja gani ya kuiondoa CCM ambayo inajisafisha yenyewe ili tupate MSETO wa CHADEMA, CHA ZITTO, CUF mseto na hawa CCM tena?