Hivi CCM wanatuona Wanachi hatuna akili nzuri

Hivi CCM wanatuona Wanachi hatuna akili nzuri

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
123,248
Reaction score
98,242
Akiwa mkoani Iringa katibu mkuu wa ccm ametoa kali ya kumalzia mwezi wa tano.

Bwana mkubwa huyo nadhani amekosa cha kuongea mara baaa ya kutoa katazo kwa wana Iringa wasitumie fursa walizo nazo kujipatia ajira.

Amesema kuanzia sasa hakuna mwana Iringa kumruhusu mtoto wake ambaye anasifa za kuwa mfanyakazi wa ndani kwenda kufanya kazi hizo.

Wazazi hawana uwezo wa kuwasomesha watoto wao kutokana na gharama za elimu kuwa juu na mwisho wake wanaishia darasa la 7.

Ajira kwa darasa la 7 mara nyingi ni kazi za ndani,leo hii wewe unawaambia wasiwaruhsu watoto wao waliokosa elimu kwenda kufanya kazi za ndani.

Unataka wakae kwa wazazi wao ili iweje kwa mfano?
Wewe watoto wako wanafanya kazi gani? Je wapo nyumbani wako wanasubiri msimu wa mvua waadae mashamba?

Jamani ccm wacheni maneno ya kutukatisha tamaa maana hata kazi za nyumbani ni ajira pia.
Screenshot_20230530-182804_Instagram.jpg
 
Pia hakuna ruhusa Watanzania kufanya kazi Mashairiki ya kati, hakuna kupata passport bila kupata kazi nje ilihali huwezi pata kazi bila passport
Unaambiwa kalime huku Bashe kachukua chini ya vijana ( probably wahuni wahuni wa uvccm)elfu kati ya mamilioni kufundishwa kulima.
Huyu Bashite aliwahi kumuambia hadharani "shut up".
 
Wanatufanya kama wakimbizi ndani ya nchi yetu
 
Elimu ni bure bwashee, hizo gharama unamaanisha nini?
 
Hakuna urafiki kati ya tajiri na masikini tutafute pesa watoto waishi maisha bora
Kila mtu anatafuta pesa kwa kadri anavyoweza lakini wapo wanaofanikiwa kupata zaidi na wengine wanaishia kupata mlo wa siku tu !! Hata ulaya na marekani wapo mpaka Homeless lakini Serikali zao zinafanya kila linalowezekana kuwafanya wapate mahitaji muhimu !! Angalau waweze kuishi !!
 
Nauunga mkono comment yako hapa kwetu mananchi masikini anaonekana kuwana thamani kipindi cha uchaguzi tu
 
Back
Top Bottom