Wazee wangu nimewasikia,
Ninaomba tukubaliane kuwa kama mnayosema ni ya kweli basi tatizo ni lile lile la viongozi wabovu na utekelezaji,
yes kisheria, Wanachi wanatakiwa kutangaziwa kwanza, baadaye kufanyika kikao cha public na serikali, ambapo wananchi wanatoa maoni yao na serikali inatoa yake, baadaye kamati independent ambayo inayafuatilia kwa makini malumbano ya serikali na wananchi wa eneo hilo, inakaa chini na kutoa ripoti yao ambayo ndiyo inakuwa the final, na ikibidi kunafanyika kikao kingine cha dharura tena baina ya wananchi na serikali,
sasa kama haya hayakufanywa, then kweli kuna tatizo lakini sio la CCM nzima, hapana ni viongozi wanaohusika tu,
Halafu ngoja niongeze, ninasema kwamba JK, anaweza kuwa na matatizo fulani kiuongozi sawa na yeye ni binadamu kama sisi wengine na mapungufu yetu, lakini ninataka ndugu zangu niwaambie kitu kimoja, kuhusu nidhamu kwa viongozi siadhani kama ana mchezo nalo, nimemuona kwa macho yangu akimuwashia Mzee Nchimbi na Masha, wakati alipowaita mtandao mmoja baada ya mwingine kwa wakati mbali mbali, nimemsikia akimuambia Nchimbi kuwa "......Wewe nasikia unalalamika huko mitaani kuwa sikukupa uwaziri, ukifanya mchezo nitakutoa hata huo unaibu, nataka kazi..........", sasa hamuwezi kuniambia kuwa huyu rais anataka mchezo,
leo mawaziri wote wamenywea kama wamelowa mvua, kwa hiyo ndio bado CCM tuna matatizo ya uongozi, lakini so is upinzani!