Chifu Ihunyo
Member
- Jul 3, 2006
- 63
- 10
Jangwani nayo imebinafsishwa
Mikwara yote ya kusafisha eneo la Jangwani kuwaokoa walio mabondeni na mafuriko ya mara kwa mara kumbe ni danganya toto.
Eneo hilo linadaiwa kuwa tayari lina magabacholi wanne waliolinasa tangu mwaka 2004 tangu enzi za Mzee wa Jiji Yusufu Makamba.
Serikali ya Mkuu mpya wa Dar, Abbas Kandoro baada ya kumalizana na hali ya uwanja wa fisi kwa kuwatimua wenye gesti, na vichagudoa vidogo (kiumri), ilihamia bonde la Jangwani na kubomoa nyumba kibao za wakazi wa mitaa hiyo.
Sasa imeibuka kuwa serikali imeshasukuma viwanja hivyo kwa
wafanyabiashara wenye nazo tangu mwaka 2004 na imekuwa ikitafuta kisingizio cha mafuriko kama chanzo cha kuwatimua waliojenga maeneo hayo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Jangwani Mohamed Bendera amekiri kuwepo kwa kimbembe hicho pamoja na kulalamika kuwa kesi yao ya kupinga kutimuliwa eneo hilo bado iko Mahakama Kuu na haijamalizika.
Baadhi ya wanaodaiwa kuhusishwa na sakata la uuzaji wa eneo hilo ni pamoja na Katibu wa sasa wa CCM, Yusufu Makamba na Spika wa Bunge Samuel Sitta akiwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji.
Hadi sasa nyumba 70 zimeshapigwa tindo huku wakazi wa eneo hilo wakilalamikia uonevu huo wakidai kuwa walipatiwa eneo hilo na aliyekuwa Rais wa kwanza J. K Nyerere mwaka 1974 na kuwapatia huduma safi ya visima vya maji.wengine.