katib mkoa
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 1,574
- 2,163
nadhan waliobak ni wanacham jez tu saab ata uyo makomeo anawakubali ukaw kinomanoma
Wasalaam wanajamvi.
Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa wananchama wanaojitoa kwenye chama chetu kikongwe cha CCM kwa siku za karibuni na kuona nililete hili hapa jamvini ili mwenye data atusaidie.
Naangalia picha kila siku wanachama wakirudisha kadi na hata zingine wakizichama na kuzichoma moto. Kwa idadi niliyoshuhudia mwenyewe ni wanachama wengi na bado wanaendelea kutokihama chama.
Swali langu ni juu ya tulivyoaminishwa kuwa CCm ina wananchama 6,000,000 (milioni sita), kwa mwendo huu watakuwa wamebakia wanachama wangapi!?
Mwenye taarifa na data za karibuni anisaidie.
Nawasilisha.
Siasa hizi sie tunazipigia debe mjini tu.
Na Mikoa yenye mihemko ya kisiasa Arusha,na Dar kwa wavivu wengi.
Ila huko Vijijini watu bado wana misimamo yao na wanaendelea na maisha yao.
Na ukichunguza UKAWA wengi ni vijana waliokata tamaa ya maisha wao wenyewe kwa uvivu wao.Na hii mbinu waliitumia saana CUF huku Zanzibar kuhamasisha wananchi juu ya Maisha bora mbadala wakichukua Dola.Sasa waulize leo hii hali ipoje na wamo ndani ya Baraza la maamuzi.Hahaha utacheka mpaka basi,sasa hivi ADC Hamad Rashid ndio anakuja kupiga msumari ule ule wa ahadi za CUF kuhusu vijana.
Siasa ni kama ugonjwa ambao watu tunaambukizana,yaani ukikaa na mtu fulani basi ukikutana na mwenzio basi maelezo yao yanafanana ila kwenye kuchambua hoja ndio shida sasa.Mtu anakuambia tu mie UKAWA au CCM.Ukimuuliza anakuambia maisha haya yameishanitosha,ukienda kwa undani anakula na kulala kwao na shule alikimbia.
Au mwingine anakila kitu ila mvivu kama yeye hakuna,anatamani kesho yaje mameli ya Kigiriki awe baharia.Political Science ni zaidi ya tunavyoijua kwa wana Siasa wa Tanzania.Na wanaisasa wana Target sana waliojikatia tamaa wao wenyewe.
Sasa watu mkiona pale watu wamejazana kwenye mikutano basi mnaona ndio idadi ya wanachama wenye nguvu,bila kujua upana na uimara wa chama chenyewe.
Mimi sifanyi kazi ya kuhesabu na ndio maana nikauliza. Nimeona juzi kadi ambazo zingine ni za miaka ya sitini zikirejeshwa, na haikuwa mjini bali huko huko vijijini.Mimi nimejiunga na CCM, siku waliomkata Lowassa.
Nihesabu ndio utajua tuko wangapi?
Ukawa mtashangaa, hizi elfu thelathini anazo mwaga Lowasa tutazila, kutubeba kwenye mabasi tutapanda ili tutalii, NA KURA HATUMPI
Wasalaam wanajamvi.
Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa wananchama wanaojitoa kwenye chama chetu kikongwe cha CCM kwa siku za karibuni na kuona nililete hili hapa jamvini ili mwenye data atusaidie.
Naangalia picha kila siku wanachama wakirudisha kadi na hata zingine wakizichama na kuzichoma moto. Kwa idadi niliyoshuhudia mwenyewe ni wanachama wengi na bado wanaendelea kutokihama chama.
Swali langu ni juu ya tulivyoaminishwa kuwa CCm ina wananchama 6,000,000 (milioni sita), kwa mwendo huu watakuwa wamebakia wanachama wangapi!?
Mwenye taarifa na data za karibuni anisaidie.
Nawasilisha.
Kuchoka umechoka peke yako, na uende kwenye maadamano ya pokea Lowassa na under 20s wenzio
Sie chama chetu kina songa mbele.