Hivi Bongo tunasoma ili iweje?

Naafiki baadhi ya mambo ila sio yote
Kwa mfano mdogo tu kuna kijana sio msomi ila amebadili mfumo wa Bajaj kutoka kwenye mafuta na kuwa mfumo wa solar
Ila serikali haina Habari nae kabisa
Sasa kama vijana wakipelekwa nje kama Enzi za mwalimu kule Havana kufundishwa udaltari nk
Huwezi kuleta wachina wafundishe namna ya kutengeneza simu wakati huna hata vyombo na vifaa
Ndio maana nasema bora wakajifunze nje

Imagine engineers wakapelekwa Germany au Holland kujifunza zaidi kwenye viwanda vyao na kupata ujuzi hata kama ni wajenzi

Tatizo letu ni nidhamu ya kujituma hatuna ila unapopeleka vijana kwenda kuona na kujifunza kwa wenzetu wanakuwa na maadili zaidi na kuona wenzetu walivyo

Kikwete alisema natuma vijana Kenya wakajifunze namna ya kupakia vyakula na matunda kwenye maboksi REALLY yaani hata packaging hatuwezi wenyewe hebu lione hilo
 
Me naona bhas tumeumbwa wazembe wachache wetu wana uwezo na uwajibikaji wao mkubwa ila ndo unamezwa na wazembe na wajinga wengi tulio nao, pengine tunatakiwa kupelekwa msobe msobe mwendo wa jeshini mpaka tubadilike. Maana kuna vitu ni vidogo ety yani ata kubadlisha jembe la mkono kwenda kwenye kifaa kidogo cha umeme cha kumsaidia mkulima mdogo kulima haraka eneo lake kuokoa muda na kuongeza ufanisi shambani kifaa kiwe cha gharama ya chini au kati ila watu wamudu kukipata kwa bei nafuu maana matrecta kukodi gharama kwa wakulima wa nchi hii. Hii nayo twende china?
 
😆 😂 Naona umeongea kwa uchungu sana
Kama India bado wana machine za kutengeneza nguo walizoachiwa na mkoloni mpaka leo miaka 150 bado zinafanya kazi tena ni za familia najua kuna mama mmoja baba yake alifariki akaendeleza mpaka leo ni kiwanda kikubwa sana kinazalisha
Sisi ni wazembe sana na waizi sana
Kila wanachoona ni dili hata madaraja wangekuwa na uwezo wa kuyaiba wangeyaiba tu

Kuhusu majembe inatakiwa vijana wetu so called wasomi wa vyuo ndio waje na ubunifu halafu wengine wanawekeza kwa kununua vifaa au machine za kutengenezea
Najua ni ngumu sana maana tumezoea kutumia vya watu ila sisi ni wazembe wa akili
 
Ubunifu gani watu vyuoni wanapata marks kwa kutoa chini, unaweza kuwa na wazo mwalimu asione impact yake akakukatisha tamaa, amaa mahabara isijitosheleze wewe kufanya unachotaka plus una njaa boom ujapata utaanzia wapi
 
Ubunifu gani watu vyuoni wanapata marks kwa kutoa chini, unaweza kuwa na wazo mwalimu asione impact yake akakukatisha tamaa, amaa mahabara isijitosheleze wewe kufanya unachotaka plus una njaa boom ujapata utaanzia wapi
Ni shida kila sehemu ndio maana vijana wanaishia kuwa Boda
Hapo tegemea kila awamu itakuwa ya kuomba omba tu na misaada inapigwa na wanasiasa
 
Haujamuelewa mtoa mada laiti ungemuelewa ungejubu vzr,yeye ameingeka kwa mapana yake kwa lengo la elimu ni kuweza watu kujikwamua na changamoto zinazowazunguka sasa vipi sisi mbona elimu tunayo lkn still changamoto hata ndogondogo tunashindwa kuzitatua?
 
Na kwanini tuwaze kutafuta watu wa nje kutupa ujuzi huo?sisi wenyewe tumeshindwa kabisa kuja na ujuzi ambao utatuletea tija?yani ukifikiria hii elimu yetu unabaki kukuona huruma elimu Haina msaada wowote kwenye ivyo vyuo sasa ni mambo ya hovyo tu yanafanyika ivi sisi nani katuroga sisi ni WA kupewa misaada kwenye kila sekta? Kilimo misaada,afya misaada,umeme,barabara kila eneo misaada ivi kweli hatuoni haibu?
 
Watu wa ndani wameshindwa kusimamia mawazo yenye tija kwa jamii, labda sasa tuajiri wenye uwezo wa kusimamia wawasaidie watanzania wenye mawazo pengine matokeo yataonekna, baada ya muda waliosimamiwa na wakafanikiwa watakuwa na uwezo wa kusimamia watanzania wenzao wafanakiwe kama wao, nani aone aibu? Wakati mtu akila vizuri na familia yake anaona kamaliza aoni hata haya kutokea kwenye jamii ya kimaskini, wanaenda kwenye mikutano na watu wenye uchungu na mataifa yao wanaoboresha mazingira ya wananchi wao kila leo na wanakaa kwa amani ata haya awapati
 
Nashindwa kuelewa

Yeye ana hoja kwamba elimu zinazotelewa na shule expensive the private zenye mitaala ya Western countries kama US na UK ni duni,eti ya kutoka shule za serikali ambazo hazina hata dawati la kusomea ni bora?

Ndio tulikua tuna debunk hiyo nonsense kwamba this dude is dellusional,si kweli ana anadanganya umma which is so insensitive of him to do this!
 
Wewe mtu,sasa hapo utakuwa unalaumu (1)Nyerere aliyenmarehemu?(2)Jina lake?(3)Kuzaliwa kwake?(4)Makosa yake?Au unalaumu tu ili uwe umelaumu?
Unamlaumu mtu ambaye hayupo?Akujibu nani hapo?Na wewe umefanya kitu gani ili kufuta makosa yale?
Mimi nimelaumu wapi ?

Kwa nini wewe hutaki watu wamlaumu Nyerere ?
 
Bado hujajibu swali, kwa nini hautaki Nyerere alumiwe ?

Wewe unaingilia uhuru watu wa maoni na kuwaoangia nani wa kumlaumu na kuto kumlaumu.

Swali la nyongeza Nyerere akilaumiwa wewe unaumia ?
 
Mawazo yako ni sehemu ya madhara ya kua na elimu duni, mtu wa kulaumu katika nchi hi ni mwl Nyerere, hakutaka kuelimisha wa Tanzania zaidi ya kuwapa basics za elimu tu.
Huna akil nyerere alikua wakwanza kugundua adui mkuu wawatanzania ni elimu... Kwanza kujenga vyuo vingi sio kutatua ujinga wawatz saiv mavyuo kibao ila ujinga ndo umejaaa.... Seleman mkubwa wew
 
Huna akil nyerere alikua wakwanza kugundua adui mkuu wawatanzania ni elimu... Kwanza kujenga vyuo vingi sio kutatua ujinga wawatz saiv mavyuo kibao ila ujinga ndo umejaaa.... Seleman mkubwa wew
Nyerere ndo chanzo cha ujinga na elimu duni, isipo kua alikua anayaongea ongea nyerere alikua kiongozi mnafiki sanaa alipotezea baba zetu mda na ujinga wake wa ujaama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…