Hivi bado tunawahitaji wawakilishi hawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi bado tunawahitaji wawakilishi hawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Matteo, Apr 23, 2011.

 1. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mbunge ni mwakilishi wa wananchi wake katika Bunge, yaani baada ya kuona kuwa watu wote nchi nzima hatuwezi kwenda Dodoma kujadili mambo yanayohusu maslai ya Taifa letu, tukaamua kuwatuma wawakilishi wachache kwenda kujadili kisha kutuletea majibu ya kile walicho kubaliana. Mbali na hapo vilvile Wabunge na Bunge wapo pale kuhakikisha Serikali inatekeleza kile inachostahili kukitekeleza. Tukiacha tafasiri finyu za kifisadi, Serikali inatakiwa kuweka mbele maslai ya Taifa zaida ya mtu mmoja, mmoja. Yaani kupitia maslai ya Taifa ndio mtu mmoja mmoja anapoweza kufaidika. Mathlani kabla Serikali haijafikiria kumnunulia waziri gari lenye thamani inayozidi milioni miambili ni lazima ihakikishe wananchi wake wanapata hudumu zote muhimu kwanza. Ila kama hizo huduma muhimu hazijawafikia raia wote, then serikali inaweza ikapunguza matumizi ya sio ya lazima ili iweze kumjali Raia wake. Ila kwa Tanzania hilo jambo ni Kinyume. Mawaziri, wabunge, na maofisa wakuu Serikalini wanajinufaisha alafu wakisha saza ndio sisi wananchi wengine tunatupiwa makombo.

  Mijadali mingi ambayo inaendelea katika Bunge letu, inaweza ikatuacha na maswali kama, ni kweli tuna wahitaji wabunge wa style ile??? Wabunge walioathiriwa na siasa za upepo, wabunge wasiofuatilia na kusoma kwa umakini miswaada mbalimbali inayojadiliwa Bungeni, wabunge wakuitwa kwa kengele kuja kupitisha mswaada then wanarudi nje. Report ya LHC kuhusu bunge lilopita linaonyesha ni vipi wabunge wengi hasa wa CCM walivyo lewa madaraka na wasivyo tujali wananchi tulio wapeleka Dodoma.

  Mimi Rai yangu kwa wabunge ni kuwa ninaomba wasituharibie nchi, ninajua wengi wao mambo yakienda ndivyo sivyo wataikimbia nchi hii wao na familia yao, na kutuachia dhahama sisi, naomba wasitufikishe hapo wanapo taka kutupeleka. Wakiwa Bungeni waache tofauti zao na wawe kitu kimoja kama kuna la msingi lililotolewa na wapinzania kwa nia ya kujenga nchi inabidi waliunge mkono ili tuweze kujenga taifa zuri na kama kuna la kuangamizi litakalo tolewa na Mbunge hata wakwao (CCM) inabidi wote walikemee na waachane nalo, Kwa sababu iko wazi kuwa binadamu wote hatulingani in term of thinking capacity. Mbunge wa CCM anaweza akapotoka inabidi wabunge wote wa mkanye, na si kumshangilia kwa nia ya kuwazodoa wapinzani. Bungeni siyo klabuni, na muda mnaopoteza kwa kuongea upuuzi na majibishano yasiokuwa na tija, mngeutumia kwa maswala ya Msingi.

  kuna hili swala la Tindu Lissu kama nililo andikwa na mwanajamii mmoja kwenye thread yake Mbunge wa singida mashariki (chadema)Tundu lissu,wakati akijadili kipengele cha wajumbe wa kamati za maadili na nidhamu za mahakama.Lissu ambaye pia ni mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni alipendekeza wakuu wa wilaya na mikoa wasiwe wajumbe wa kamati za maadili na nidhamu za mahakama kwani kwa kufanya hivyo ni kupeleka watawala kwenye vyombo vya kutoa haki na hivyo kuingilia mgawanyo wa madaraka baina ya dola na mahakama.Kadhalika wakuu wa mikoa na wakuu wa wilya kimsingi ni makada wa ccm na hivyo unapowaweka kwenye vyombo hivyo vya kutoa haki ni kuingilia uhuru wa mahakama kwa kupeleka itikadi za chama chao,jambo lisilo kubalika na kwamba mambo ya kimahakama yanatakiwa kuendeshwa na wanasheria wenyewe bila kuingiliwa.

  Hilo swala la Lissu lilikua halihitaji Ushabiki wa Kisiasa kwa sababu lilikua jambo la msingi na la wazi kabisa, kama waziri Mkuu alivyo liunga mkono na wabunge wengine wa CCM walipaswa nao waliunge mkono ili liweze kupita. Ila kwa sababu ya wabunge wengi wa CCm kutokujua hasa ni nini kilicho wapeleka Bungeni na kuathiriwa na siasa za upepo wakaligomea na kwa sababu ya wingi wao Bungeni likashindwa kupita.

  Ifike wakati sasa na sisi wananchi tusema tosha kwa wabunge wasiowajibika, tuwaambie wazi bila ya kuficho kuwa tunahitaji Utaifa kwanza then CCM baadae. Na kwa kuwakumbusha tu, wewe Mbunge unavyojitenga na wananchi wako kwa sababu ya hao mafisadi wachache na uzandiki unao utetea, siku ukitoka kwenye system, hawatakujua (waliobaki kwenye system) na hata simu yako wataifuta, na utabaki unaadhirika huku wananchi wakisema "yako wapi". Naomba usifike kuzomewa na kuzodolewa na wapiga kura wako. Vilevile ninajua wengi wenu mnadhani wananchi hawana sehemu kubwa kwa kua ulienda kwa mganga (wazee wa Tunguri) na akakuhakikishia ushindi na ukashinda, si kweli kwa sababu mlienda wengi na ukashinda wewe ni wananchi ndio waliamua na sio kibabu chako. Badilikeni wabunge wa CCM la sivyo 2015 Bunge zima litapambwa na vyama vingine na ninyi mkiwa nje mnazomewa na Raia mliokuwa mnawaona hawafai.
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwenye aerial font, kuna ukweli kwa kiasi kikubwa, kwamba wakuu wa wilaya/mikoa wasiwepo. Lakini hayo yote yatapatiwa ufumbuzi kwa katiba mpya ijayo. Lissu kuna mambo mengi ya muhimu anayoongoza japokuwa pia mara nyingi huchemka. kitu pekee ambacho angefanya nidigest in detail kila kitu anachokipeleka pale bungeni ili kulinda credibility yake.
  ila cha kuchekesha ni KUHUSU MHAMASISHAJI A.K.A FREEMAN, SIMSIKII KABISA BUNGENI. HUYU JAMAA ANAVYOONEKAKA NI KAMA YUPO EMPTY KICHWANI, NITOFAUTI KABISA NA AKINA ZITTO, LISU RASHID NA SLAA KWA AWAMU ILIYOPITA. YEYE KAMA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI TUNATARAJIA ALEAD MOVE NYINGI BUT IT IS OTHERWAY ROUND. AU ANATUPROVIA KUWA YEYE NI MHAMASISHAJI TU?
   
 3. U

  Uswe JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mbunge tusiyemuhitaji kabisa ni AMINA AMOUR yule alopendekeza eti serikali iongeze ushuru wa magari ili kupunguza foleni dar es salaam
   
Loading...