Hivi aliyeruhusu wanafunzi wa sekondari kuvaa hijabu alijua madhara yake?

Status
Not open for further replies.
Suala la hijabu kuvaliwa shuleni sisi wanaoona mbali tulishajua litaleta matatizo,

Hasa kwa wanafunzi wanaokua tena ni wakike, madhara yake wameshaanza kuzificha mimba, Nywele chafu, na wengine wamesuka, inaondoa Uniformity of students,
Alafu pia nasikia maeneo mengine hata wakatoliki wameanza kudai nao kuvaa baadhi ya ishara za kikatolik shuleni, vipi kila dini hata hasiyekuwa na dini akisema aende na Tunguli zake?

Tutafakari upya juu ya hijabu kuvaliwa shuleni kwa shule za serikali,

Britanicca
Suala la uchafu wa nywele na mengineyo ni tabia ya mtu.
Ulilogusa lingine ni madhehebu mengine kuruhusiwa na umetaja wakatoliki.Masister wa kikatoliki wanavaa magauni marefu na pia hawatembei vichwa wazi,unaonaje tukiwahimiza ma binti wa kikatoliki kuanza hivi.
Brittanica ni mzoefu hapa, na kwa tamaa ya kuingiza/kupata wapiga kura tunajenga mambo mengine pia ambayo si mazuri.Nakupa assignment kasikilize salaam wakati wa kufungua mikutano,je zinajenga utaifa au zinabomoa?
 
Tuendeleze kamjadala kidogo hapa ili nipate elimu nawe upate, karne hii ya 21 na ongezeko hili la joto tunalolishuhudia je ni sahihi kwa mwanamke na binti wa kiislamu kujitanda manguo hivyo? Nna ushuhuda wa kutembea na mabinti kaza wa namna hiyo hawavai kabisa nguo za ndani (simaanishi chupi) yani anavaa lile juba tu na wanakuwa na rangi mbili (Sio wote)

Na kuhusu msichana kuvunja ungo anaweza kuolewa kwa sheria za kiislamu kwa karne hii watoto wanavunja ungo wakiwa na miaka 12 je ni kweli dini ya kiislamu ni ya haki na inazingatia utu wa mwanamke? (Achilia mbali aliyoyafanya Muhammad ya kuowa mabinti wadogo nyakati hizo tuzungumzie wakati uliopo)
Uislamu ni haki na unazingatia utu wa mwanamke, masuala ya kutovaa nguo za ndani ni utashi wa mtu maana wapo tu wanaovaa vimini hawavai. Kuhusu joto hilo ni sehemu ya sababu hasa kwa wasiyovaa hilo vazi, ili ionekane wengine wanaonewa.

Mwanamke ni ana thamani kubwa mno, na maungo yake nayo ni sehemu ya thamani yake, yapaswa kuwekwa wazi na kuonekana kwa wanaostahiki na si kila mtu njiani aone. Ndiyo maana Uislamu ukahimiza wavae hijabu,.

Kuruhusiwa kuolewa akishavunja ungo si kwamba inatakiwa akivunja ungo tu aozwe, bali kama akitaka kwa hiyari yake bila shinikizo la mtu yeyote ndiyo aolewe.

Kwani umri huo kuna vishawishi vingi mno, ambapo Uislamu unazungumzia njia nzuri ya kuepuka kufanya machafu kwenye umri huo ni kuoa au kufunga. Kumbuka mtu huwezi kufunga kila mara pia.

Usichana wa mwanamke wapaswa utolewe na mwanaume mwenye heshima ya kumuweka ndani, hapo ndiyo itahesabika ya kuwa ni miongoni mwa wanawake wenye heshima. Kuupoteza kwenye mahusiano yasiyo rasmi, itaonekana hana heshima. Hivyo ili kutimiza hilo ndipo uislamu ukatilia mkazo, kwa anayetaka kuolewa ili asivunje heshima yake kama hatoweza kuhimili vikwazo na vishawishi, ruksa kuolewa.

Hivyo uislamu bado unazingatia utu wa mwanamke, kwa kumfanya alinde heshima yake. Kuchagua wa kuolewa naye, kuchagua mahari yake, kuficha viungo vya thamani yake.

Utu wa mwanamke si kumwacha akaonesha maungo wazi atamaniwe, asumbuliwe, hata iwe rahisi kwake kuangukia kwenye machafu. Stara itamwepusha na mengi
 
Suala la hijabu kuvaliwa shuleni sisi wanaoona mbali tulishajua litaleta matatizo,

Hasa kwa wanafunzi wanaokua tena ni wakike, madhara yake wameshaanza kuzificha mimba, Nywele chafu, na wengine wamesuka, inaondoa Uniformity of students,
Alafu pia nasikia maeneo mengine hata wakatoliki wameanza kudai nao kuvaa baadhi ya ishara za kikatolik shuleni, vipi kila dini hata hasiyekuwa na dini akisema aende na Tunguli zake?

Tutafakari upya juu ya hijabu kuvaliwa shuleni kwa shule za serikali,

Britanicca
Hautaweza kuona mbali wakati una upofu. Ungekuwa na uoni ungekuja na mpango mkakati wa kudhibiti hao wanaokwenda kinyume na vazi la hijabu. Sasa unataka akili yako ndogo iwaponze wote,mpaka wale wanaovaa kama ilivyotakiwa wavae?

Sijaona chochote kwako wewe na alieunganisha uzi huu isipokuwa chuki tu, BAAAASI.
 
Suala la hijabu kuvaliwa shuleni sisi wanaoona mbali tulishajua litaleta matatizo,

Hasa kwa wanafunzi wanaokua tena ni wakike, madhara yake wameshaanza kuzificha mimba, Nywele chafu, na wengine wamesuka, inaondoa Uniformity of students,
Alafu pia nasikia maeneo mengine hata wakatoliki wameanza kudai nao kuvaa baadhi ya ishara za kikatolik shuleni, vipi kila dini hata hasiyekuwa na dini akisema aende na Tunguli zake?

Tutafakari upya juu ya hijabu kuvaliwa shuleni kwa shule za serikali,

Britanicca
Zama zilibadilika saana toka walipoingiza udini ili hijabu ziruhusuwe.
Wengine wakaingiza 50/50 ya kuvaa masuruali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha wavae kwani wakificha mimba unapoteza nini? Wakificha uchafu na minywere ikisukwa wewe unapungukiwa nini na watoto wako? Vitu vingine sio vya kudiscuss.
Acha wafu wazike wafu wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ilisababishwa na kikwete sasa nasikia wana hata mahakama ya qadhi singida , na.magufuli naye ka mute
Hapa Kikwete anaonewa; hili lilianza Enzi za Mkapa miaka ya mwishoni mwa 90. Halafu kitu ambacho hua sikielewi kwa hawa wavaa HIJABU (sio lazima wawe waislam, siku hizi hata wake za watu nao wakitaka kwenda kugawa PAPUCHI huvaa hivyo hivyo) baada ya mambo hayo ya public kwa maana ya shule na kazini, wana vaa kawaida tu
 
Uislamu ni haki na unazingatia utu wa mwanamke, masuala ya kutovaa nguo za ndani ni utashi wa mtu maana wapo tu wanaovaa vimini hawavai. Kuhusu joto hilo ni sehemu ya sababu hasa kwa wasiyovaa hilo vazi, ili ionekane wengine wanaonewa.

Mwanamke ni ana thamani kubwa mno, na maungo yake nayo ni sehemu ya thamani yake, yapaswa kuwekwa wazi na kuonekana kwa wanaostahiki na si kila mtu njiani aone. Ndiyo maana Uislamu ukahimiza wavae hijabu,.

Kuruhusiwa kuolewa akishavunja ungo si kwamba inatakiwa akivunja ungo tu aozwe, bali kama akitaka kwa hiyari yake bila shinikizo la mtu yeyote ndiyo aolewe.

Kwani umri huo kuna vishawishi vingi mno, ambapo Uislamu unazungumzia njia nzuri ya kuepuka kufanya machafu kwenye umri huo ni kuoa au kufunga. Kumbuka mtu huwezi kufunga kila mara pia.

Usichana wa mwanamke wapaswa utolewe na mwanaume mwenye heshima ya kumuweka ndani, hapo ndiyo itahesabika ya kuwa ni miongoni mwa wanawake wenye heshima. Kuupoteza kwenye mahusiano yasiyo rasmi, itaonekana hana heshima. Hivyo ili kutimiza hilo ndipo uislamu ukatilia mkazo, kwa anayetaka kuolewa ili asivunje heshima yake kama hatoweza kuhimili vikwazo na vishawishi, ruksa kuolewa.

Hivyo uislamu bado unazingatia utu wa mwanamke, kwa kumfanya alinde heshima yake. Kuchagua wa kuolewa naye, kuchagua mahari yake, kuficha viungo vya thamani yake.

Utu wa mwanamke si kumwacha akaonesha maungo wazi atamaniwe, asumbuliwe, hata iwe rahisi kwake kuangukia kwenye machafu. Stara itamwepusha na mengi
Hongera kwa utashi wa kufikiri kuna jamaa mmoja humu anaharibu sana taswira ya dini yenu
 
Mimi naona japo hili linaonekana jambo dogo lakini lina athari fulani, tena ambayo sio ndogo. Kuvaa hijabu kunamtambulisha binti kwamba ni Mwislamu. Baadhi ya wanafunzi wenzake ambao sio Waislamu wanaweza kujihisi 'kubaguliwa' Hata huu uzi umeletwa kwa sababu mtu aliyeuleta amefikiri kuvaa vazi ambalo linaonyesha wazi kwamba huyu ni mtu wa dini fulani ni aina ya ubaguzi wa kidini.

Nadhani ili kila binti asitirike kimavazi na lisiwepo lolote la kuashiria ubaguzi wa mavazi ya kidini, basi kila binti atakiwe kuvaa nguo ndefu. Nguo ndefu zilizoshonwa kwa namna fulani ziwe ndio sare. Zikiwa nyeupe ndio itakuwa hata vizuri zaidi maana itawafundisha watoto wa kike kuwa wasafi zaidi kwa sababu uchafu kwenye nguo nyeupe unaonekana haraka zaidi. Tena kwenye hiyo sare, binti akichagua kufunika nywele ni sawa tu. Naomba tubadilike kimawazo jamani !

Kwa wale Wakristo wenzangu ambao hawajui kwamba Biblia inaagiza wanawake wajisitiri kwa mavazi ya heshima, someni mstari huu kwenye Biblia:-

Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri...., (1 Timotheo 2:9)
 
Kwani wewe nani hadi uwaamini?uwaamini usiwaamini wao wanasonga mbele mbaki mnaumia na vijiba vyenu vya roho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, relax! Nikueleze tu, dini ni ugonjwa mbaya sana wa akili.

Kwa mfano, mimi ni Roman Catholic, nimekulia mazingira ya dini, tena seminarini. Lakini tangu nilipogundua kuwa dini ni upumbavu mtupu, nikakaa kando, nikaacha kabisa kuwa mfia dini.

Ndio maana huwa nacheka sana pale ninapoona wakatoliki wenzangu wanapopambana kuwatetea mapadri wanaolawiti watoto. Nacheka kwa dharauu.

Sisumbuki kabisa. Huwa napenda tu kuwatoa mapovu wafia dini wote, wawe wakristo ama waislamu. Kwahiyo kuwa mpole tu, chukua glass ya maji shushia kidogo upooze koo.

Kama utapenda kujiunga na mimi kwenye chama cha wasio na dini nakukaribisha sana. Huku hakuna stress, ni raha tu hasa pale unapotizima wafia dini wanakatana mapanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa utashi wa kufikiri kuna jamaa mmoja humu anaharibu sana taswira ya dini yenu
Si kila mmoja anaijua dini ya Uislamu, ukitaka kufahamu mengi kuhusu uislamu tuulize ambao tuliisoma kama somo tutakueleza.

Wapo wengi wanachojua wao ni Quran kuisoma na hadithi tu, ila hawavijui maana yake kiupana zaidi ya kukariri. Elimu ya dini inasomewa kabisa, si mzahamzaha
 
"Inaondoa uniformity of student" mana lake nini????? kwamba wakivaa hijabu ndio hiyo uniformity inaondoka?? Hijabu ni vazi la stara. Basi wasivae nguo kabisa ili uniformity ipatikane vizur!!!!!!!!!!

Huyu atakuwa hana madada, au ameridhika uvaaji wao kama ni vimini au suruali za kubana atajua yeye. Mtu mwenye busara hawezi muona dada yake kichwa wazi, mapaja wazi,kifua matiti yote yanaonekana, na ndio chanzo cha matamanio yanaanzia hapo. Lakini akivaa hijab/baibui hutomtamani. Hawa viumbe wanasikitisha sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom