Hitilafu kituo cha Ubungo yawakosesha umeme wateja

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,297
tanesco+pic.jpg

TANESCO imesema hitilafu imetokea katika mashine namba tatu ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia kituo cha Ubungo II.

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa kwa wateja katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuwa baadhi ya maeneo hayana umeme kutokana na hitilafu iliyojitokeza.

Taarifa ya TANESCO imesema baadhi ya maeneo ya mikoa hiyo hayana umeme kuanzia saa 3:20 asubuhi ya leo Jumatano Novemba 29,2017 kutokana na mashine namba tatu ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia kituo cha Ubungo II kupata hitilafu.

“Mafundi wa shirika wanaendelea na jitihada za kutatua hitilafu hiyo kwa haraka ili kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida,” imesema taarifa ya TANESCO.

Shirika hilo limesema litaendelea kutoa taarifa za maendeleo ya kazi hiyo.

Pia, TANESCO imetoa tahadhari kwa wananchi kutosogelea, kushika wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Uongozi wa shirika hilo umewaomba radhi wateja kwa usumbufu uliojitokeza.

Mwananchi
 
View attachment 640454

Haya ndiyo madhara ya kuendesha nchi kwa kutumia akili za kiCCM.
 
Back
Top Bottom