Historia ya Wasubi na Wilaya ya Biharamulo

Hao wote ni jamii ya Interlacustrine na ukiacha Wazinza, Wakerewe na Wakara wana mchanganyiko na jamii za watu kutoka Ethiopia -Wagalla ambao ni hamites. Vilevile, jamii hizi zinaishi ziwani na samaki ni kitoweo chai cha asili. Aidha, Hali ya hewa ya jamii hizo hasa Wakerewe na Wakara ili kuwa nzuri almost kama Bukoba huku wakizalisha na migomba.
Sababu nyingine kuu ni kuwa Ukerewe na Ukara (ukiacha Uzinza) hakukuwepo sana magonjwa hatari ya asili hasa trypanosomiasis na yellow fever (licha ya uwepo pia wa malaria). Mwisho maeneo ya Ukerewe na Ukanda yana rutuba kulinganisha na Biharamulo. Kipimo cha ubora wa eneo lolote la vijijini, angalia msongamano wa watu.
Hivyo vitu nilivyovitaja ni muhimu sana kwa kujenga akili za jamii zilizoishi eneo husika.
It seems upo vizuri sana kwenye historia mkuu, je kuna relation yoyote kati ya wasubi, wahaya na wanyambo?

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
 
It seems upo vizuri sana kwenye historia mkuu, je kuna relation yoyote kati ya wasubi wahaya na wanyambo?

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
Yes kuna mahusiano makubwa kati ya Wasubi na Wahaya na Wanyambo kutokana na jamii hizo zote kuweka katika kundi moja la lugha zinazoshabihiana kwa asilimia kubwa ambalo kwa wataalamu wa lugha za kibantu linaitwa Group J linalochukua makabila yote ya Mkoa wa Kagera, Waha na Wavinza wa Kigoma, Wakerewe na Wazinza wa Mwanza, makabila yote ya Nchi za Burundi na Rwanda (ukitoa Watwa) na makabila ya Kusini mwa Uganda, pamoja na Mashariki ya DRC (Interlacustrine ethnic groups).
Hata hivyo, Wasubi wanafanana zaidi kilugha (lexical) na Makabila ya Wahangaza (asilimia 85%), Warundi (77%), Waha (pia ni 77%), Wanyarwanda (71%) kuliko Kabila la Wahaya (na Wanyambo).
Ndio maana licha ya kuwa mbali na Wanyarwanda, kuna uhusiano mkubwa kilugha tofauti na majirani zenu Wasumbwa wenye uhusiano na lugha ya Kinyamwezi-Sukuma huku lugha zenu zikiingiliana kwa asilimia 49% pekee.
 
Duh, muingiliano wa lugha unanikumbusha Waluguru na ndugu zao Wakwere na Wazaramo wanasikilizana kwa 95%
 
Yes kuna mahusiano makubwa kati ya Wahaya na Wanyambo kutokana na jamii hizo zote kuweka katika kundi moja la lugha zinazoshabihiana kwa asilimia kubwa ambalo kwa wataalamu wa lugha za kibantu linaitwa Group J linalochukua makabila yote ya Mkoa wa Kagera, Waha na Wavinza wa Kigoma, Wakerewe na Wazinza wa Mwanza, makabila yote ya Nchi za Burundi na Rwanda (ukitoa Watwa) na makabila ya Kusini mwa Uganda, pamoja na Mashariki ya DRC (Interlacustrine ethnic groups).
Hata hivyo, Wasubi wanafanana zaidi kilugha (lexical) na Makabila ya Wahangaza (asilimia 85%), Warundi (77%), Waha (pia ni 77%), Wanyarwanda (71%) kuliko Kabila la Wahaya (na Wanyambo).
Ndio maana licha ya kuwa mbali na Wanyarwanda, kuna uhusiano mkubwa kilugha tofauti na majirani zenu Wasumbwa wenye uhusiano na lugha ya Kinyamwezi-Sukuma huku lugha zenu zikiingiliana kwa asilimia 49% pekee.
Asante sana....

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
 
Habari za wakati Great Thinkers wa JF...

Mheshimiwa Maxence Melo,

Waheshimiwa Moderators wote, JF Senior members, JF Expert members, Members kama mimi, Wataalamu woooote wa masuala ya historia,,, Itifaki imezingatiwa...

Mimi nimezaliwa katika Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera lakini sijakulia huko hivyo sikubahatika kujua asili yangu hadi nilipokua na kuanza research mbalimbali zisizo rasmi na kupata machache sana kupitia wahenga na mitandao ya kijamii hususani JF.

Lakini maelezo ambayo nimekuwa nikiyapata yanatofautiana kiasi kwamba sielewi niamini lipi niache lipi. Baadhi husema sisi ni jamii ndogo ya wahaya, wengine husema sivyo.

Ni kabila linaloonekana kuwa dhaifu sana ukilinganisha na jamii nyingine za mkoa wa Kagera. Tupo chini kielimu, kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa, hata "kupenda misifa" ambayo ni asili ya Kagera tupo chini. Sijui hata tujivunie nini kwenye ka-wilaya ketu ambako hata serikali ilishakatenga kwenye maendeleo (japo mkoa mzima wa Kagera umetengwa).

Kwa yeyote mwenye kuelewa historia ya kabila la wasubi, wilaya ya biharamulo pamoja watu maarufu wa kabila hili anaowafahamu atoe mchango wake hapa.

"Jasiri haachi asili"
Sote ni watanzania lakini kuijua asili si dhambi.

Karibuni...

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app

Mna sifa kadhaa nzuri na asili yenu, uwindaji na uchawi, kwa mkoa wa Kagera mnashindana na wanyambo kwa uchawi.
 
Duuuh mbna ndgu yenu anawakana anajiita ngosha wakati tunajua yeye ni msubi mix na muhaya,ukiona mtu anakana kabila lake jua kichwani mwake iko shida kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tusipende kuwasemea watu, alijiita lini? Au kwakuwa huongea hiyo lugha? Maana watu ndio husema yeye ngosha sababu huongea sana hiyo lugha. Mi mwenyewe kutokana na sababu fulani huwa naongea vizuri sana lugha fulani kuliko ya asili ya kabila langu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pale B'mulo alikuwepo chifu wa kabila la kisubi kwa jina la Kasusula na pia aliwahi kuwa mbunge katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania miaka ya nyuma sana, kabla ya Mheshimiwa kabuye, hivyo ukitaka history anzia na ukoo huo wa kichigu maana wao watakuwa wanajua zaidi.
Niliwahi kukaa huko nikiwa mdogo sana sana na niliona wakimsalimu huyo chifu(mbunge Kasusura) kwa kupiga magoti na kusema "kasinge rugaba kadinge chombeka" sijui maana ya hayo maneno ila niliona kwa macho yangu na siyo mara moja. Pia alikuwa na mtoto wake maarufu hapo akiitwa Max sijui kama yupo au la, ni hayo niliyonayo.

Asante mkuu. Na Anatory Choya je unampata?

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
 
Wasubi ni watu wenye wivu na chuki +wachawi yani ukienda Runazi, Bh na pengine ukianza fanikiwa wanakuletea zengwe.
Hawapendi mafanikio majamaa wale

Hilo lina ukweli japo unaweza onekana mchochezi mkuu, usiombe ukafika huko Kabindi ukirudi wewe uliaga vizuri.
 
Hilo lina ukweli japo unaweza onekana mchochezi mkuu, usiombe ukafika huko Kabindi ukirudi wewe uliaga vizuri.
Duh! Hizi stori naziona hapa tu, mbona nikienda kule huwa sioni hata dalili ya hizo mambo!?

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom