Historia ya Wanyakyusa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,627
154,986
HISTORIA YA WANYAKYUSA Historia inasema kwamba asili ya Wanyakyusa ni mkoani Morogoro. Kabila hilo likitokana na kabila la Waluguru. Hili hasa ndilo chimbuko la Wanyakyusa. Inasemekana kwamba mwindaji mmoja wa Kiluguru alitembea peke yake porini bila ya kuongozana na mtu mwingine. Alitembea hadi akafika maeneo ya Kabale huko Suma, Tukuyu wilayani Rungwe. Akiwa huko, akaendelea na kazi yake ya uwindaji. Baadaye akatokea Mzulu mmoja kutoka Afrika Kusini aliyekuwa na binti yake. Akafika maeneo alikokuwa akiishi yule mwindaji Mluguru, naye akapiga kambi hapo Kabale, wakaungana katika maisha ya uwindaji.


Ikawa kila yule Mluguru akitoka asubuhi kwenda kuwinda, alikuwa akifanikiwa kurejea nyumbani na wanyama wakati rafiki yake wa Kizulu alikuwa akirudi mikono mitupu. Kutokana na hali hiyo, Mluguru akageuka kuwa mfadhili wa Mzulu, kwa kutoa misaada mara kwa mara, na kwa kulipa fadhila hizo, akamwoza bintiye kwa Mluguru. Akamwoa na maisha yakaendelea huku nyumbani kwa mwindaji wa Kiluguru na mkewe binti wa Kizulu, kukiwa hakukosekani nyama kama kitoweo. Kwa sababu ili kuihifadhi nyama ilibidi kwanza ibanikwe, basi kitendo hicho kilisababisha harufu nzuri ya kitoweo kile kusambaa eneo kubwa na kufika hadi ukweni kwake nyumbani kwa Mzulu.


Moja ya nyumba za asili za wanyakyusa Ndipo Mzulu yule akawa anasema mara kwa mara: “Pale panatoa kyusi kila siku” akimaanisha moshi kwa lafudhi ya lugha ya kwao. Mazoea ya kutamka ‘kyusi’ kila siku, yakaligeuza neno ‘kyusi’ na sasa likawa linatamkwa ‘kyusa’, baadaye ‘kyusa’ ilipozidi kutamkwa kwa mara nyingi, nayo pia ikabadilika bila kukusudia ndipo watu walipokuwa wakimwita Mluguru ‘Mnyakyusa’, kwa kuwa moshi ukiambatana na harufu ulikuwa ukitokea ndani ya nyumba yake na kusambaa. Kwa hiyo, tangu hapo na kutokana na jina hilo alilopewa kwa ajili ya mazoea ya kukosea kutamka kitu, hata watoto wake pia waliozaliwa na Mluguru na mkewe Mzulu, wakawa wakiitwa ‘Wanyakyusa’.


Hiyo ndiyo asili na chimbuko la kabila la Wanyakyusa, na kwa kuwa Mnyakyusa alikuwa tayari ana asili ya pande mbili - wakati baba akiwa na asili ya Kiluguru na mama Mzulu wa ‘kwa Madiba’. Na hata uchifu ukaanzia mahali pale palipokuwa panaitwa Kabale, na yule Mluguru aliupata uchifu kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mwanzilishi na mkazi wa kwanza wa eneo lile na ndiye aliyekuwa anafahamika zaidi. Mavazi yao Kwa upande wa mavazi, Wanyakyusa walikuwa wakivaa mavazi yaliyokuwa yakijulikana kama ‘Lyabi’, Ni mavazi ya kwanza kwa kabila yakivaliwa enzi za utumwa. Mavazi haya ni yale yanayofunika maeneo ya siri pekee, na kwa wale ‘waheshimiwa’, kidogo basi wao walivaa vazi lililokuwa likiitwa ‘kikwembe’ au ‘kilundo’.


Mavazi haya yaliyovaliwa kwa mtindo kama lubega, ndiyo yaliyomtambulisha na kumtofautisha mhusika mbele ya jamii. Ngoma yao Ngoma iliyokuwa ikichezwa na Wanyakyusa enzi hizo, ilikuwa ni ya kuchezea mikuki na mara nyingi ngoma hiyo ilikuwa ikichezwa wakati wa msiba. Lakini ngoma za kawaida zilizokuwa zikichezwa pasipo kutumia mikuki na wakati wa sherehe na shughuli nyingine, ni ‘Ipenenga’. Hii mara nyingi ilikuwa ikichezwa na watu ‘wastahiki’ tena kwa madaha na maringo ya hali ya juu. Hata machifu walikuwa wakiicheza sana ngoma hii. Chakula chao Chakula chao kikuu na ambacho Mnyakyusa angeonekana kuwa amemkarimu mgeni, si kingine bali ni dizi zinazomenywa na kupikwa maarufu kama ‘mbalaga’.


Mnyakyusa halisi kama atakula chakula lakini akakosa ‘mbalaga’ hujiona kama bado hajakamilisha mlo, ingawaje siku hizi kuna mabadiliko fulani ambayo wengi hupendelea ugali na wali; lakini bado asili ya chakula chao hawawezi kuibadilisha kamwe. Na ni lazima chakula kama ‘kande’ kipikwe kwenye tukio la msiba uwao wote, kama shughuli za msiba zitakwisha pasipo kupikwa chakula hicho chenye mchanganyiko wa mahindi na maharage; msiba huwa haujakamilika hata kama wafiwa ni watu wenye kujiweza kifedha zaidi lakini ni lazima kande zitapikwa japo kiasi. Utamaduni wao Kwa kawaida Wanyakyusa hawana mambo ya unyago kama ilivyo kwa baadhi ya makabila hapa nchini.


Wao hawapendelei kabisa mila na desturi za kuwaweka mabinti ndani au kuwafanyia mambo yoyote ya tohara. Hii ni pamoja na upande wa vijana wa kiume ambao nao hawafanyiwi ya tohara kama makabila mengine isipokuwa tu kwa upande wa vijana wa kiume mara tu wanapotimiza umri wa miaka 13 na kuendelea.
 
Wasokile ni kina nani?

Kama kwa mruguru na mzulu kuklikuwa kunanukia nyama kila siku, hadi pakawa panaitwa chusi, alilyekuwa anapaita Kyusi ni nani, kama kulikuwa na fmilia moja ya mzulu na watoto wake yaani mrugulu na binti Mazulu?

Bujibuji rafiki yangu, na wewe haya mambo ya sanaa umeanza lini? Nauliza tu lakini!.
 
Acha uongo mimi ni mnyakyusa na hatuna uhusiano na walugulu bali tuna uhusiano na wapogoro na wanyakyusa walitokea huko mahenge morogoro.nenda kajipange tena ndio uje hapa sio unakulupuka
 
Wanyakyusa ni neno la kikisi lenye maana ya wakuja. wakisi ni wenyeni wa Kyela. Wanyakyusa tabia zao copyright na wahaya.
 
Aiseee...kumbe..! Ila nijuavyo mimi ni kwamba, waluguru wana uhusiano wa moja kwa moja na wazaramo, wakutu na pia wakwere. Kwa sababu wote ni watu wenye asili moja. Kuhusu wanyakyusa...sidhani, ila labda ngoja tuifuatilie hii habari
 
Kuhusu wapogoro yaweza kuwa kweli...hata mimi nilipokuwa mahenge niliwahi sikia habari za undugu wa wanyakyusa na wapogoro. Pia wapogoro hufanana pia na wangoni, na wangoni hufanana kiasi fulani na wanyakyusa. Hvyo yaweza kuwa haya makabila ya wangoni, wapogoro na wanyakyusa yana uhusiano wa damu
 
Aiseee...kumbe..! Ila nijuavyo mimi ni kwamba, waluguru wana uhusiano wa moja kwa moja na wazaramo, wakutu na pia pwakwere. Kwa sababu wote ni watu wenye asili moja. Kuhusu wanyakyusa...sidhani, ila labda ngoja tuifuatilie hii habari

Kwa makabila hayo uliyoyataja ni wazi mnyakyusa hana uhusiano nao.
 
wikipedia husema wanyaki walitokana na malikia wa kinubi aliyeitwa nyanseba. huyu alitekwa na walinzi wwake na kwenda kumzalisha. kutokana na hadhi ya huyo mama nahisi ndiyo sababu wanyaki hupenda kupanda waume zao vichwani.
 
Red giant...kajaribu kidogo, ukweli bado haujajulikana but kama walivyo wabantu wengine inasadikika walitokea niger delta as branch ya wahausa lakin sources zingine zinasema from nubian queen ndio maana wanyakyusa majina hutoka kwa mama...mf. Kilasa akizaa mtoto wa kiume ataitwa mwakilasa,kyusa-mwakyusa etc.
 
Kuhusu wapogoro yaweza kuwa kweli...hata mimi nilipokuwa mahenge niliwahi sikia habari za undugu wa wanyakyusa na wapogoro. Pia wapogoro hufanana pia na wangoni, na wangoni hufanana kiasi fulani na wanyakyusa. Hvyo yaweza kuwa haya makabila ya wangoni, wapogoro na wanyakyusa yana uhusiano wa damu

Upo sahihi hawa wote ni watani
 
Mkuu hakuna uhusiano wowote wa wanyakkyusa na waluguru ila wapogoro. Hapo naona historia inapotoshwa
 
Back
Top Bottom