Shaaban Robert Alizawa (1 Januari 1909 - 22 Juni 1962) alikuwa mshairi na mwandishi wa riwaya. Mchango wake katika lugha ya Kiswahili ni mkubwa kwani kazi zake zinaheshimika katika fasihi ya Kiswahili na pia zinatumika shuleni.
Misha yake
Shaaban Robert alizaliwa
tarehe 1 Januari 1909 katika
kijiji cha Vibambani, jirani na
Machui,
kilomita 10
kusini mwa
mji wa
Tanga.
Wazazi wake wote wawili walikuwa wa
ukoo wa
Mganga wa
kabila la
Wayao, lakini hakujiita Myao kabisa, bali alikuwa mmojawapo wa wachache ambao daima walijiita
Waswahili.
Kabla ya
baba yake kuitwa Roberto
[1], mwanzo alifahamika kwa
jina la Ufukwe na jina hili lilitokana na Mzee Robert kuzaliwa karibu na
ufukwe [2]. Jina la Roberto lilitokana na
tajiri mmoja aliyekuwa amemuajiri baba yake (babu yake Shaabani Robert). Baada tu ya Shaaban Robert kuingia katika shule za
Wazungu alibadili jina kutoka Roberto na kuwa Robert.
Alipata
elimu yake katika shule ya Msimbazi,
jijini Dar-es-Salaam kati ya miaka
1922 na
1926, akawa mtu wa pili katika
wanafunzi kumi na mmoja waliofaulu
mitihani yao na kupewa
shahada ya kutoka
chuoni, yaani School Leaving Certificate.
Akaajiriwa na
serikali ya
kikoloni akawa
karani katika
idara ya
forodha huko
Pangani miaka 1926 –
1944. Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa
kihistoria uliokuwa mahali pa
utamaduni wa
Waswahili tena mahali patulivu kulisaidia maendeleo yake Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili.
Tangu mwaka 1944 hata
1946 alihamia
ofisi nyingine ya Hifadhi ya Wanyama, baadaye ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Tanga (tokea mwaka
1952 hata
1960).
Alipandishwa
cheo kuwa Grade III Higher Division mwaka
1929, na katika mwaka wa 1944 akapandishwa tena kuwa Grade II Local Service.
Kwa ujumla Shaaban Robert aliandika
vitabu ishirini na mbili. Baadhi ya vitabu hivi ni:
Adili na Nduguze,
Kusadikika, Kufikirika, Wasifu wa Siti Binti Saad,
Maisha Yangu Baada ya Miaka Hamsini, Utubora Mkulima.
Vitabu vyake
vimetafsiriwa katika lugha za
Kichina,
Kiingereza na
Kirusi.
Mbali na maandiko yake alikuwa na
athari kubwa katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili akiwa
mjumbe wa
kamati za
East Africa Swahili Committee, East Africa Literature Bureau na
Tanganyika Languages Board. Alikuwa pia mwanachama wa Tanga Township Authority.
Alifariki
dunia huko Tanga tarehe
22 Juni 1962 akazikwa Machui. Aliacha
wake watatu na
watoto watano, ingawa aliwazaa
kumi. Mke wa kwanza alikuwa
Mdigo. Pia aliacha
dada yake (wa baba mmoja) Mwana Saumu, na
mama yake.
Alitunza kwa zawadi ya waandishi inayoitwa ‘Margaret Wrong Memorial Prize’; pia alikuwa ametunzwa nishani ya M.B.E.
Vitabu vyake
- Mwafrika Aimba (1969), Nelson. Nairobi
- Almasi za Afrika (1971), Nelson, Nairobi
- Koja la Lugha (1969), Oxford, Nairobi
- Insha na Mashairi (1967), Nelson, Nairobi
- Ashiki Kitabu Hiki (1968), Nelson, Nairobi
- Pambo la Lugha (1968), Oxford, Nairobi
- Kielezo cha Fasili (1962), Nelson, Nairobi
- Masomo Yenye Adili (1959), Art & Literature, Nairobi
- Mapenzi Bora (1969), Nelson, Nairobi
- Tenzi za Marudi Mema na Omar Khayyam (1973), TPH, Dar-es-Salaam
- Utenzi wa Vita vya Uhuru (1961), Oxford, Nairobi
- Almasi za Afrika Na Tafsiri Ya Kiingereza (1960), Art & Literature, Nairobi
- Mashairi ya Shaaban Robert (1971), Nelson, Nairobi
- Sanaa ya Ushairi (1971), Nelson, Nairobi