Hii habari inaweza kuwa kweli maana niiona mahali, hatar sanaWakatoliki ndio walioanzisha Uislamu Ili kuwaweka waarabu ndani ya utawala mmoja wa kiimani, kabla waarabu walikuwa wakiabudu miungu yao mbalimbali kupitia masanamu Ili iwe rahisi kuwatawala, Majasusi wa Shirika la Jesuit vatican wakaanzisha dini mpya itwayo islam,itakayowaunganisha waarabu wote kiimani mwaka 600 AD. Mapadre watano wa kikatoliki ndio walioandika kitabu cha Quran na kumtafuta mwanamke mfanyabiashara aitwae Bi Hadija na kumpa utajiri. Bi khadija ndie alimtafuta kijana aitwae Muhammad akamkabidhi kwa mapadre wa kikatoliki ndio waliomfunza Quran mapangoni.Ndipo Uislamu ukaenea kwa kasi Sana Katika nchi za kiarabu ambazo zamani zilikuwa ni nchi za Kikristo ukavuka mpaka na kutaka kuingia nchi za Ulaya mashariki kutokea Uturuki Ili kwenda kuiteka Vatican, Majasusi wa Jesuit wakaingia tena vitani wakarudisha nyuma kupitia vita vya msalaba waarabu wakala Sana panga toka vatican wakarudi nyuma, rejea vita vya msalaba na ottoman empire. Majuzi magaidi wa ISIS tokea iraq wakataka kuendeleza mpango ulioshindwa wa ottoman empire kuupenyesha utawala wa kiislamu Ulaya. Wakasambaratishwa na USA na NATO na kumuua Al baghad kiongozi wa ISIS. Huku kundi la ISIL tawi la ISIS Syria likipelekwa kuzimu na ndege za Putin.
Dini zote uzionazo duniani ni tawi la ukatoliki, maprostetant wote ni watoto wa katoliki.
Nimesikiliza vizuri sana, na kiinglish nakipata vizuri sana.Sikiliza vizuri au una lengo lako jengine hapo hapajasemwa njia ya kuwashinda Juja wa maajuja ni kupitia Issa bin mariam au kiengereza huelewi vizuri nikuwekee ya kiswahili ??
🤣 🤣 🤣nani alimshushia hiyo kuran? pia, kwanini alieneza dini kwa upanga? kwanini aliwaelekeza hadi leo hii muuwe wasio waislam? tumewakosea nini?
Hii Ndio ukweli, zingine walichoma.Naona mtunzi alipoona Musa alishushiwa zile amri kumi nae akasema imeshushwa ila kihistoria zilikua nyingi kabla ya utawala mmoja uarabuni kuzikusanya na kuchambua kuiweka kuwa moja na kuzipiga marufuku kuran nyingine kutumika.
Yesu alikuwa Myahudi.NYIE mnaosema muhammad alikuwa anaabudu nini before mulishawahi swali hilo hilo kwa yesu,musa na wengineo?
Wakati wa Yesu kulikuwa na makundi kadhaa ya Wayahudi.Unataka kuniambia wayahudi wakimjua Mungu kwa jina la Yesu ?
Propaganda hizo mkuu. Waislam hujipa moyoKama hakukuwa na uislamu Mona inasemekana watangulizi wake mtume walikuwa waislamu yaani akina Ibrahim Musa na Adam, hapo imekaaje?
Nimesema, uenda Mohammed alikuwa anajua kusoma au alikariri Bible. Ukisoma Quran utaonaUmeandika
Kuhusu Mohamad kushushiwa Quran. Kwa kifupi Mohammad alikuwa ni mtu mwenye akili nyingi sana, ni mtu alieisoma Biblia au alikariri kwa umakini na akaja na idea ya kupinga utatu mtakatifu. Ukweli ni kwamba Mohammad alitunga Quran na kuanzisha dini, na msingi wake mkubwa ulikuwa ni kupinga utatu mtakatifu, ukuu wa Yesu na ufufuko wa Yesu, hizo ndio hoja zake kubwa.
Swali
Lete ushahidi wa haya maneno yako kwamba Mtume alijua kusoma
Mwezi wa ramadhani ulikuwepo kabla ya mtume ni jumla ya miezi katika mwaka wa kalenda ya kiislamu lakini kabla ya mtume hakukuna na swaumu za mwezi mzima Kama ilivyo Sasa Ila swaumu ilikuwepo kabla ya mtume mwezi huu una fadhila nyingi mno kwa waumini wa kiislamu na mtume ametusihi tufunge ndani ya mwezi huu ili kujiongezea thamani ya fadhila zinazopatikana kwenye mwezi huu na kusherehekea kushuka kwa Quran pia na hitisho lake ni siku ya iddy'l fitr ambayo tunasherehekea kukamilika kwa ibada yetuQuran imeshushwaje mwezi wa ramadhani wakati uislam ulianza baada ya kushushwa kwa Quran na Muhammad ndiye aliyekuwa muislam wa kwanza
Kama una aya inaosema kuwa manabii kabla ya Muhammad walikuwa na mwezi wa ramadhani onyesha hapo au reference yoyote kama ipo
Pia kwanini Allah ashushe hadithi ambazo zilikuwa tayar zipo kwenye biblia?
Njoo uthibitishe ya kuwa Biblia ilikuwepo.Yesu kazaliwa mwaka 0 na muhammad mwaka wa 600 huko alafu unasema biblia haikuwepo
nzuriHISTORIA YA QUR'AN.
Sehemu ya Pili (3).
Naam, Kama tulivyopata kuona mwanzo wa DARASA hili juu ya kuteremshwa kwa Qur'an, lakini pia Qur'an imeshushwa kwa lengo la kuwaongoza wanaadamu katika kila kipengele cha maisha ya kila siku ya kibinafsi na kijamii. Lengo la Qur-an linabainishwa katika aya ifuatayo:
👉“Ni mwezi wa Ramadhani ambamo imeshushwa Qur-an ili iwe mwongozo kwa watu na hoja zilizo wazi na upambanuzi (baina ya haki na batili) " (2:185)
Katika kuendea lengo lake hili, Qur-an humuongoza mwanaadamu kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na kijamii na hutoa hoja zenye mashiko dhidi ya wapinzani wake.
Katika kuonesha uwezo wake katika kumuongoza mwanaadamu katika kila kipengele cha maisha yake, Qur-an imeitwa (imesifiwa) kwa majina yafuatayo:
1. Al-Qur-an
Maana yake ni "Chenye kuunganishwa pamoja" au "chenye kusomwa. "Yaani Qur-an ni kitabu kilichofumwa na herufi, silabi, maneno, aya na sura, kinachosomwa mara kwa mara. Kitabu hiki kimeitwa kwa jina hili la "Al-Qur-an" kwa sababu ni mkusanyiko wa mafunzo ya msingi ya maisha ambayo mtu hanabudi kuyarejea mara kwa mara. Qur-an ndio Mwongozo sahihi pekee wa maisha ya mwanadamu hivi sasa.
2. Kalamullah:
Maneno ya Allah (s.w). Qur-an yote ni maneno ya Allah (s.w) yenye kutoa mwongozo kwa walimwengu wote kupitia kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kwa njia ya Wahy kupitia kwa Malaika Jibril (a.s).
3. Al-Mus-haf:
Mkusanyiko wa kurasa. Hili ni jina mashuhuri lililotumiwa na maswahaba wa Mtume (s.a.w) baada ya Qur-an kukamilika kushuka na kuwekwa katika sura ya kitabu kikubwa.
4. Al-Kitaab:
Kitabu pekee (Unique book). Qur-an ni kitabu kikamilifu kisicho na upogo wala dosari yoyote wala hakina mfano wa kitabu chochote kimuundo, maudhui na uwasilishaji wa maudhui hayo. Qur-an yenyewe imeliweka hili wazi katika aya ifuatayo:
👉"Hiki ni kitabu pekee (Al-Kitaab) kisicho na shaka ndani yake na ni mwongozo kwa wamchao Mwenyezi Mungu." (2:2)
5. Al-Furqaan:
Kipambanuzi cha Haki na Batili au ukweli na uwongo. Yaani Qur-an ndio kipimo cha Haki na Batili au Zuri na Baya au Jema na Ovu, Tawhiid na Shiriki, Uislamu na Ukafiri
6. Adh-Dhikru:
Mawaidha au ukumbusho. Qur-an ni mawaidha yenye kumkumbusha kila mwenye kusoma na kuzingatia.
7. At-Tanziil:
Mshuko au wahy kutoka kwa aliye juu. Jina hili linasisitiza kuwa Qur-an ni kitabu cha Allah (s.w) kilichoshushwa kwa njia ya wahy kwa Mtume Muhammad(s.a.w) kupitia kwa malaika Jibril(a.s) ili awaongoze walimwengu kwacho.
8. Al-Hukmu:
Kitabu pekee kinachostahiki kumuhukumu mwanaadamu. Hukumu yoyote kinyume na Hukumu ya Qur-an ni upinzani na uasi dhidi ya Allah (s.w) na ni dhulma dhidi ya wanaadamu kama inavyosisitiza Qur-an yenyewe:
👉“…Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri." (5:44)
👉“….Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu." (5:45)
👉“…. Na wasiohukumu kwa yale alioteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio waasi (mafasiki)." (5:47)
Neno “wasiohukumu” hapa limetumika kwa maana ya wanaoendesha maisha yao kinyume na yale aliyoteremsha Allah au wale wasioendesha maisha yao kwa mujibu wa Qur-an
9. Al-Hikma:
Kitabu pekee chenye Hikima isiyo kikomo. Ni kitabu cha Allah (s.w) ambaye ndiye chimbuko (source) la Elimu na Hekima. Hekima ni jambo la sawa sawa lililofanywa kwa namna ya sawa sawa katika mazingira na wakati wasa wasa ili kufukia lengo tarajiwa. Qur’an ni Hikma na humuuongoza binaadamu aishi maisha ya Hikma.
10. Ash-Shifau:
Ponyo au dawa pekee. Qur-an imeitwa kwa jina hili la "Ponyo pekee" kwa sababu Qur-an ndio dawa pekee ya kuponya maradhi ya "nafsi". Maradhi makubwa ya nafsi ni Ukafiri, Ushirikina, Unafiki na Uasi wa kila aina. Qur-an imejizatiti katika kuyaelezea magonjwa haya ili kila mtu mwenye akili timamu ayafahamu bayana na imeelekeza kwa ufasaha namna ya kuyatibu.
11. Ar-Rahmat:
Rehema kwa watu. Vipawa vinavyomfanya binaadamu atofautiane na wanyama ni akili na elimu. Vipawa hivi vikitumika bila ya kufuata mwongozo kutoka kwa Allah (s.w) humpelekea binaadamu kufanya uharibifu katika ardhi kuliko mnyama yoyote yule. Binaadamu akitumia akili yake na elimu aliyotunukiwa kwa kufuata mwongozo wa Qur-an huwa juu na bora kuliko viumbe vyote.
12. Al-Khayr:
Qur-an ni kheri pekee. Yaani Qur-an ndio chanzo cha kheri zote. Kheri hupatikana kwa kufuata Qur-an vilivyo.
13.Ar-Ruuhu:
Qur-an ni roho ya maisha. Yaani mtu asiyeishi kwa kufuata Qur-an ni kama maiti japo anaishi. Allah (s.w) anawaasa waumini wasiwakumbatie wapinzani wa Qur-an (makafiri) kwani wao ni kama maiti walio makaburini.
👉"Enyi mlioamini! Msifanye urafiki wa ndani na watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia na wamekata tamaa ya akhera kama walivyokwisha kata tamaa makafiri waliozikwa makaburini." (60:13)
14. Al-Bayaana:
Qur-an ni kitabu pekee chenye maelezo ya wazi na kinachofafanua aya zake kwa uwazi kwa kutumia mifano iliyozoeleka katika mazingira ya watu kwa nyakati zote za historia. Hivyo, kila mwenye akili timamu anao uwezo wa kuielewa Qur-an na ikamuongoza.
15. An-Nuur:
Qur-an ni nuru pekee. Qur-an ni mwanga unaomuonesha binaadamu njia sahihi ya maisha itakayomfikisha kwenye lengo la kuumbwa kwake. Kuishi bila ya kufuata Qur-an ni sawa na mtu anayetembea katika giza nene na matokeo ya kutembea kwenye giza nene yanafahamika kwa kila mwenye akili timamu. Qur-an inatukumbusha:
👉"Allah ni kiongozi wa walioamini. Huwatoa kwenye giza na kuwaingiza katika nuru (mwanga). Lakini waliokufuru viongozi wao ni Matwaghuti huwatoa katika nuru na kuwaingiza katika giza. Hao ndio watu wa motoni, humo watakaa milele." (2:257)
16. Al-Burhan:
Hoja pekee iliyowazi. Qur-an ni kitabu kinachotoa hoja zilizo wazi kwa wasomaji wake. Kwa mfano Qur-an inatoa hoja zilizo wazi, kuwa lazima pawe na Muumba mmoja wa ulimwengu na vyote vilivyomo mwenye ujuzi na Hekima. Pia Qur-an pamoja na kutoa hoja maridhawa juu ya kumuamini Allah (s.w) na nguzo nyinginezo za imani , huonesha lengo la kumuabudu Allah (s.w) na umuhimu na hekima ya kufuata Qur-an na Sunnah kama mwongozo pekee wa njia sahihi ya maisha ya binaadamu.
17. Al-Haqq:
Qur-an ni Haki. Qur-an ni haki kwa sababu ni maneno ya Allah (s.w) ambaye ni mjuzi wa kweli aliyeepukana na upungufu wa aina yeyote. Qur-an humuongoza binaadamu kwenye njia ya haki na huhukumu kwa waki.
18. Ahsan-ul-Hadith:
Maneno mazuri au maelezo mazuri kuliko yote kwa kuwa yanatoka kwa Allah (s.w), Mjuzi, mwenye hekima.
Kitabu hiki cha Allah (s.w), kilichosifiwa kwa majina haya, kina aya 6,236 zilizogawanywa katika sura 114 (Rejea jedwali 1). Pia kitabu cha Qur-an (Al-Mas-haf) kimegawanywa kwenye juzuu au mafungu (30) yaliyo sawa sawa.
Inaendelea InshaaAllah...
Allah Ni Mjuzi Zaidi.
Allah akulipe kheriFAHAMU FAIDA KUMI ZA KUSOMA
QUR'AN KILA SIKU
☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆
Mtu Mwenye Kusoma Qur'an Kila Siku Ni Sawa Na Mtu Huyo Kuwa Ni Mwenye Nuru Kubwa Katika Maisha Yake
Ewe Ndugu Yangu Katika Imani Tambua Kwamba Mtu Mwenye Kukisoma Kitabu Cha ALLAH SUBHANA WA TA'ALA Na Akakizingatia Maneno Hayo Ipasavyo Hakika Mtu Huyo Hatopata Tabu Katika Ulimwengu
#FAIDA
1》Qur'an Ni Kinga Katika Majumba Yetu Na Viwiliwili Vyetu
2》Qur'an Ni Msaada Mkubwa Na Huondosha Huzuni Katika Matatizo
3》Qur'an Huleta Furaha Katika Nyoyo Za Wenye Kuisoma
4》Qur'an Ni Shufaa Kubwa Kwa Wenye Maradhi
5》Qur'an Huleta Rizki Za Mali Na Watoto
6》Qur'an Huleta UchaMungu Kwa Wenye Kuisoma
7》Qur'an Huleta Ulinzi Mkubwa Katika Mali
8》Qur'an Huongeza Ufahamu Mkubwa Wa Akili Hasa Kwa Watoto Wanao Soma Elimu Na Wakawa Hawana Ufahamu
9》Qur'an Ni Tiba Halisi Ya Hasidi Anapo Taka Kukuhusudu
10》Qur'an Huleta Ushindi Na Mafanikio Kwa Mwenye Kuisoma
☆☆☆☆☆☆☆☆☆
Tambua Mwenye Kuisoma Qur'an ALLAH SUBHANA WA TA'ALA Humpa Dhamana Mja Huyo Kwa Rizki Zake Zote Za Siku Nzima
#TIBA
Kama Una Matatizo Yako Binafsi Kwanza Hakikisha Swala Tano Unatimiza Kisha Hakikisha Kwa Siku Hukosi Juzuu Moja Hakikisha Una Hitimisha Msaafu
PENDELEA SANA KUSOMA
Sutatul Nass ×3
Suratul Falaq ×3
Suratul Ikhlas ×3
Kila Siku Hakika ALLAH SUBHANA WA TA'ALA Atakupa Nuru Kubwa Ya Maisha Yako Bila Kutegemea
Hii Ndio Sadaka Yangu Kwako Hakikisha Unampa Na Mwenzio Mkono Kwa Mkono Hadi Peponi...
NAMUOMBA ALLAH SUBHANA WA
TA'ALA ATUJALIE MAZINGATIO
TUNAPOISOMA QUR'AN
#Allahummah_Aamiin
Kwa Leo naishia hapa kwenye nakala hizi mpaka wakati ujao wako katika Imani KatetiMQ
Nimesema, uenda Mohammed alikuwa anajua kusoma au alikariri Bible. Ukisoma Quran utaona
Mfano hapa hii Aya ya Surah Al Mahidah 116, ukitafakari vizuri hii ni akili ya Mwanadamu ikitunga majungu
Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana.