Historia ya ngome kubwa ya Ugiriki

Historia ya ngome kubwa ya Ugiriki

Chilojnr

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
308
Reaction score
1,354
Najua hili somo litakuwa refu sana na lisiweze kuisha hata mwaka huu. Nitajitahidi sana kuwaandikia kuhusu Wagiriki, walipoanzia mpaka sasa hivi, ni kwa namna gani waliwahi kuitawala dunia, moja ya tawala iliyokuwa na nguvu sana ukiachana na China, Warumi na hata Wamarekani ambao tunao sasa hivi.

Nitaandika mengi sana, yaani kwa kifupi ni kwamba tunaingia darasani. Kama wewe hukupenda historia tangu darasani, hapa tuache tu kwa kuwa tunazama ndani, tunachimba na kuchimbua, tukitoka hapa, utakuwa umewaelewa Wagiriki kwa undani sana, yaani ukisikia mtu anazungumzia Wagiriki, hautoshangaa, utakuwa umewajua, na utakuwa umeyajua mengi kuhusu wao kuliko hata mwanafunzi aliyeingia darasani kusoma.

Okay! Acha nianze kuwaelezea kwa undani kabisa kuhusu hawa watu. Kumbuka hili somo haliishi leo hata kesho, nyie tusomeni mpaka pale tutakapoona imetosha.

Abdera: Huu ni mji muhimu sana kule Ugiriki, upo Kaskazini mwa Pwani ya Aegean, karibu na mto wa Nestos. Abdera ilikuwa sehemu maarufu sana ya kufanyia biashara kipindi hicho cha zamani. Watu walikuwa wakitoka na meli zao sehemu mbalimbali duniani na kwenda huko kuhakikisha biashara zao zinafanyika vizuri. Yaani kwa miaka hiyo ya nyuma, sehemu hii ilikuwa ni kitovu kikubwa cha biashara.

Huu mji uligunduliwa na kabila la Herakles ambao walikuwa wakiongozwa na Abderos. Mji huu uligunduliwa mwaka 650 Kabla ya Kristo.

Mji ulidumu kwa miaka kadhaa kabla ya kuharibiwa na kabila la Thracians lakini baadaye wafanyabiashara wa watumwa hapo Ugiriki wakaujenga upya, hiyo ilikuwa ni mwaka 545 Kabla ya Kristo.

Wagiriki hao wafanyabiashara ambao waliamua kwenda kuujenga upya walitoka sehemu iitwayo Teos, mji uliokuwa Magharibi mwa Ugiriki, karibu na sehemu iitwayo Ionia.

Miongoni mwa watu waliamua kwenda kuishi mahali hapo alikuwemo dogo aliyeitwa Anacreon. Wakati huo mfalme wao aliitwa Cyrus wa Kwanza.

Kama ilivyokuwa kwa makoloni mwengine sehemu nyinginezo, Abdera ilikuwa ikifanywa biashara na watu mbalimbali ambao walikuwa wakipeleka mbao, almasi, dhahabu na hata watumwa waliokuwa wakipatikana vitani.

Baadaye mji huu ukakabidhiwa kwa Mfalme wa Persian aliyeitwa Xerxes na yeye akawa mfanyabiashara mkubwa mjini hapo ila baada ya Persian kupigwa mwaka 479 Kabla ya Kristo, mji huu ukawa mwanachama muhimu wa Athenian ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Delian League. Kwa maana hiyo Abdera ikaanza kulipa kodi kila mwaka kwa hao Dealian League.

Wagiriki wengine waliwaona hawa watu wa Abderan kuwa wajinga sana kwa sababu mji huo ulikuwa ukitoa watu wenye akili zaidi ya wawili kwa mwaka. Hii ilimaanisha nini? Kwamba kulikuwa na miji ilikuwa inajitawala yenyewe kupitia watu wenye akili, watu hawa walikuwa na uwezo wa kuziongoza serikali kimapato na kila kitu, hazikuweza kutawalika.

Sasa hawa Abderans walionekana wajinga kwa sababu hiyo tu. Walikuwa na watu wenye akili kama Protagoras na Demokritus lakini pamoja na kuwa na watu hao, bado walitawalika.

Mwaka 404 Kabla ya Kristo, Abdera ikatawaliwa na Spartans lakini baadaye walikuja kupigwa na Athens katika vita viitwavyo Peloponnesian. Hivyo baada ya hapo huu mji ukaanza kulipa ushuru na kodi zake kwa Athenian League ambao ulikuwa unaongozwa na Mfalme wa Macedonia aliyeitwa Philip wa Pili.

Abdera ikabaki kuwa chini ya utawala wa Macedonia kwa miaka 180. Katika karne ya nne, mji ukaanza kupanuka upande wa Kusini. Sasa hapo Abdera ikaanza kuwa bize kupitia bandari zake mbili, wakaingiza pesa nyingi lakini baadaye wakaja kupigwa na majeshi ya Kirumi mwaka 170 Kabla ya Kristo katika vita vya Tatu vya Macedonia. Sasa mji huo ukaanza kutawaliwa na Warumi, hivyo ushuru na kodi zote za bandari na vinginevyo vikaanza kwenda kwa hawa majamaa.
***
Akademia Ilikuwa sehemu nyingine ya kupata elimu zaidi iliyokuwa ikipatikana mbali kidogo na Mji wa Athens, sehemu hii ilikuwa inaongozwa na jamaa aliyeitwa Akademos. Katika karne ya sita, moja ya sehemu kubwa ya mazoezi huko Ugiriki ilipatikana mahali hapa.

Katika mwaka 387 Kabla ya Kristo, Plato alinunua ardhi mahali hapo na kujenga shule ya wanafilosofi ambapo baadaye ikaja kuwa chuocha kwanza kujengwa huko Magharibi. Lengo la Plato lilikuwa ni kuwafundisha viongozi wa baadaye. Hapa ndiyo tunarudi palepale nilipowaambia kipindi cha nyuma kwamba Ugiriki walipata elimu kabla ya Misri na Warumi, wao walikuwa na elimu zao, ustaarabu wao na ndiyo maana walitoa wasomi wengi waliotingisha dunia.

Wasomi hao kipindi hicho hawakulipia ada, walikuwa wakisoma bure kabisa, na walikuwa wakifundishwa kwa namna ambavyo Plato alihitaji wao wafundishwe. Walifundishwa Hisabati, mashairi na Platonic ambayo ilijulikana kama Dialectic.

Kipindi hicho ni wanafunzi wawili ndiyo walionekana kuwa na uwezo mkubwa, ambao walifaulu vizuri sana, wanafunzi hao walikuwa ni Mwanahisabati na Mwanaanga, Knidos na Mwanafilosofo Aristotle. Huyu Aristotle ndiye ambaye alionekana kuja kuwa mrithi wa Plato kama rais wa chuo hicho lakini baada ya Plato kufariki, viongozi wa chuo wakamchagua binamu yake Plato aliyeitwa Speusippus kuwa mrithi.

Baada ya kuona amezinguliwa, Aristotle akaamua kujenga chuo chake mwenyewe na kukiita Lyceum

Chini ya rais Speusippus na warithi wake, chuo chao kiliendelea kuwa na watalaamu wa Hisabati hadi Arcesilaus wa Pitane (rais kuanzia 265 mpaka 242 Kabla ya Kristo) kuanza kufundisha masomo ya Filosofa.

Baada ya Warumi kuivamia Ugiriki mwaka 146 Kabla ya Kristo), chuo hicho cha Academy kikawavutia Warumi wengi kwenda kupata elimu humo. Chuo hicho kilidumu kwa miaka 900 kabla ya Mtawala wa Christian Byzantine aliyeitwa Justinian kukifunga chuo hicho na vyuo vingine.

Itaendelea....
IMG-20230621-WA0043.jpg
 
Itaendelea....View attachment 2664193
Acha michezo bwana mdogo uiendeleze hii story mpaka mwisho

Tumeelewanaaaa???
JamiiForums790734876.jpg
 
Tawala KUU nne za Dunia.

Usipozikuta kwenye bible utazikuta kwenye history Darasani.

1 .Babeli.
2. umedi na Ujemi.
3. UYUNANI. ( Grece.).
4. Roman Empire
Kwenye bible zimeandikwa wapi?
Halafu mbona Islamic ottoman empire haimo wakati ilisumbua kulkko hata hizo Uyunani na umedi na ajemi??
 
Kwenye bible zimeandikwa wapi?
Halafu mbona Islamic ottoman empire haimo wakati ilisumbua kulkko hata hizo Uyunani na umedi na ajemi??

Bible Imeandika hizo tawala zote KUU nne za Dunia.

Kwenye maagano yote mawili.
Agano la kale na Agano jipya.

Na Huu utawala wa Rumi ndio utawala wa MWISHO kabla ya Yesu kurudi kwa mala ya pili.
 
Huwezi izungumzia Ugiriki bila ya kuizungumzia Misri. Hao wanazuoni wote wa kigiriki walisoma Misri. Aristotle alienda Misri kusoma kwa miaka 20. Plato alienda Misri kusoma kwa miaka 13. Ustaraabu na elimu yote ya Wagiriki, kuanzia hesabu, ujenzi, afya, dini, falsafa, sayansi nk, waliiga kutoka Misri.
 
Bible Imeandika hizo tawala zote KUU nne za Dunia.

Kwenye maagano yote mawili.
Agano la kale na Agano jipya.

Na Huu utawala wa Rumi ndio utawala wa MWISHO kabla ya Yesu kurudi kwa mala ya pili.
Hivi Yesu amewasiliana na nani ya kwamba anarudi??na anarudi kutoka wapi??
 
SEHEMU YA PILI

Achaea ni sehemu moja maarufu sana iliyokuwepo tangu kipindi cha nyuma. Hii sehemu ama mji inapatikana sehemu mbili, ya kwanza ni huko milimani upande wa Kaskazini ilipojulikana kama Peloponnes na pia ilipatikana katika eneo dogo lililoitwa Thessaly.

Sasa hapo Achaea kulikuwa na miji kumi na mbili ambao nao sasa waliform muungano wao na serikali zao. Sijui umenielewa hapa. Acha nikufafanulie vizuri. Achaea ilikuwa kama yale majimbo ya Marekani ambayo yaliamua kujiunga na kutengeneza taifa moja. Sasa ndiyo kama wao. Yaani ni miji kumi na mbili ambayo ikaamua kujiunga na kuwa mji mmoja wa Achaea.

Sasa hawa Achaea wakaamua kuweka league yao kwa ajili ya kukusanya mapato ya kibiashara yaliyokuwa yakipatikana. Hiyo league ilianzishwa karne ya tano na ilidumu kwa karne nne.

Hapa unaweza kujiuliza kwa nini hawa watu waliamua kujiunga? Ni kwa sababu kipindi hicho ndicho kulipoanza vita na Mfalme Phillip wa Macedonia. Waliona kabisa kama wangepigana naye mmoja mmoja wangeshindwa na ndiyo maana wote kumi na mbili wakaamua kujiunga na kuwa mji mmoja.

Achaea ilikuwa ni sehemu muhimu sana kwenye ukoloni wa Kigiriki kwa kuwa ilikuwa ni sehemu kubwa na iliyokuwa ikiingiza sana pesa. Kwa maana hiyo Wagiriki waliishikilia kwa nguvu zote ili isiweze kutekwa na mtu yeyote yule.

Baadaye hawa Achaea wakaendelea kujitanua zaidi mpaka nchini Italia ambapo huko wakachukua miji kadhaa ikiwemo Croton na Sybaris ambapo ilipatikana kwenye eneo moja lililoitwa Magna Graeca. Ukisoma historia, hii miji miwili baadaye iliharibiwa kwa kuchomwa moto, Waitalia walimaindi kishenzi, sasa wakasema tukose wote ila si miji hii kuchukuliwa na Wagiriki.

Mji uliokuwa muhimu sana kwa Achaea ulikuwa ni Sicyon uliokuwa huko Corith. Mji huu ulikuwa ukiongozwa na Tyrant, baada ya hao majamaa kukimbizwa, sasa mji huo ukaanza kuongozwa na jamaa aliyeitwa Aratus ambaye alikaa madarakani kutoka mwaka 251 – 213 Kabla ya Kristo.

Baada ya Aratus kugundua kwamba Tyrant wanaweza kujiunga na kumuangusha, akaamua kuuingiza mji huo katika muungano wa Achaean League ili kujilinda, ni kama Finland alivyoamua kujiingiza NATO ili apate ulinzi wa kijeshi dhidi ya Mrusi ambaye alikuwa bize akimshambulia Ukraine. Nadhani umenielewa hapo.

Kwa hiyo Achaea ikazidi kuimarika na kupata nguvu zaidi na zaidi.

Kwa sababu Ugiriki na Macedonia walionekana kama hawaivi, Aratus pia akaamua kuichukua ardhi ya Kaskazini mwa Peloponnese ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Macedonia. Kwa hiyo Achaean League wakamwambia Macedonia aachane na mji huo vinginevyo angepokea kichapo kikali, akaamua kuuachia mji huo. Sasa hapa Ugiriki ikazidi kujijenga na kuwa mkubwa zaidi huku wakiwa na mpango mkakati wa kutawala sehemu kubwa huko Ulaya.

Kwa kuwa mfalme wa Macedonia aliona kabisa ameshindwa, hivyo akakimbilia kwa Warumi (Roma) na kuhitaji nguvu zaidi kwani Achean League walionekana kuwa tishio, hapo ndipo Warumi wakaingia vitani kupambana na Achean katika vita ambavyo Warumi walishinda na hivyo Achean yote kuwa chini ya utawala wa Kirumi.
***
Achilles ni eneo mojawapo huko Ugiriki ila hili jina lilitokana na shujaa wao wa zamani katika Vita vya Trojan ambaye alikuwa ni mtoto wa shujaa mwingine aliyeitwa Peleus ambaye alizaa na mungu wa kike aitwaye Thetis.

Ukisoma stori za Kigiriki, huyu Achilles amezungumziwa sehemu nyingi sana. Katika vita vya Trojan, huyu jamaa alifanikisha ushindi mkubwa na mwisho kabisa kumchinja jamaa aliyeitwa Hector, huyu Hector alikuwa mwamba sana kipindi hicho, aliogopeka kwa kuwa alikuwa na nguvu mno ila hilo halikuwa tatizo kwa Achilles, alifanikisha kumuua mapigano hayo yaliyodumu kwa muda mrefu. Hapo nazungumzia mwaka 750 Kabla ya Kristo.

Achilles alikuwa mbabe wa vita kipindi hicho, alikuwa hashikiki linapokuja suala la kupambana vitani kwa mapanga na farasi.

Sasa kwenye hiyo vita ya Trojan kuna kastori fulani kazuri sana hapa. Unajua ilikuwaje mpaka jamaa akaamua kwenda kwenye hiyo vita na jeshi lake? Hapa kumbuka jambo moja kwamba zamani watu walikuwa wakiwateka mateka wa kike na kuwaweka ndani ya nyumba zao na kuwatawala kingono.

Sasa kipindi hicho kamanda wa vita, Mfalme Agamemnon alichukua mateka wa kike aliyeitwa Briseis kitu kilichomkera sana Achilles kwa kuwa naye alionekana kuvutiwa na huyo mwanamke, hilo likasababisha ugomvi mkubwa, mwisho wa siku Achilles akasema anajitoa yeye na jeshi lake, hatokwenda vitani kupambana na Hector. Mfalme hakujali, akasema wewe jikatae, hivi vita tutashinda bila wewe.

Watu wakaingia vitani kupambana na Hector. Huyu jamaa hakuwa mtu wa huruma, wakati Achilles akiwa amejitoa, mfalme akamchagua Patroklus aongoze majeshi kwenda kwenye uwanja wa vita, tena akiwa amevalia mavazi ya vitani ya Achilles.

Patroklus hakuwa na nguvu za kupambana na Hector, yeye na majeshi yake wakajikuta wakipigwa vibaya sana na kushindwa kwenye vita hivyo vya Trojan. Hector akauchukua mwili wa Patroklus na kuukatakata vipande.

Taarifa ya kifo cha Patroklus ikamfikia Achilles. Hasira zikampanda kwa kuwa jamaa alikuwa swahiba wake mkubwa, akaona endapo angekaa tu nyumbani na kuendelea kula bata lisingekuwa jambo zuri hata kidogo, hivyo akaamua kuwaambia vijana wake kwamba muda wa vita ulifika na ilikuwa ni lazima kwenda kupambana kumlipia kisasi swahiba wake.

Kwa kuwa mavazi yake ya kivita yalichukuliwa na Patroklus, yeye akaamua kuchukua mavazi ya mungu wao, Hephaistos na kuingia vitani. Alipambana sana kwenye vita hivyo na kufanikiwa kumuua Hector, akauchukua mwili wake na kurudi nao Ugiriki na kwenda kuutundika mahali ili kila mtu auone na kuona ni kwa namna gani alipambana na jamaa huyo hatari na kumuua.

Baada ya siku kadhaa, baba yake Hector, Mfalme Priam akaomba sana kurudishwa kwa mwili wa mtoto wake ili auzike kwa heshima zote, ombi lake lilikataliwa mara ya kwanza lakini baadaye likakubaliwa na hivyo mwili kuchukuliwa na kurudishwa huko nyumbani kwao na kuzikwa kwa heshima.

Ukisoma vitabu vya Kigiriki viliandika kwamba baada ya miaka mingi kupita, Achilles alikuja kuuawa na watu walioamua kujiunga, yaani mtoto wa Mfalme wa Trojan aliyeitwa Paris na mungu Apollo.

Ukiendelea kusoma vitabu vya Kigiriki vinaeleza kwamba kipindi ambacho Achilles alizaliwa, mama yake alitaka kumfanya kuwa mtu asiyekufa (Immortal) hivyo alimchukua akiwa mtoto na kutaka kumtupa kwenye mto Styx (Mto huu ulikuwa ni wa moto, yaani muda wote unachemka)

Huku akiwa amedhamiria kufanya hivyo, ghafla watu wakatokea, lakini tayari mguu wa kulia wa mtoto ulikuwa umekwishatumbukizwa ndani ya maji, hivyo Achilles akakua na kukua huku mguu wake mmoja ukiwa umeungua. Na hata siku alipokwenda kupigana katika Vita vya Trojan mama yake alijua asingeweza kurudi akiwa hai, ila bahati nzuri kwake alirudi akiwa hai huku akiwa na mwili wa Hector kuonyesha walishinda vita hivyo.

Katika kipindi ambacho walikuwa wakipigana vita, kila mmoja huko Ugiriki alijua kabisa Achilles asingeweza kurudi akiwa hai, nini kifanyike kipindi alichokuwa vitani? Wakaona ni bora watoto wake wafichwe kwa sababu walijua endapo angeshindwa, Hector angekwenda huko na kutaka kuimaliza familia yake yote.

Hivyo mawasiliano yakafanyika. Thetis wakapanga na Mfalme Lykromedes wa Kisiwa cha Skyros kuwaficha watoto wa Achilles, Deidameia ambaye alikuwa wa kike na wa kiume aliyeitwa Neoptolemus.

Kushinda vita kwa Achilles kukawa kumekamilisha unabii uliowahi kuwekwa huko nyuma kwamba kamwe wasingeweza kushinda vita hivyo bila Achilles, kama kweli Wagiriki walitaka kushinda vita ilikuwa ni lazima kwenda na Achilles, yeye ndiye ambaye angevimaliza vita hivyo, na kweli unabii huo ukawa umekamilika.

Katika maisha yake ya vita, Achilles alifanikiwa kushinda vita dhidi ya Hector, Cycnus, Troilus, Malkia Pnenthesilea wa Amazon na Mfalme wa Ethiopia aliyeitwa Memnon.

Achilles alikufa baada ya kupigwa mshale wa mguuni na Paris ambaye alikuwa akipigana vita na kulindwa na kikosi cha Apollo. Ukisoma stori za Kigiriki zinasema kwamba mshale huo ulikuwa na sumu hivyo baada ya kupigwa mguuni, mguu ulianza kuoza kwa haraka sana kitendo kilichopelekea kifo chake akiwa vitani.

Kumbuka ili uijue Ugiriki ni lazima ujue maeneo yake na watu ambao waliwahi kuipigania vita na kushinda ama kupigwa.

Itaendelea.
 
Tawala KUU nne za Dunia.

Usipozikuta kwenye bible utazikuta kwenye history Darasani.

1 .Babeli.
2. umedi na Ujemi.
3. UYUNANI. ( Grece.).
4. Roman Empire
Hizo tawala namba Moja na mbili zilikuwa noma sana enzi zake... Enzi za kina mfalme Nebuchadnezzar, koo ya wakaldayo ambayo mungu alimpiga marufuku Suleiman asioe huko.. dah ni hatari sana . Tawala hizi ndio ibada za kishetani zilikuwa zinafanyika sana na ndio chimbuko la illuminati
 
Kwenye bible zimeandikwa wapi?
Halafu mbona Islamic ottoman empire haimo wakati ilisumbua kulkko hata hizo Uyunani na umedi na ajemi??
Hizi tawala zipo kwenye kitabu Cha Daniel
 
Hizo tawala namba Moja na mbili zilikuwa noma sana enzi zake... Enzi za kina mfalme Nebuchadnezzar, koo ya wakaldayo ambayo mungu alimpiga marufuku Suleiman asioe huko.. dah ni hatari sana . Tawala hizi ndio ibada za kishetani zilikuwa zinafanyika sana na ndio chimbuko la illuminati
Hatari sana.
 
mungu wa kike, kumbe akina Zumaridi walikuwepo tu?
 
Back
Top Bottom