Historia ya Mahakama Tanzania

Mwandwanga

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,059
1,568
Mfumo wowote wa maisha ya binadamu lazima uwe na sheria, kanuni au miiko inayoongoza jamii husika. Kadhalika lazima kuwe na utaratibu wa kuamua migogoro inayotokana na ukiukaji wa sheria, kanuni au miiko hiyo. Kwa sababu hizo, Tanzania imekuwa na mfumo wa kutatua migogoro kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya uhuru.

Mahakama ya Tanzania katika ukuaji wake kuanzia kipindi cha Uhuru hadi sasa imepitia katika matukio makuu kama ifuatavyo:-

• Mwaka 1964, majaji wawili wazawa waliteuliwa. Majaji hao ni Mhe.Augustino Said (baadaye aliteuliwa kuwa Jaji Mkuu) na Mhe. Merk P.K.Kimicha. Ikumbukwe kwamba kabla na baada ya Uhuru kulikuwa hakuna Jaji mzawa.

• Mwaka 1965, Bw.S.Tukunjoba aliteuliwa kuwa Msajili wa Mahakama ya Kuu wa kwanza mzawa.

• Mwaka 1971, Tanzania ilipata Jaji Mkuu wa kwanza mzawa, Mhe.Augustino Said.

• Mwaka1974, Mhe. Julie Manning aliteuliwa kuwa Jaji mwanamke wa kwanza wa Mahakama Kuu.

• Mwaka 1979, Mahakama ya Rufani ya Tanzania ilianzishwa kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

• Mwaka 1979, Mhe. Francis.L. Nyalali aliteuliwa kuwa Kiongozi wa Mahakama ya Rufani na hivyo kuwa Mkuu wa iliyokuwa Idara ya Mahakama.

• Mwaka 1979, Mhe. Nassoro S. Mnzavas aliteuliwa kuwa Jaji Kiongozi wa kwanza.

• Mwaka 1979, Bw.C.G. Mtenga aliteuliwa kuwa Msajili wa kwanza wa Mahakama ya Rufani na cheo cha Msajili Mahakama ya Rufani kilitambuliwa na kupewa hadhi sawa na Katibu Mkuu wa Wizara.

• Mwaka 1981, iliyokuwa Idara ya Mahakama ilishusha madaraka ya uongozi kwenye Kanda, Mikoa na Wilaya (decentralization).

• Mwaka 1981, Mahakama ilianzisha Kurugenzi tatu.Kurugenzi hizo ni Kurugenzi za Mahakama ya Wilaya hadi Rufani, Kurugenzi ya Mahakama za Mwanzo na Kurugenzi ya Utawala na Utumishi.

• Mwaka 1987, Kamati za Kusukuma Mashauri ya Jinai (Case flow Management Committes) zilianzishwa kupitia Waraka Na.2/1987 wa Jaji Mkuu.

• Mwaka 1993, kupitia Waraka wa Jaji Mkuu Na.3/1994 utaratibu wa kila Jaji na Hakimu kuwa na ratiba binafsi ya mashauri (individual calendar) uliazishwa.

• Mwaka 1994, iliyokuwa Idara ya Mahakama kwa kupitia mabadiliko ya Sheria kuendesha mashauri ya madai (Civil Procedure Code Act) utaratibu wa suluhu kwenye mashauri ya madai (Alternative Dispute Resolution - ADR) ulianzishwa.

• Mwaka 1994, lilitolewa tamko la Morogoro na Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Idara ya Mahakama ikiwa na lengo la kuhifadhi mazingira.

Mwaka 1996, Siku ya Sheria ilianzishwa ikiwa na madhumuni ya kuadhimisha kuanza rasmi kwa shughuli za Mahakama na pia kutoa ujumbe maalum kwa umma kuhusu Mahakama.

• Mwaka 1997, Julai Mahakama ya Watoto ilaanza rasmi katika jengo tofauti na Mahakama zingine maeneo ya Kisutu.

• Mwaka 1999, Septemba Mahakama Kuu (T) Divisheni ya Biashara ilianzishwa

• Mwaka 1999, Kamati za Mahakama na Mawakili (Bench Bar Monitoring Committees) kushughulikia na kutatua ucheleweshaji wa mashauri ya madai zilianzishwa. • Mwaka 2001 Mei, MahakamaKuu (T) Divisheni ya Ardhi ilianzishwa.

• Mwaka 2004, Mhe.Eusebia N.Munuo aliteuliwa Jaji mwanamke wa kwanza wa Mahakama ya Rufani.

• Mwaka 2004 Sheria ya kuanzishwa Divisheni ya Kazi ya Mahakama Kuu ya Tanzania ilipitishwa na Bunge.

• Mwaka 2005, iliyokuwa Idara ya Mahakama ilipewa hadhi ya kuwa Muhimili wa dola na kuitwa Mahakama ya Tanzania.

• Mwaka 2007, Februari ulianza utaratibu wa Siku ya Sheria kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa dola.

• Mwaka 2007, Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ilianza kazi rasmi.

• Mwaka 2010, Tovuti ya Mahakama www.judiciary.go.tz ilianzishwa kukidhi maendeleo ya kiteknologia. Uzinduzi wa tovuti hii uliendana sambamba na utumiaji wa vifaa maalum vya kurekodi mashauri. Aidha Tovuti ya Mahakama Kuu (T) Divisheni ya Biashara ilianzishwa (www.comcourt.go.tz ).

• Mwaka 2010, Kada ya Wasaidizi wa Sheria wa Majaji ilianzishwa.

• Mwaka 2011, Sheria ya usimamizi wa Mahakama (Sheria Na.4/2011) ilipitishwa na Bunge na kuanzisha Mfuko wa Mahakama.

· Mwaka 2016 mahakama ya Mafisadi yaanzishwa rasmi kushughulikia wahujumu wa uchumi nchini.

©Mchwa Shababi
 
shukrani mkuu kwa uzi mzuri
 
Back
Top Bottom