Kati ya mwaka 1947 mpaka 1975 wakoloni waingereza walikuwa ni wamiliki wa kiwanda kilichokuwa kinaitwa TANGANYIKA PACKERS LTD (TPL) kiliajiri wafanyakazi zaidi ya 1200 na walikuwa wanafanya kazi kwa shift na walichukuliwa kwa mabasi ya kazini, mpaka mwaka 1975 serikali ilikitaifisha kutoka kwa waingereza kuingia serikalini kufuatia sera za ujamaa.
Kiwanda kilikuwa kikubwa sana, kikisindika nyama za kusaga kwenye makopo na kusafirisha nje ya nchi mpaka kwa malikia wa Uingereza, Neno KAWE maana yake ni COW WAY yaani njia za ng'ombe, Serikali ilivyokichukua tu kwanza walinyimwa leseni ya kusafirisha nje (walinyimwa cheti kilichokuwa kinaitwa PHYTOSANITARY CERTIFICATE cheti cha kuthibitisha ubora wa vyakula vya package)
hivyo soko la ndani likawa gumu kikawa kinasambaza nyama zake kwenye mabucha ya Dsm na badae kija kufa mwaka 1993!
Pana mbunge mmoja wa kawe alikinunua kwa Bei ya chini sana nae akashindwa kukiendesha hatimae akaanza kuuza mashine na baadhi ya vipuri kama chuma chakavu na mwishoe kikafa kabisa!
Baada ya kufa kabisa familia nyingi za Kawe zilikosa ajira na kuanza kuhangaika huku na kule
Maono ya mamlaka yameonelea ni heri kuyapangisha majengo husika kwa manabii na mitume ili wawaombee wakazi wa Kawe na Watanganyika wengine wapate ajira kwa njia za miujiza huku wakilipia huduma hiyo kwa njia ya sadaka nk