Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Ndugu zangu wanaJukwaa La Historia nianze kwa kupongeza juhudi tukufu za mheshimiwa Kichuguu kwa kuanzisha hoja ya kuundwa kwa jukwaa hili na wale wote waliochangia na kuunga mkono hoja (siwezi kutaja wote kwasababu hili sio jukwaa la kutajana majina)
Leo kwa kuanzia au kupasha misuli ningependa nitoe historia fupi ya bwana Karl Marx baba wa Scientific Socialism,
Karl Marx alizaliwa mwaka 1818 huko Trier Prussia ambayo ni Ujerumani kwa sasa (kama nimekosea naomba marekebisho). Baba yake ni Myahudi ambaye alibadiri imani yake na kuamini katika Ukristu,
Marx alisoma katika vyuo vya Bonn na Berlin akiwa ameegemea zaidi kusomea History (historia), Philosophy(falsafa), Jurisprudence (sijajua kiswahili inaitwaje) na Political Economy (siasa ya uchumi).
Baadae Marx alienda Paris Ufaransa huko ndiko alikokutana na mwana Ujamaa mwingine Friedrich Engels ambaye nadhani aliishi tangu mwaka 1820-95 (kama siko sahihi nitaomba maoni).
Mwaka 1847 aliombwa kuandaa Manifesto ya German Communist League In Paris ndipo mwaka 1848 alifanikiwa kuandaa vitabu viwili 1- Communist Manifesto na 2-Das Kapital. Kwa upande wangu nimewahi kusoma kitabu cha Communist Manifesto japo kwa ufupi humo ndani jamaa ametoa theory nyingi sana kuhusu matatizo ya wafanyakazi kupitia hicho kitabu utapata suluhu ya migomo ya madaktari na waalimu hapa nchini, mfano kuna sehemu anasema "Wakulima na wafanyakazi wanauwezo wa kuliondoa tabaka tawala" kama haliwaridhi.
Vitabu hivyo vilisaidia sana kufanikisha mapinduzi ya Urusi 1917 (nitasimulia siku nyingine), mapinduzi ya Ufaransa 1879 (pia nitasimulia muda upo wakuu) na mapinduzi ya mwaka 1848 yaliyotokea sehemu nyingi ulaya.
Nimeshindwa kuelezea kifo chake kwa kuwa sijapata chanzo na mwaka (Kama kuna mdau anajua ni vema akatiririka hapa).
Ndugu zangu wanaJF nimeamua kutoa utangulizi huu kwasababu Karl Marx ni chanzo cha historia nyingi hapa ulimwenguni.
Ahsanteni sana
Source: Kitabu cha "A History Of Modern Times" by C.D.M KETELBEY.
Nilikinunua 1000 kwa wale wanaomwaga chini najua haiwahusu lakini nilitaka kuwasihi msivizarau vile vitabu vina mengi.

Last edited by a moderator: