Historia ya Julius Nyerere, Sumbawanga 1959 kwa maneno ya Dkt. Mzindakaya

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
MAKALA YA DR. MZINDAKAYA KATIKA HABARI LEO: NYERERE ALITEULIWA AKIWA SUMBAWANGA

Naweka hapo chini makala kuhusu harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kama alivyosimulia Dr. Mzindakaya kisha nami nitaweka historia hiyo hiyo kama nilivyoiandika katika kitabu cha Abdul Sykes kuikamilisha:

Mzindakaya: Nyerere aliteuliwa akiwa Sumbawanga

habarileo.co.tz10/13/2020

MWANASIASA mkongwe nchini Dk. Chrisant Mzindakaya amesema, Gavana wa Serikali ya kikoloni ya Uingereza Edward Twining alipomteua Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere awe Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika alikuwa katika ardhi ya Ufipa - Sumbawanga.

Alilieleza HabariLEO kuwa, mwaka 1959 Hayati Baba wa Taifa Nyerere alikuwa katika ardhi ya Ufipa ambayo ni mkoa wa Rukwa kwa sasa.

Mkoa huo ulianzishwa 1974 na Mji wa Sumbawanga ukawa Makao makuu. Wakati huo Sumbawanga ilijulikana kama Ufipa District.

Akizungumzia hilo Dk Mzindakaya alisema anakumbuka mwaka 1959 wakati Baba wa Taifa akiwa katika mji mdogo wa Sumbawanga Gavana Edward Twinning alimteua kuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika hivyo ilimlazimu kusafiri kwa gari hadi nchi jirani ya Zambia ambako alipanda ndege kwenda Dar es Salaam .

Alisema wakati huo kulikuwa hakuna barabara iliyokuwa iliunganisha Sumbawanga na Mji wa Mbeya.

"Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alilazimika kukimbizwa na gari hadi nchini Zambia ambako alipanda ndege kuwahi sherehe za kuapishwa kwake...itoshe kusema enzi hizo ukitaka kusafiri kwenda Dar kwa ndege kutokea Mbeya ilitulazimu kwanza kupitia Mwanza.... hakukuwa na barabara ya kutoka Sumbawanga hadi Mbeya “alisema Dk Mzindakaya.

Alisema, wakati huo kulikuwa na ndege iliyojuliakana grasshopper "panzi' iliyokuwa na kasi ndogo hivyo safari ya Mbeya – Dar ilichukua saa sita na ile ya Mwanza hadi Dar saa tano.

Dk Mzindakaya alisema, hadi mkoa wa Rukwa unaanzishwa mwaka 1974 ulikuwa nyuma kiuchumi hadi Mwalimu Nyeyere alipofanya maegeuzi makubwa ya kilimo miaka minne baadaye kwa kuutangaza kuwa ni mkoa huo ni miongoni mwa mikoa nchini inayolima chakula kwa wingi.

Aidha machifu wa kabila la Wafipa walisema, walikuwa wa kwanza kumzawadia Baba wa Taifa fimbo ikiwa ni ishara ya kumkubali na kumpa nguvu na baraka za kutawala nchi akiendelea na harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika.

Mwenyekiti wa machifu Mkoa wa Rukwa, Chifu Kutazunga Sisampa Sichula wa Himaya ya Mambwe alilieleza HabariLEO kuwa, barua ya wito kwa Mwalimu Nyerere kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa (UNO) katika Jiji la New York nchini Marekani aliipokea akiwa katika ardhi ya Ufipa.

"Aliipokea barua hiyo akihudhuria mkutano wa chama cha TANU katika kijiji cha Mpui sasa kiko katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga”alisema Chifu Sichula.

Alisema, barua hiyo Mwalimu alipewa na Dantesi Ngua ambaye alikuwa ni mtoto wa Mwene Maria (mdogo wa Chifu Agustina Nti wa Wafipa Himaya ya Lyangalile) mwaka 1959...barua hiyo ndiyo iliyosababisha Tanganyika kupata madaraka ya kiserikali." alisema.

Chifu Sichula alisema, wakati Mwalimu Nyerere alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika alikuwa katika mji mdogo wa Sumbawanga akiwa kwa rafiki yake, marehemu Baba Askofu Kalolo Msakila, ambaye alikuwa ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga.

"Mwaka 1970 Mwalimu Nyerere alihamishia kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja vikao vya Halmashauri Kuu ya TANU na Baraza la Mawaziri katika kijiji cha Matai sasa makao makuu ya wilaya ya Kalambo katika chuo cha makatekista- Santa Maria”alisema.

Chifu Sichula alisema, vikao hivyo vilijadili, kujifunza na kuhamasisha uanzishaji wa vijiji vya ujamaa.

“Mipango ya kuanzisha vijiji vya ujamaa na utekelezaji wake ni baada ya chama na serikali nzima kuja kujifunza Ufipa District (Sumbawanga) ambako tayari wakazi wake walikuwa wakiishi katika vijiji vya ujamaa kutoka enzi, kabla ya sera ya vijiji vya ujamaa" Chifu Sichula.

Alisema, baada ya vikao hivyo mwanaRukwa Profesa Athanas Kauzeni aliteuliwa na Serikali kuwa Kamishna wa Uanzishaji Vijiji Kitaifa na hadi leo katika baadhi ya mikoa vipo vijiji vinaitwa "kijiji cha Kauzeni".
Screenshot_20201115-190002.jpg
 
Yani historia yetu sisi waafrika ni ya kuokotezaokoteza sana. Yani yule aseme na huyu aongezee ndo tupate kitu.

Hatukuwa na utamaduni wa ku-keep record kabisa.

Mtoto wa shule ya msingi ukimuuliza mzungu wa kwanza kuona Mt. Kilimanjaro atakwambia Rebmann. Wa kwanza kuona Mt. Kenya atasema Ludwig Krapf. Wa kwanza kuchora ramani ya inland lake ( victoria ) mjerumani Jacob Erhadt ila mambo haya ya Nyerere hayafahamu.

Ingali kina Vasco Da Gama, Sir Francis Drake na B. Diaz wa 15th century AD ana taarifa nazo!
 
Hatuna utaratibu wa kuandika historia yetu, tunasubiri wazungu watuandikie, vitabu vingi vya historia yetu vimeandikwa na wazungu.
 
Rekodi nzuri lakini Mzindakaya naye ni bomu tu katika historia ya nchi hii; wakati mwingine ni vigumu kuamini anayosema.
Angeisema hiyo historia kabla ya kifo cha Nyerere tungeamini anatudanganya kwa kuwa Nyerere hayupo ili kuthibitisha.
 
Yani historia yetu sisi waafrika ni ya kuokotezaokoteza sana. Yani yule aseme na huyu aongezee ndo tupate kitu.

Hatukuwa na utamaduni wa ku-keep record kabisa.

Mtoto wa shule ya msingi ukimuuliza mzungu wa kwanza kuona Mt. Kilimanjaro atakwambia Rebmann. Wa kwanza kuona Mt. Kenya atasema Ludwig Krapf. Wa kwanza kuchora ramani ya inland lake ( victoria ) mjerumani Jacob Erhadt ila mambo haya ya Nyerere hayafahamu.

Ingali kina Vasco Da Gama, Sir Francis Drake na B. Diaz wa 15th century AD ana taarifa nazo!
Hadi kuna mzungu aliwahi kushangaa et mtu wakwanza kufika ziwa victori, Mt. Kilimanjaro😂😂

Kwamba wengine walikuwa hawauoni😂😂

Nilikaa nikajitafakari sana juu ya historia ya mwaafrika na bara zima.

Unaandikiwaje historia yako na mzungu. Utegemee matokeo gani?

Na ndio matokeo ya wasomi waliozalishwa kwenye jamii yetu-

Pengine ndio asili yetu waafrika. Najiuliza sana
 
Kuna kijiji cha Kauzeni katika Wilaya ya Kisarawe.... Hii hoja ya Chrisant Majiyatanga Mzindakaya huenda ina mashiko...
 
Back
Top Bottom