Historia Ya Extra Musica (Sehemu ya II)

Historia Ya Extra Musica (Sehemu ya II)

Kazi nzuri mkuu Roga Roga,naomba kama hutojali utuletee na history ya TP OK JAZZ na wanamuziki wake kwa ujumla pia kuna mtu anaitwa Mavon Marie Marie kama utafanikiwa kuipata history yake itakuwa poa sana.
 
Last edited by a moderator:
Kesho ntapitia mkuu nimeipenda sana ntajazia
 
Rubbish!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kwa hili hapana jifunze kuwa msitarabu mkuu .....mziki huleta watu pamoja wewe unafanya ugomvi.jamaa pia kaeleza vemasana wewe unaleta mbwembwe ka lijitu la ccm.

Jiheshimu sana elimu hata wadudu wanayo.tafakari sana.

HIstoria iloletwa ni extra musica....wewe mara wenge si utupie uzi wako?
 
HISTORIA YA EXTRA MUSICA SEHEMU YA II
Sehemu ya pili inahusu
(a) Kutoka Uimbaji wa kwaya/misibani hadi Extra musica na baadae kugawanyika
(b) Nini wanafanya baada ya mgawanyiko
(A) Kutoka Uimbaji wa kwaya/misibani hadi Extra musica na baadae
kuGawanyika

Mwishoni mwa miaka ya 1980 baadhi ya vijana ambao baadae walikuja kuwa waasisi wa Extra Musica walikutana kama waimbaji wa kwaya katika kanisa la St. Therese huko Quarter Ouenze Manzanza mjini Brazaville. Kabla ya kukutana kwao tayari baadhi yao walikuwa wakifahamiana tangu utoto wao mfano ni Durell Loemba na Giscar Ngolali aka Ramatoulaye ambao walikuwa darasa moja shuleni na walikaa pamoja darasani, pia Rogatien Ibambi Okombi aka Roga Roga and Esperance Mouanda aka Espe Bass nao katika shule nyingine walikuwa darasa moja. Tofauti na wenzao walianzia uimbaji wa kwaya katika makanisa mbalimbali, Quentin Moyascko alikuwa akiimba mitaani huko Talangai na Roga Roga alikuwa ni mwanachama wa kikundi cha utamaduni huko Roi Bongol Le Grand Mumboshi akiwa na wengine kama Papy Bombé(aliekuja kujulikana kama Papy Kakol) na Jules Kibens.

Mwaka 1992 Moyascko aliwaita wakina Oxygene, Roga Roga, Espe Base,Durell Loemba, Guy Guy Fall, Christian Ambe, Killa Mbongo na Ramatoulaye ili waunde kundi la pamoja ambalo lilijulikana kama Cogiex Musica ambalo lilikuwa likitumbuiza katika misiba na klabu za usiku kwa kutafsiri nyimbo za Wenge Musica, Zaiko, Empire Bakuba n.k Pia walikuwa wakiimba nyimbo ambazo zilitungwa na Quentin Moyascko. Ndani ya kundi Moyascko ndiye alikuwa mkubwa kuliko wenzake yeye alizaliwa 1969, Espe Bass 1973, wakati Roga Roga, Doudou, Herman Ngassacki, Guy Guy Fall, Ramatoulaye na Durell Loemba walizaliwa 1974, na Kila Mbongo alizaliwa 1975. Waliendelea na staili hii ya uimbaji hadi walipokutana na Ferreol Gassackys aliyekuja kuwa meneja wao, na kama meneja aliwashauri kuunda kundi ambalo lipo ki-proffessional zaidi. Jina Extra Musica lilibuniwa kwa pamoja kati ya Roga Roga na Espe Base mwaka 1993, katika misingi ya kuwa kundi lao ni Extraordinary na ndipo Extra Musica (Bon Pied Bon Look) ikazaliwa rasmi. Waliendelea kuandaa albamu yao ya kwanza ambayo ilitoka miaka miwili baadae yaani mwaka 1995.


Miaka miwili baadae yaani 1995 tangu kundi kuundwa, waliwasili wanamuziki wengine ambao hawakupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika albamu ya kwanza ya kundi hili la Extra Musica lakini walikuja kuwa muhimili bora wa kundi hili kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele. Kwanza aliwasili mpiga gitaa la rhythm Sylver Ndinga aka Sonor Digital (amezaliwa 1975) akitokea cogiex stars, Dominique Elenga aka Doudou Copa aliyeletwa na rafiki yake Guy Guy Fall, Hermann Ngassaki aliyeletwa na binamu yake ambaye alikuwa meneja wa kundi Ferreol Gassackys, Emery Mbonda na Gildas Pozzi walikuja wakitokea kundi hasimu la Cogiex Stars, na Christian Kingstall mpiga kinanda aliyeletwa na Roga Roga.

Albamu yao ya kwanza ya Les Nouveaux Missiles iliwafanya waonekane kuwa ni moto wa kuotea mbali kwani walifanikiwa kuuza nakala za santuri 50,000 miezi mine ya kwanza. Wimbo wa Freddynelson ulikuwa maarufu kiasi Raisi wa kundi na mtunzi wa wimbo huo Moyascko alibatizwa jina hilo huko Brazaville. Baada ya Albamu hii ambayo iliwashitua wakongwe wengi wa muziki wa kikongo, na kuanza kuwashutumu kuwa wanaiba kazi za watu hasa za Wenge. Hawakukata tamaa kutokana na shutuma hizi bali waliamua kujibu mapigo kwa kutoa albamu ya pili iitwayo Confirmation wakiwa na maana ya kuuthibitishia ulimwengu wa muziki wa kikongo kuwa ni wao na wala hawaibi kazi ya mtu kama inavyodaiwa.

Waimbaji Papy Jah and Papy Bastin walijiunga na Extra Musica baada ya Moyascko na wenzake kuondoka na kwenda kutengeneza kundi lao. Lakini Papy Jah and Papy Bastin hawakuweza kushiriki katika albamu ya Etat Major iliyorekodiwa Ufaransa baada ya wao kuachwa nyumbani Congo. Baada ya kurejea nyumbani, Papy Jah and Papy Bastin pamoja na rapa mpya Arafat (aliletwa kwa ajiri ya kusaidiana na Kila Mbongo) walijiunga na kundi katika ziara mbalimbali Afrika na pia kufanikiwa kushiriki kuimba katika albamu ya Shalai.

Kundi lilichaguliwa kama kundi bora la Afrika mwaka 2000 wakati wa utoaji wa tuzo za Kora huko Afrika kusini. Kundi lilirekodi albamu ya Trop C’est Trop na kampuni ya Cameroon iitwayo JPS bila Kila Mbongo aliyekuwa ameachana na kundi baada ya tatizo lake la koo kuzidi kuwa mbaya huku katika atalaku akibakia Arafat pekee. Baada ya Trop C’est Trop, miaka mitatu ilipita bila kutoa Albamu huku moja ya sababu ikiwa ni kufirisika kwa kampuni ya JPS ambayo walikuwa wameingia nayo mkataba wa kurekodi. Lakini baadae 2004 wakatoa Obligatoire ikijumuisha rapa kamaTyphoid Tarzan aliyekuja kuziba pengo la Kila Mbongo, waimbaji kama Fiston Boko kutoka Les Pipuyu ya Wenge BCBG, Rossen Superman, Levyson na Kerson Saddam wakitokea ZI International. Ni katika albamu hii jina la Extra Musica Zangul lilianza kutumika.

Baada ya Obligatoire ukazuka tena mgogoro mkubwa uliosababishwa na Roga Roga kutaka ku-dominate kundi na ndio mgogoro uliomfanya Doudou Copa kuachana na kundi hili kwenda kufanya mziki kama mwanamziki anayejitegemea na ni muda huohuo Roga Roga alim-recruit mwanaziki anyefanana na Doudou kwa kila kitu aitwaye Dido Senga. Mwaka uliofuata yaani 2005, Oxygene, Papy Bastain, Rossen Yaourt (Rossaine Kimance), Typhoide Tarzan, Baudoin Missapi na Kerson Saddam nao walijiondoa na kwenda kuanzisha kundi la Universal Zangul. Lakini Regis Touba alikuwa amerejea kundini baada ya shida aliyokutana nayo huko Wenge BCBG, awali Touba alipitia Extra Musica International baada ya kuondoka Extra Musica baadae ZI International kabla ya kuvuka mto Congo kwenda BCBG huko Kinshasa. Kumbuka Touba ndiye mtunzi wa wimbo Angela katika albamu ya Confirmation.

Kundi halikuweza tena kutoa albamu na JPS baada ya kampuni kufungwa rasmi na kuilazimu kundi kutafuta studio mpya na ndipo waliposaini mkataba na kampuni ya Sonima Music. Pia kuwasili kwa waimbaji kama Juventus aliyechukua mikoba ya Kerson, Rav 4 aliyeziba pengo la Papy Bastin na Kassoumbalessa aliyem-replace Rossen ndipo albamu ya La mainore ikatoka. Baada ya kutoka Albamu hii ya La mainore bendi ikaanza kufanya tour mbalimbali Afrika taratibu Roga Roga akaanza kuwaondoa wote aliowaona kama uwepo wao katika bendi wangemtisha katika ufalme wake, lengo kuu ikiaminika ni kutaka kuwa Untouchable president. Herman Ngassaki akaachwa nje ya ziara hizo kwa kisingizio kuwa alihitaji ku-promote nyimbo zake alizokuwa akizi-perform na Extra Musica Zangul katika night clubs mbalimbali, huku Regis Touba naye sababu ikiwa hiyohiyo. Arafat naye akawa replced na Zaparo de Guerre aliyetokea Z1 International. Pia akamleta rapa mwingine Etats Unis d'amerique kutokea Extra Musica International.

Ni Ramatoulaye na Espe Base waliokubali ubabe na ufalme wa Roga Roga pamoja na Sonor Digital ambaye kwasasa ndiye chef d'orchestre wa bendi. Hadi kufikia hapo haikuwa tena Extra Musica Zangul moja bali ikageuzwa na kuwa Roga Roga & Extra Musica Zangul, pia akiwa na vijana ambao ni wadogo na hawana nguvu yoyote ya kuhoji mamlaka yake katika bendi. Pia katika hali ya kushangaza Roga Roga akaachana na upigaji wa gitaa la solo na kuwa mwimbaji kiongozi wa kundi. Pia akamuongeza atalaku namba tatu De brazza, na pia Obama Synthé aliye-mreplace Baudoin Missapi ambaye alienda na Oxygene huko Universal zangul. Baada ya mageuzi makubwa katika safu ya waimbaji ya bendi, ndoto za Roga Roga zikafanikiwa na hatimaye kutoa albamu yake iitwayo Sorcellerie Kindoki ambayo imefanikiwa sana huko Congo Brazaville, na kwa sasa ametoa baadhi ya nyimbo kuelekea Albamu ya pili iitwayo Contentieux ambapo nyimbo hizo aliziimba wakati wa kumbukumbu ya miaka 20 (1993-2013) ya Extra Musica iliyofanyika Desemba mwaka jana.

Pia katika kumbukumbu hiyo ya Extra Musica ya miaka 20, Roga Roga alikataa kupanda steji moja na wenzake hasa Moyascko ili kukumbushia enzi za Freddynelson,Chagrin Plus plus, Denide,Losambo n.k pia hakuwa tayari kurudi katika nafasi yake ya awali yaani mpiga gitaa la solo ambayo ndiyo iliyomtambulisha kwa washabiki wake na asilimia 99 ya washabiki wake walimpenda sabau ya gitaa la solo. Hivyo wenzake wakina Guy Guy Fall, Oxygene, Ngassacky, Abilisi, Espe Base, Christian Ambe, Doudou, Moyascko, Durell Loemba, Sonor Digital walipanda steji moja na kuimba nyimbo nyingi za zamani kwa pamoja na waliposhuka Roga Roga na vijana wake nao wakapanda. Alichokutana nacho ni zomeazome na baadae washabiki walimrushia vyupa vya bia na chochote kilichokuwa mikononi mwao wakati akiwa stejini ili kuonyesha hasira juu tabia yake ya kujiona bora kuliko wenzake na ikizingatiwa aliingia stejini muda umeenda sana, kiufupi alijidhalilisha sana. Pia hata hao wakina Oxygene na wenzake walivyopanda jukwaani bado kuna hali fulani ilionekana kama ya kupigana vijembe wao kwa wao, hivyo tamasha halikufana sana kama lilivyotarajiwa.

View attachment 166787

(B) Nini wanafanya baada ya mgawanyiko
Ifuatayo ni historia ya wanamuziki waliokuwepo Extra Musica na walipo kwa sasa na nini wanafanya kwa sasa.

GUY-GUY FALL & EXTRA MUSICA;
Amezaliwa mwaka 1974. Ni mmoja ya waasisi wa Extra Musica na pia ndiye alikuwa mwimbaji mkuu/kiongozi wakati albamu ya Les Nouveaux Missiles inatoka. Alikuwemo wakati Albamu ya Kwanza na ya pili zikitoka, na aliondoka Extra Musica kutokana na mgogoro wa kimaslahi uliozuka katika kundi hilo baada ya kutoka kwa albamu ya Confirmation na kwenda kufanya kazi kama mwanamziki anayejitegemea yaani SOLO ARTIST na mpaka sasanafanya muziki kivyake. Baada ya kujitoa Extra Musica amefanikiwa kutoa Albamu kama Cote Quest na Ndoki Zoba zenye nyimbo zifuatazo.

Cote Quest (ilitoka tarehe 01 Oktoba 1999).
1.Double Impact 2.Effets Speciaux 3.Fant Sylla 4.Kiripo kiri 5.Mokili Oyo 6.Cote Quest 7.La Parade De Fifi 8.Mr L’Ambassadeur 9.M’Bamda

Ndoki Zoba
1.Perle Rare 2.Ndoki Zoba 3.Sorel Wambongo PP 4.Martine Kante La Guineenne 5.Ndoki Zoba II 6.Mobembo Merlyoles PP 7.Didi Kimuani 8.Le Parolier 9.Patience Ibara Love 10.Le Roi De Mapinga 11.Papa na Bawa Version



DOUDOU COPA;
Jina lake kamili anaaitwa Bienvenu Dominique Laka Elenga. Amezaliwa mwaka 1975 huko Owando. Alianza kuimba akiwa kijana mdogo katika seminari ya kikatoliki iitwayo Owando na baadae kwaya ya kanisa katoliki la Sainte Marie de Ounze huko Brazaville. Aliletwa Extra Musica na rafiki yake Guy Guy Fall na alikuwepo Extra Musica kuanzia Albamu ya Confirmation. Alipendwa sana kwa staili ya uimbaji wake mfano nyimbo kama Probleme sur probleme (Trop c'est trop), Horizon 2000(Shalai) na pia kwa utunzi bora wa nyimbo kama Ecart (Etat Majol Album), Zongi Sanga (Trop c'est trop) na L’Oublier (Obligatoire Album). Aliondoka Extra Musica mwaka 2004 baada ya kuchoshwa na tabia ya Roga Roga yakutaka ku-dominate kundi na kwenda kufanya kazi kama mwanamuziki anayejitegemea.

Mpaka sasa amefanikiwa kutoa jumla ya Album nne kama Solo Artist ambazo ni Echafaudage (2005), Independence Day (2007), Evolution (2010) na Menu (2013). Nyimbo zilizopo katika albamu hizi ni

Echafaudage (Sonima) 2005
1. Echafaudage 2.L’or noir 3. Universal 4. Labala 5.Mayi 6.Manfoulou 7.Bandeko 8.Etoile de femme 9.Ndongo 10. Yawe 11. Makoko

INDEPENDANCE DAY (SONIMA) 2007
1.Independence day 2.Vincent Gomez 3. Zara na botomo 4.Cathy 5. Serge Makouala 6.Bolingo 7. Anais Baryth 8.Akindou 9.Plaisir d’Owa 10. Fille a papa 11. Photo roman

EVOLUTION (SONIMA) 2010
1.Eyala 2.Palado 3.Emery Alcatel 4.Evolution 5.Gaiton Kodja 6. Akindou II 7.Michelle
8. Nazo Kamwa Te 9.Eyindi 10.Bon Mariage

MENU(Letiok Productions), 2013
1.Mossaka 2.Bouillon 3.Ofoula 4.Pondu Ya Limbondo 5.Liboke 6.Ntoba Mbori 7.Tiep Bou Diem 8.Madesu 9.Ngoulou Mou Manko 10.matembele 11.3 Pieces



OXYGENE “LE GENERAL SOTONYOTO” & UNIVESAL ZANGUL.
Jina lake ni Sylvain Mbon, Extra Musica alijulikana sana kama Oxygene na kwasasa ni maarufu kama Le General Sotonyoto akiwa ni kiongozi wa Kundi la Universal Zangul aliloliunda mwaka 2005 baada ya kujitoa Extra Musica sababu ikiwa ni ileile ya kuchoshwa na vijitabia vya kijinga vya Roga Roga. Ni mmoja wa wanamuziki wa kwanza wa kundi hili. Aliondoka Extra Musica na wanamuziki ambao wengi wao walihisi kuwa hawapewi nafasi ya kutosha katika kundi, Wanamuziki hao ni Papy Bastain, Rossen Yaourt (Rossaine Kimance), Typhoide Tarzan, Baudoin Missapi na Kerson Saddam. Kwa pamoja walifanikiwa kutoa Album iitwayo Tapis Rouge (Red Carpet in English). Katika Albamu hii upande wa Vocal walikuwepo Oxygene kama Raisi wa kundi, Papy Bastain, Rossen Yaourt, Kerson Saddam, Apotre Noumaz, Thierry Berger na Yellow Man; Marapa wakiwa ni Typhoide Tarzan na Bulldog; Solo gita likichalazwa na Bondo Mania; B-Magic akisimama katika Rhythm gita, Davy Mbazo katika Gita la Base, Edjo Mapendo katika Mi-solo gita; Drums zikipigwa na Okouere Miracle huku Baudouin Missipi akiwa kama Synthesizer na Kiki Lombonda akisimama katika Congas. Mjumuiko huu ulifanikiwa kutoa Album ambayo ilionekana kuwa bora kwani haikuwa na kelele kama albamu ya Extra Musica Zangul ya La mainore. Wakiwa huko Universal Zangul, Bastin alitunga nyimbo mbili ambazo ni Tout à Coup na La vie Onongo, lakini wimbo C'est Dejà Fait
Akiwa Extra Musica,Oxygene alipendwa zaidi kutokana na staili yake ya uimbaji mfano nyimbo kama Na Ko Bala Yo Na Ko (Les Nouveaux Missiles ) na utunzi wake bora wa nyimbo kama Ziya (Confirmation), Generation Mechante (Ouragan), Cri Du Coeur (Etat Majol) na Rufin Bouka (Obligatoire). Huyu ndiye Oxygene ambaye kutokuwepo kwake Extra Musica kunaifanya bendi ionakane kama kunakitu kinapungua, na ndivyo hivyo hivyo binadamu unapokosa hewa ya Oxygen. Nje ya muziki Oxygene ni Askali polisi na amekuwa askali tangu akiwa Extra Musica Zangul. Albamu hii ilikuwa na nyimbo zifuatazo
TAPIS ROUGE (Kiki Toure) 2006
1.Tapis Rouge 2.Pepero 3.Yaourt Love 4.C’est Fait Deja 5.Tout a Coup 6.Pourquoi Papa Tape Maman 7.La Vie Onongo 8.Mso 2 9.Sans Hypocrisie 10.Ibrahim Sylla





Quentin Moyascko & Extra Musica International.
Amezaliwa mwaka 1969. Quentin Moyasco ni mmoja wa wanamuziki wa kwanza na waliowezesha na kusababisha mafanikio makubwa ya kundi hili la Extra Musica kabla ya kuachana nalo baada ya Albamu ya tatu ya Kundi la Extra Musica iiltwayo Ouragun nakwenda kuanzisha kundi linguine liitwalo Extra Musica International kutokana na mgogoro mkubwa uliozuka katika kundi hili sababu ikiaminika kuwa ni kugombania madaraka kati yake Raisi wa kundi Moyascko na chef d'orchestre wa wakati huo wa kundi Roga Roga, Simon Music akatumia mgogoro huu kuligawa kundi na Extra Musica International kuzaliwa (Kwa wasiofahamu, Simon Music ndiye aliyeligawa pia kundi la Wenge baada ya kutumia mgogoro uliokuwepo katika bendi kutokana na kutoelewana kati ya JB Mpiana na Werrason baada ya Mpiana kutoa albamu kama solo artist ya Feux de L'amour). Wakati Moyascko akiondoka Extra Musica aliondoka na wanamuziki wengine wengi na kwenda kunda kundi la Extra Musica International. Wanamuziki hao ni Pinochet Thierry, Regis Touba, Cyrille Malonga, Durell Loemba na Arnaud Laguna, ambao waliungana na Christian Ambe aliyekuwa amekwisha jitoa Extra Musica baada ya Albamu ya Confirmation. Wakiwa pamoja walifanikiwa kutoa albamu moja iitwayo Super Helico lakini miaka miwili baadae Simon Music akafanikiwa tena kuutumia mgogoro uliopo Extra Musica International na kundi kugawanyika, kundi la ZI International likaundwa chini ya uongozi wa Christian Ambe, Durell Loemba, Pinochet Thierry, Regis Touba na Cyrille Malonga, huku Extra Musica International ikibakiwa na Quentin Moyascko na Arnaud Laguna. Baada ya mgawanyiko huu, Extra Musica International chini ya Moyascko ilifanikiwa kutoa albamu zingine mbili ambazo ni Merci na Virgule. Zifuatazo ni nyimbo katika albamu hizo

SUPER HELICO (Simon Music), 1999
1. Marc 2.Ange Panisse 3. Amie Tendresse 4. Biwela-wela 5. Rafrain pour l’humanite 6.Envoye Special 7. Mon Reve 8. Pres de moi 9. Rafrain for humanity
MERCI (Qemi 01), 2001
1.007/USA 2.Mechancete 3.Ya we 4.Baby doll 5.To Libissana 6. Nojindji 7. T.G.A
8. Mon souhait 9.Princes Angie
VIRGULE (WedooMusic/QEMI), 2007
1.Virgule 2.Ingratitude 3.Ma Rho 4.Ngongo 5.Vinoge 6. Congo-Mali 7.Rety 8.Ya Lelo
9.Heritage 10.Makaramba 11. Freddy Nelson (Bonus in DVD)


PAPY BASTIN
Ngoma Samba aka Papy Bastin au Maboulango au Jet Li amezaliwa 17 Machi 1975 mji wa Makabana huko Congo Brazzaville. Alihamia Brazaville pamoja na wazazi wake akiwa na umri wa miaka 14, na pia alipenda sana kuimba na kutafsiri nyimbo za King Kester Emeneya, Papa Wemba, Pepe Kallé akiwa shule. Miaka miwili baadae mapenzi yake kwenye muziki yaliongeza na kuanza kuimba katika vikundi mbalimbali mtaani.
Baada ya kumaliza shule, akiwa na umri wa miaka 19 wazazi wake walimruhusu kutoa wimbo wake uitwao “Etudient” ukieleza umuhimu wa shule kwa binadamu. Alianza chuo kikuu huku akiwa amejiunga na kikundi cha uimbaji cha mitaani kiitwacho Gloria Ecerta ambapo katika kikundi walikuwa wakiiga staili za uimbaji za Victoria Eleison huku yeye role model wake akiwa King Kester. Mwaka huohuo aliachana na kundi hili la Gloria na kujiunga na Folk Stars ambako alikutana na Jules Kibens na Zulema, katka kipindi cha miezi 8 alichokua bendi hii aliimalika sana katika uandishi wa nyimbo na kuachana na tabia ya kunua kazi za watuambazo zimekwisha andikwa. Baada ya miezi nane aliachana na kundi la Folk Stars na kujaribu bahati yake kwa kuanzisha kundi lake mwenyewe lakini vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka vilifanya kusiwepo tena na mazoezi nayeye kuamua kuondoka Brazaville na kwenda Pointe Noire (mji kubwa baada ya Brazaville) ambapo usumbufu haukuwa mkubwa, akiwa hapo aliunda kundi lake upya akiwa na wanamuziki wapya na kuanza kuandaa albamu yake kabla hajakutana na Espe Base siku moja akiwa katika matamasha mbalimbali aliyokuwa akiimba usiku.
Alikubaliwa na kujiunga rasmi na Extra Musica baada ya kujaribiwa mwaka 1999, alikuwa akiimba, akitembea na hata nywele akikata kwa staili ya King Kester lakini akashauliwa na Roga Roga kuwa inabidi naye awe na Identity yake badala ya kukopi ya King Kester na pia alikabidhiwa CD zote za Wenge Musica na Kutakiwa kumsikiliza na kumuiga JB Mpiana, lengo likiwa ni kumix staili ya JB Mpiana na King Kester ambayo yeye angeimba.
Baada ya kukubali na kulifanyia kazi wazo la Roga Roga ndipo akapewa nafasi ya kushiriki na kuimba katika albamu ya Shalai. Pia ilimbidi kutoa nyimbo zake alizoandika kwa Roga Roga na Espe Bass ilizionakane zimeandikwa na wao wakati si kweli mfano ni wimbo Laissez Passer katika albamu ya shalai, Gambala aliompa Ramatoulaye (Albmu ya Trop C’est Trop), na Foundation Muller (Obligatoire) aliyompa tena Ramatoulaye. Taratibu naye akawa moja ya watu muhimu katika bendi badala ya kuwa akitunga nyimbo na kuwapa viongozi wa kundi au waimbaji wa muda mrefu kama Doudou na Ngassaki na hivyo nyimbo zake kuanza kutoka kwa jina lake tofauti na awali.
Baada ya Obligatoire, hali tete ndani ya bendi iliyosababishwa na Roga Roga kwa kuwa mbinafsi na hulka yake yakutaka madaraka zaidi na pia kuondoka kwa Doudou kuliwafanye yeye na wenzake wengi pamoja Oxygene kujitoa na kuunda kundi lao la Universal Zangul mnamo tarehe 16 desemba 2005 saa 4.16 PM. Wakiwa huko Universal Zangul, Bastin alitunga nyimbo mbili ambazo ni Tout à Coup na La vie Onongo, lakini wimbo C'est Dejà Fait walimshambulia Roga Roga idirect kwa kuimba "ilikuwa tarehe 16 ya Desemba saa 4:16 PM, tuliokoka utumwani na yule mtawala anayejiita mfalme".
Albamu yao ilifanikiwa kiasi Congo Brazaville na baadhi ya nchi za kiafrikana pia walikuwa washindani imara wa Roga Roga na Extra Musica yake. Pia mafanikio ya Albamu hii ilifungua milango ya udhamini kutoka kwa makampuni mbalimbali na moja ya kampuni iliyojitokeza ni kampuni inayotengeneza bia ya Primus lakini walishindwa kusaini mkataba na kampuni hii baada ya Roga Roga ambaye naye alikuwa tayari ameshasaini mkataba na kampuni hii kutishia kuvunja mkataba endapo Universal Zangul wangefunga mkataba na Primus, pamoja na yote huwa wanashirikiana japo kwa kiasi kidogo na Roga Roga katika baadhi ya concert zinazoandaliwa na Primus.
Wakiwa katika maandalizi ya albamu ya pili (Conjugaison) ya kundi la Universal Zangul, kiongozi wa kundi Oxygene ambaye nje ya muziki pia ni Afisa wa Polisi tangu akiwa Extra Musica alikwenda Cameroon kwa ajiri ya mafunzo ya miaka miwili na hivyo kusitisha zoezi zima la kutoa albamu hiyo ya pili ya kundi na kukubaliana kuendelea na mpango huo wa kutoa Albamu hiyo pindi Oxygene atakaporejea kutoka mafunzoni, kuona hivyo Bastin akaamua kujitoa katika kundi mwaka 2007 kwa ajiri ya kufanya solo na mwaka mmoja baadae yaani 2008 akafanikiwa kutoa albamu iitwayo “Bravo” ambayoilikubalika zaidi kwa mashabiki wake na kumfanya kuzuru nchi kadhaa za kiafrika akiwa na bendi yake mwenyewe. Kitambo kilipita akiwa kimya na baada ya miaka 6, mwaka 2014 amefanikiwa kutoa albamu ya pili iitwayo “Notez Bien” aliyowashirikisha wakali kama Ferré chair de poule, Didier Lacoste, Eboa Lotin, rafiki yake Doudou Copa na Mbuta Likasu.


ROGA ROGA & EXTRA MUSICA ZANGUL
Jina lake kamili ni Ibambi Okambi Rogatien amezaliwa mwaka 1974. Ndiye Raisi na kiongozi wa Extra Musica Zangul. Mbali ya kuwa mpigaji gitaa la solo bora kuwahi kutokea Congo Brazaville, Roga Roga pia ni mwimbaji na mtunzi bora wa nyimbo huko congo mfano wa nyimbo alizotunga ni Dieu L'eternel (katika albamu ya Les Nouveaux Missiles ), Losambo, Hommage, na mélange (Ouragun Album au Hurricane in English), Racine, La Plule na Etat Major (Etat Major album) na zingine nyingi sana.
Alikuwepo Extra Musica tangu kuanza kwake wakati huo wakiimba nyimbo mitaani na misibani kama Cogiex stars na ndiye muasisi wa jina la Extra Musica. Awali kabla ya Cogiex Stars alikuwa ni moja ya wanamuziki waliounda kikundi cha utamaduni huko Roi Bongol Le Grand Mumboshi. Ingawa ni moja ya watu waliofanikisha Extra Musica kuwa hapa ilipo lakini upande mwingine ndie moja ya sababu kubwa wanamuziki wa kundi hili kukimbia. Hii imeelezwa na wanamuziki wengi waliopitia bendi hii na hasa tabia yake ya kujikweza na kujiona kuwa bila yeye wengine si lolote katika muziki, pia ni mbinafsi.
Wakati mwingine unaweza kujiuliza ilikuwaje Roga Roga awe mjanja kuliko wenzake kiasi kwamba wote wamkimbie na kumuacha afanye atakavyo wakati kama ni kundi walilianzisha kwa pamoja? Jibu ni dogo sana, Roga Roga ni mtu mwenye akili sana hasa katika kucheza na akili za watu, pia akili yake kubwa katika utungaji wa muziki, kupangilia sauti wenzake waimbeje hata kama wimbo hakuutunga yeye na ujuzi alionao katika kupiga gitaa na kuimba ndio siri ya mafanikio yake. Maana wengi wao waliopita pale walionekana Lulu sana wakiwa pale lakini wengi wao wameshindwa kabisa kuonesha ubora wao waliokuwa nao baada ya kutoka pale (mfano Abilissi, Papy Jah, Tarzan, Arafat, Gildaz Pozi, Emery Mbonda, Herman Ngassacki n.k), huku wengine waamue kurudi na kumpigia goti (mfano Regis Touba) baada ya mambo kuwa magumu huko walikokwenda na baadhi kung’ang’ania kuwa naye wakati ye anafanya anavyotaka na bendi kashaifanya kama yake (Mfano Sonor, Ramatoulaye na Espe Base). Pia uwezo wake waku-recruit vijana wapya au waliopo kwaajiri ya kuziba mapengo yawalio ondoka, mfano Dido aliyeziba pengo la Doudou, Abilisi aliyeziba pengo la Christian Ambe na Herman Ngassaki aliyeziba vizuri pengo la Guy Guy Fall kiasi unaweza kujikuta ukisema hakukuwa na haja ya kuwa na Guy Guy Fall wakati Herman ndio kila kitu. Ukiachana na tabia zake zisizo na tija, mimi mwenyewe namkubali sana huyu jamaa kuliko mwanamuziki yeyote aliyepitia Extra Musica kwasababu ya kipaji alichonacho.


PAPY JAH
Alikuja Extra musica baada ya kuondoka wakina Moyascko na wenzake na iimbidi asubiri mpaka albamu ya shalai ndio apewe nafasi ya kuimba, pia albamu ya Trop C’est Trop alionesha vitu vyake baadae aliondoka kwenda Quartier Latin(QL)ambako huko hakuwa na maelewano mazuri na Soleil Fally na waimbaji wengine wakundi la QL, akaamua kuachana na QT na kuwa solo kabla ya baadae kutimkia Ulaya alipo hadi leo.

HERMAN NGASSAKI
Amezaliwa mwaka 1974. Anafahamika pia kama Do-mfumu kisumu au manu manu. Aliletwa Extra Musica na binamu yake ambaye alikuwa meneja wa kundi Ferreol Gassackys. Ni Muimbaji mwenye kipaji kikubwa na uwepo wake Extra Musica ulifanya pengo la Guy Guy Fall kuzibwa kwa haraka kuliko ilivyotarajiwa.
Alikuwepo Extra Musica tangu albamu ya kwanza japo hakupata nafasi ya kuonesha kipaji chake hadi ilipofika Albamu ya pili ndipo Herman Ngassacki alianza kuonesha mavituzi yake. Alijipatia umaarufu sana hasa kwa kunengua (kukata mauno) mfano mzuri mtazame katika video ya wimbo kama Losambo au Etat Major zinapokuwa zinamalizika anakuja na kupandisha shati na kuanza kunengua. Sababu ya kuondoka Extra Musica ni vituko vya Roga Roga kiasi wakati Extra Musica wakizunguka nchi mbalimbali Afrika kunadi albamu yao ya 8 iitwayo La Mainoire aliachwa kwa kisingizio kuwa anaandaa promotion ya nyimbo zake. Kwasasa anafanya muziki kama mwanamuziki anayejitegeme huku akiwa amesha toa nyimbo kadhaa katika mfumo wa audio na video, mfano Generique. Huyu alikuwa rafiki mkubwa wa Roga Roga lakini alitoswa narafiki yake huyo.


CHRISTIAN AMBE & ZI INTERNATIONAL
Pia anafahamika kama Papa Lutumba. Alikuwepo tangu Extra Musica inaanza lakini aliondoka baada ya Confirmation Albamu kutoka japo hakupewa nafasi kubwa ya kuimba katika Albamu hii huku sababu ikielezwa kutoelewana kati yake na chef d'orchestre wa bendi wa wakati huo Roga Roga. Aliungana na Moyascko na wenzake walioondoka baada ya albamu ya Ouragun na kuunda kundi moja liitwalo Extra Musica International. Wakiwa pale walitoa albamu moja iitwayo Super Helico, baadae ulitokea msuguano uliosababisha yeye na wenzake kama Durell Loemba, Regis Touba na Pinochet Thierry kuondoka na kuunda kundi la ZI International ambapo yeye ndiye kiongozi wa kundi hili mpaka sasa. Wamefanikiwa kutoa Albamu Ere d’e Verte ambayo sehemu kubwa wanamshutumu Moyascko kwa kutokuwa mkweli. Kiukweli huyu jamaa nilimpenda sana hasa staili yake ya uimbaji mfano msikilize kwenye Chagrin Plus plus, Angela, Amie Reviens na Dieu L'eternel jinsi anavyolialia wakati wakuimba, utampenda tu. Pengo lake Extra Musica lilizibwa vizuri na Abilissi baada ya yeye kuondoka.



DURELL LOEMBA
Amezaliwa 1974. Unapozungumzia mafanikio ya mwanzo ya Extra Musica huwezi kuacha kumtaja huyu jamaa hasa upande wa utunzi wa nyimbo bora na nzuri kama Amie Reviens, Lolango na M'ere S. Pia unapofikiria ubora wa albamu ya Confirmation hasa kataka mpangilio wa vyombo huyu ni mmoja wapo wa wapiga gitaa hasa la Rhythm Albamu. Ni mmoja ya waanzilishi wa Extra Musica tangu enzi zile za Cogiex Stars na ni mmoja ya waasisi wa Extra Musica International na ZI International. Kwasasa yupo ZI International huku yeye ndiye aliyechukua jukumu la kupiga gitaa la solo katika bendi hiyo. Wakati mwingine huwa anakodishwa Extra Musica International kwenda kufanya nao kazi.


WENGINEO
Ukiacha Killa Mbongo ambaye aliachana na muziki baada ya koo lake kuleta hitilafu, wengineo hawajulikani leo hii wako wapi japo katika tamasha la kuazimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Extra Musica walikuwepo, mfano ni Abilisi, Pinochet Thiery, Anaurd Laguna, Arafat, Christian Kingstall, Emery Mbonda, Regis Touba, Gildaz Pozi n.k. Tatizo alilokutana nalo Kila Mbongo ni sawa na alilokutana nalo rapa wa Wenge Musica wa wakati huo Roberto Wunda. Kumekuwa na maneno yakisemwa kuwa Kila Mbongo anajiandaa kurudi stejini lakini bado haijathibitishwa kutoka kwa swaiba wake Roga Roga. Nitakapopata habari zao mara moja nitawajulisha kupitia hapa jukwaani. Lakini Espe Base, Ramatoulaye na Sonor bado wapo na mfalme Roga Roga katika bendi ya Extra Musica Zangul.

AWAMU IJAYO NITAKUJA NA STORI KUHUSU KIZAZI CHA WENGE MUSICA WALIPOTOKEA NA WALIPO KWA SASA NA WANACHOFANYA.

Shukrani za pekee ziende kwa Musiques-afrique.com, Arches aliyeko Kinshasa na Guy guy fall waliofanikisha stori hii ya kizazi cha Extra Musica.
Mawasiliano zaidi napatikana kupitia
Bislisk@yahoo.com


UNAWEZA KUDOWNLOAD FAILI HILI HAPA CHINI UPATE PIA PICHA ZAO
View attachment 166855

Hivi Titina, Aimelia, Alain Mpela na Burkina Fasso wako wapi? Titina utampenda wimbo wa Tour Eiffel, Aimelia wimbo wa Liberation, Alain Mpela wimbo wa Serge Palmi japo ulitungwa na mpiga drum Burkinafaso.

Kiukweli Jules Kibens ni.mtaalam. Wimbo wa Papito Mbala versionII, Love Airline, Mohamed Kaniasi utamjua kweli jamaa anajua.

Mdau nakuomba unipe majin ya wale waimbaji wa kwanza kwenye wimbo uitwao Le spoir de Chicago. Kuna jamaa kavaa kama Arafat na mwingine bonge hivi sijui ni nani. Wimbo ulitungwa na Fi Carre ukaimbwa na JB Mpian,hao wawili nisiowafaham, Fi Carre(mtunz mwenye sauti nzito) mwishoe kamaliza Chai Ngenge. Album ni Internet.
 
Kwa hili hapana jifunze kuwa msitarabu mkuu .....mziki huleta watu pamoja wewe unafanya ugomvi.jamaa pia kaeleza vemasana wewe unaleta mbwembwe ka lijitu la ccm.

Jiheshimu sana elimu hata wadudu wanayo.tafakari sana.

HIstoria iloletwa ni extra musica....wewe mara wenge si utupie uzi wako?

Pentium Zero! POPOMA.
 
Jules Kibens au MOLONGESHI Hajawahi na Hatowahi Kuwa Ni Zao La Extra Musica bali Huyo Jamaa Aliletwa Hapo Kwa Wanangu Wenge BCBG na Mshikaji Wake Mkubwa Maitre Ficarre Mwamba ( Mpiga Solo Namba Moja na Veteran Wa Wenge Musica BCBG ) Na Huyo Jamaa ( Jules Kibens ) Kitaaluma Ni Mhadhiri Wa Lugha Ya Kifaransa ktk Chuo Kikuu hapo Kinshasa Na Anapoimba Vipande Vyake Utamsikia Mwenye Bendi Kipenzi Changu Jean Bedele Tshituka Mpiana ( JB ) Anamtaja Kwa Kumuita Le Professer Ambapo Kwa Lugha Ya Kifaransa Inamaanisha Ni Mhadhiri AU Mwalimu Wa Hali Ya Juu Na Kwa Huyo Mpiga Gitaa Ficarre Mwamba Huwa Anamuita Maitre Ambapo Kwa Lugha Kwa Lugha Ya Kifaransa Anamaanisha Mwalimu. Kwa Sasa Jules Kibensi Ndiyo MKURUGENZI na KIONGOZI Wa Wasanii Wote ktk Kundi Zima La Wenge BCBG Na Ndiyo Anarekebisha Nyimbo Zote Za Bendi Kuanzia Matamshi Hadi Maneno Na Anapangilia Mpangilio Wote Wa Uimbaji Na JB Mpiana ANAMPENDA na ANAMHESHIMU Sana Na Mno Jules Kibens Na Ameweza Kabisa Kuziba Pengo La Injinia na Mhandisi Wa Ndege Blaise Bula Huku Akishirikiana Kabisa Na Waimbaji Wenzake Wa Kikosi Cha Kwanza Pale Stejini Ambao Ni JDL ( Jean Didier Loko ), Rio Biku Dejeneiro, Na Chai Ngenge ( Bluetooth ) Wakisaidiwa Na Waimbaji Hawa Wa Akiba Bogues Bompema, Abraham Mignon, Nono Fuchi, Erick Mente na Zulie Zulema. Nyuma Ya Watu Hawa Hapawezi Kufanikiwa Bila Kuwategeme Hawa : Mpiga Drums Maarufu au Mkaanga Chips na NAIBU MKURUGENZI Wa Bendi Seguin Migno ( Maniata ) Ambaye Mapigo Yote Ya Nyimbo Za Wenge BCBG Hutengeneza Yeye Na Huyu Akikuchukia Basi JB Mpiana Hana Mjadala Zaidi tu Ya Kukufukuza Bendini Na Mwisho Wa Yote Ni Vijana Hawa Wawili Ambao Hawana Mfano Na Ndiyo Mabingwa Wa Kughani au Kurepu Kwa Kifaransa Tunawaita Animateurs Kwa Kilingala Huitwa ATALAKUS ambao Ndiyo Wanaonogesha Nyimbo Zote Na Kuchangamsha Kuimbi Ambapo Repa Kiongozi Anaitwa ANTIBIOTIQUE Lisimo na Msaidizi Wake Anaitwa CELLULAIRE Jeune Ambao Kiukweli Wameweza Kabisa Kuziba Pengo La Bingwa Wa Kurepu Tutu Calugi Le Kalunjiste ( Yombo Lumbu ). Semeni Bendi Ila Wenge Musica BCBG Mniachie Mimi Mwenyewe Kwani Naijua Na Naifuatilia Kinagaubaga Na Naipenda Hilo Kundi Kama Sina Akili Nzuri. Hakuna Kama Jules Kibens na Hakuna Bendi Kama Wenge Musica Na Kwa Wale Wapenzi Wa Miziki Ya " Live " Nawashaurini Tafuteni DVD Za Wenge BCBG Hamtojutia Kutoa Pesa Zunu Kununua . DRC Nzima Hili Kundi Linafananishwa Na Timu Ya Taifa Kutokana na Kusheheni MAFUNDI Watupu.

Asante mkuu... Umetoa dawa
 
Asante mkuu... Umetoa dawa

Karibu. Na Kwa Sasa Bendi Imemeguka Tena Baada Ya Kuondokewa Na Wanamuziki Wake Wawili Na Wapiga Vyombo Muhimu Ambao Ni Chai Ngenge a.k.a Bluetooth Na Djino a.k.a Equalizeir baada Ya Wawili Hao Kugombana Na Msaidizi Mkuu Wa Bendi Ambaye Ni Mpiga Drums Maarufu Seguin Mignon a.k.a Manyiata Huku Wapiga Gitaa Maarufu Patrick Molesso a.k.a Le Tabe Pasimanii Na Patou Solo a.k.a Schevchenko Nao Wakiondoka Na Sasa ktk Gitaa Hilo Kiongozi Amebaki Veteran Ficarre Mwamba a.k.a Maitre. Poa!
 
Uzi umeharibiwa sana na mpuuzi mmoja humu kjitia ukichaa wa wenge wakati hajui kitu
 
duh!,aisee jf noma..yaani mimi nilivyo pagawa vibaya na mziki wa kikongo hasa rhumba,nikisoma habari kama hizi roho yangu inasuuzika sana.jioni hii baada ya kutoka job,nimepitia hapa kwenye ki-pub jirani na home nakula "mambo yangu" huku nikisindikizwa na rhumba "orgasy" ya fally ipupa na "100 kilos" ya ferre gola.yaani najihisi kama nipo dunia nyingine.

wakuu Roga Roga na GENTAMYCINE naomba sana siku mkitulia mshushe historia ya mwanamziki wangu kipenzi Ferre Gola.sipitishi siku bila kumsililiza ferre.mmetisha wakuu.OVER!
 
Last edited by a moderator:
duh!,aisee jf noma..yaani mimi nilivyo pagawa vibaya na mziki wa kikongo hasa rhumba,nikisoma habari kama hizi roho yangu inasuuzika sana.jioni hii baada ya kutoka job,nimepitia hapa kwenye ki-pub jirani na home nakula "mambo yangu" huku nikisindikizwa na rhumba "orgasy" ya fally ipupa na "100 kilos" ya ferre gola.yaani najihisi kama nipo dunia nyingine.

wakuu Roga Roga na GENTAMYCINE naomba sana siku mkitulia mshushe historia ya mwanamziki wangu kipenzi Ferre Gola.sipitishi siku bila kumsililiza ferre.mmetisha wakuu.OVER!

Hamna Noma Mkuu ILA Tafuta DVD Ya Ferre Gola Aliyopiga ktk Ukumbi Wa Zenith Na Utasuuzika Zaidi Kwani Ana Mpiga Solo Mahiri, Drummer Na Vijana Wawili Wa ATALAKU ( Kughani au Kurapu ). Jamaa Walipiga Huko Acha Masihara!
 
Hamna Noma Mkuu ILA Tafuta DVD Ya Ferre Gola Aliyopiga ktk Ukumbi Wa Zenith Na Utasuuzika Zaidi Kwani Ana Mpiga Solo Mahiri, Drummer Na Vijana Wawili Wa ATALAKU ( Kughani au Kurapu ). Jamaa Walipiga Huko Acha Masihara!

aah mkuu ile dvd nilikuwa nayo na nilikuwa naitazama mara kwa mara nilipo kuwa napata nafasi.ile show ya zenith ya ferre ilikuwa ni habari nyingine.sidhani kama fally aliwahi kuteka mashabiki kama alivyo fanya ferre paris.
 
aah mkuu ile dvd nilikuwa nayo na nilikuwa naitazama mara kwa mara nilipo kuwa napata nafasi.ile show ya zenith ya ferre ilikuwa ni habari nyingine.sidhani kama fally aliwahi kuteka mashabiki kama alivyo fanya ferre paris.

Alijitahidi Sana Japo Hataweza Kufikia Rekodi Iliyowekwa Na Wenge Musica Bon Chic Bon Genre 1999 Ambapo Ukumbi Huo Ulifurika Ndani Na Nje Hadi Kupelekea Vifo Vya Watu 15 Kutokana Na Stampede! Kumbuka Kwamba Hawa Akina Fally Na Ferre Ni Kizazi Tu Cha Sasa Na Bado Wanajifunza Kutoka Kwa Wakubwa Zao Akina Jean Bedele Tshituka Mpiana, Koffi Charles Antoine Olomide Na Ngiama Makanda Werrason.
 
Alijitahidi Sana Japo Hataweza Kufikia Rekodi Iliyowekwa Na Wenge Musica Bon Chic Bon Genre 1999 Ambapo Ukumbi Huo Ulifurika Ndani Na Nje Hadi Kupelekea Vifo Vya Watu 15 Kutokana Na Stampede! Kumbuka Kwamba Hawa Akina Fally Na Ferre Ni Kizazi Tu Cha Sasa Na Bado Wanajifunza Kutoka Kwa Wakubwa Zao Akina Jean Bedele Tshituka Mpiana, Koffi Charles Antoine Olomide Na Ngiama Makanda Werrason.

nimekusoma mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom