Asante kwa kunifungua kichwa, naendelea kuhtaji msaada na kwa wengine kuhusiana na historia hiyo.Ndugu GIPAMA,
Naona mada yako ina ugumu. Hata hivyo nianze kwa kusema kuwa mimi si mtaalam wa mambo ya India lakini kidogo nilichonacho kitakusaidia. Wengine wataongezea na kuboresha na mwisho tutapata kitu kizima.
Mahatma Gandhi (jina lake halisi ni Mohandas Karamchand Gandhi) alizaliwa Gujarat, India mwaka 1869. Alifunga ndoa ya utotoni na binti aliyeitwa Kasturbai aliyekuwa na umri wa miaka 14 (yeye akiwa na miaka 13) kadiri ya mila za Kihindi. Hiyo ilikuwa mwaka 1883.
Baada ya kuhitimu masomo yake ya sheria London Uingereza, Gandhi alirejea India. Baadae, mwaka 1894, alipata kazi katika kampuni ya uwakili ya Kihindi iliyoitwa Dada Abdalla & Company huko Pretoria, Afrika ya Kusini. Ikumbubwe kuwa Afrika ya Kusini ilikuwa na idadi kubwa ya Wahindi waliokuwa wakifanya kazi katika mashamba ya walowezi wa kizungu.Baada ya kufanya kazi katika kampuni hii kwa takriban miaka 20, akirudi tena India mwaka 1914.
Huko India Gandhi alijiunga na harakati za kisiasa na kijamii. Kwake siasa ilikuwa ni kama "kucheza katika uwanja wa nyumbani" kwani hata baba na babu yake walikuwa wanasiasa waliofahamika vizuri. Mwaka 1920 Gandhi akiwa kiongozi wa chama cha Wahindi kilichoitwa Indian National Congress ambacho kilikuwa kikipigania uhuru wa India kutoka kwa Waingereza.
Gandhi "alijizolea" umaarufu ndani na nje ya India kwa falsafa yake ya "passive resistance"ambayo ilihusisha upinzani pasipo kutumia silaha (nonviolence) na ukaidi kama vile kukataa kulipa kodi kwa serikali ya kikoloni, kukataa kununua bidhaa za wakoloni n.k. Licha ya misukosuko aliyoipata, hakurudi nyuma. Hatimaye mwaka 1947 India ikapata uhuru.
Hata baada ya uhuru Gandhi aliendelea kupinga kugawanywa kwa India katika misingi ya kidini. Licha ya upinzani wake India ikagawanywa ambapo eneo la Waislamu wengi likawa nchi ya Pakistan na life lenye Wahindu wengi likabaki kuwa India tunayoijua leo.
Baadhi ya watu walimwona ni mtu mwenye msimamo ya ajabu au isiyofaa. Hii ikasababisha kuuawa kwake mwaka 1948 ambapo alipigwa risasi tatu.
Karibuni kwa nyongeza.
Hv mkuu napenda kujua pia kuwa wale raia wa pakistanNdugu GIPAMA,